BABA AMNYONGA MWANAE MWENYE UMRI WA MWAKA MMOJA NA MIEZI SABA KISHA KUACHA UJUMBE TUTAFUTE PESA KWANZA NIITE J.M A.K.A GAIDI

DSC00361
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI  
 
MTOTO MWENYE UMRI WA MWAKA MMOJA NA MIEZI SABA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA HENRY JUMA MKAZI WA MIGOMBANI ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUNYONGWA SHINGO KISHA KULAZWA KITANDANI NA BABA YAKE MZAZI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JUMA VENANCE.
 
TUKIO HILO LA KUSIKITISHA LIMETOKEA MNAMO TAREHE 22.03.2014 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO KATIKA KATA YA MIGOMBANI, TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA AMBAPO BAADA YA UHALIFU HUO, MTUHUMIWA ALIFUNGA MLANGO KWA NJE NA KUFULI NA KUTOKOMEA MAHALI KUSIKOJULIKANA. WAPELELEZI PAMOJA NA RAIA WALIPOVUNJA MLANGO NA KUINGIA NDANI WALIKUTA MAITI YA MTOTO HUYO IKIWA KITANDANI. KATIKA CHUMBA HICHO WALIKUTA UJUMBE WA MANENO MENGI YALIYOANDIKWA NA MTUHUMIWA, BAADHI YA MANENO HAYO NI “UNYAMA UNYAMANI, TUTAFUTE PESA KWANZA NIITE J.M A.K.A GAIDI”. JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
 
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.