Thursday, February 13, 2014

WABUNGE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA WAPIGWA MSASA LE JIJINI DAR.SHIVJI AWAPA SOMO,SOMA HAPA

PRF ISSA SHIVJI AKIWA SEMINA HIYO INAYOFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM
Na Exaud Mtei
       
          PROFESA Issa Shivji amesema Rasimu ya pili ya Katiba ilitakiwa ijadiliwe  kwanza na wananchi katika mihadhara au mikutano ndipo mapendezo yao yangepelekwa bungeni ili wajumbe wayapitishe huku wakielewa wananchi wanachokitaka.
        ENDELEA NAYO----------------------

        Pia amesema wajumbe wa Bunge la Katiba kutoka katika asasi mbalimbali walitakiwa wachaguliwe na wananchi badala ya ilivyofanyika sasa kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete.
      
           Profesa Shivji ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kwanza wa kigoda cha Mwalimu Nyerere aliyasema hayo Dar es Salaam leo  wakati akitoa mada kwenye mkutano wa mafunzo kwa wajumbe wapya wa Bunge maalum la Katiba.
     
        “Kabla ya Rasimu hii kujadiliwa na wajumbe wa Bunge maalum la Katiba ilitakiwa wananchi nchi nzima waijadili kwanza na kutoa maoni yao.
    
      “Maoni hayo ndiyo yangewapa ufahamu wajumbe wa bunge hilo kuwa Tanzania wanataka Katiba ya namna gani,”alisema Prof. Shivji.
       
       Akizungumzia kuhusu namna watakavyofanya kazi hiyo alisema Rasimu siyo msaafu ambao hauwezi kubadilishwa chochote na kwamba wanaweza kuingiza mapendekezo mapya iwapo kuna haja ya kufanya hivyo.
       
       “Msije mkaingia pale mkavunja nchi yetu, Sawa Rasimu tunayo tume imekusanya maoni lakini hayawezi kutengeneza Katiba,”alisema.
          
        Wakati huo huo baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka taasisi za kiraia wameonesha mpaka sasa hawaelewi watakwenda kuzungumza nini au kama wananchi kwa sasa wakiwahoji hawana majibu ya msingi ya kuwapa.
                
WABUNGE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA WAKISIKILIZA KWA MAKINI
               Dk  Zainabu Gama wakati akichangia hoja kwenye mkutano huo alimwomba Prof. Shivji wawafafanulie zaidi wajumbe hao kuwa nini watakwenda kusema nini pia ikiwezekana awatumie  mada alizokuwa akiwafundishia hata kama ni kupitia mndao ili ziwajengee  uwezo.




No comments: