TIGO NA NMB WAANZISHA USHIRIKIANO.

Na Karoli Vinsent
     
          KAMPUNI ya Simu za Mkononi nchini ya Tigo kwa kushirikiana Benki ya NMB  leo wamezindua huduma mpya  ya kifedha ambayo itawalahisishia wateja wa Benki ya NMB pamoja na watumiaji wa mtandao wa Tigo katika kutoa na kuweka Fedha kutumia simu ya mkononi.
         
       Uzinduzi huo ulifanyika  leo Jijini Dar es Salaam na kushudiwa na Waandishi wa Habari Pamoja viongozi wa juu Benki ya NMB na kampuni ya simu ya Tigo ,Akizungumzia Faida za huduma hiyo Meneja wa Banki ya NMB ,Tom Borghol alisema huduma hii italeta mapinduzi ya Banki Nchini na kukuza hali za maisha kwa wateja wa Banki hiyo pamoja na wateja wa Tigo.
      ENDELEA HAPA---------

       “kupanuliwa kwa huduma hii ya kuweka fedha na kutoa fedha kwa njia ya Simu itawasaidia wateja zaidi ya milioni moja waliojiunganisha na NMB mobile kwa sasa, mteja wa Nmb anaweza kutoa na kuweka pesa kwa Wakala wa tigo pesa”alisema Borghol
Ikumbukwe kwa sasa kuna Mawakala wa Tigopesa zaidi ya 20000,waliotapakaa Tanzania nzima pamoja na pemba na Zanzibar
       
      Mr Borghol alisema kwa huduma hii mpya ya kutoa na kuweka Fedha kwenye Banki ya Nmb imetokana uhusiano mzuli uliopo kati ya Banki ya Nmb pamoja Mtandao wa Simu za Mkononi Nchini wa Tigo na kuwepo kwa huduma hii itasaidia kukuza uchumi wa nchi ya Tanzania na pia itarahisisha kwa wateja kutuma pesa kwenda vijijini.
       
         Kwa upande wake Meneja Biashara wa Tigo Pesa, Ruan Swanepoel alisema huduma hii iliyozinduliwa ni miongoni mwa mikakati inayofanywa na kampuni hiyo ya simu hapa nchini katika kuwajali wateja wake.
     
     “Huduma hii tulioizindua leo ni huduma bora sana na itawaondorea adha waliokuwa wanaipata wakati wa kutoa fedha kwenye Banki, lakini kuwepo kwa huduma hii sasa Mteja wa Banki ya Nmb atatumia simu yake ya mkononi kutoa fedha na kuweka fedha”
     
       “Uzinduzi wa leo ni mwenderezo wa kampuni hii simu katika kuwajali wateja wake na sasa tumeamua kuwasogezea huduma ya kibenki kwenye simu zao za mkononi”alisema Swanepoel.

       
       

Kuhusu kujiunga huduma hii,kwa mteja anayetaka kutuma pesa  kutoka kwenye banki ya Nmb kwenda Tigo pesa *150*66# na kufuata maelekezo.na watakaotaka kutuma pesa kutoka kwenye Tigo pesa kwenda kwenye Banki ya Nmb *150*01# na kufuata Maelekezo.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.