BUNGE LA KATIBA VURUGU MTINDO MMOJA,SITTA ALIAHIRISHA HADI KESHO

sita
Bunge maalum la katiba Limekutana Jioni Hii kuendelea na Shuguli zake Lakini Mvutano Mkubwa Umejitokeza Hali iliyosababisha Vurugu Iliyoambatana na Kuzomea Zomea,Mvutano Huo Uliibuka  Pale Mjumbe Mh. Tundu Lissu  Aliposimama kuomba Muongozo Kuhusu Marekebisho ya Kanuni Ambayo anamtuhumu Mwenyekiti wa Bunge  Mh Samweli Sitta  Kupitia Kamati ya Uongozi kuleta Marekebisho Ya Mabadiliko ya kanuni Kinyume cha Kanuni zilizopitishwa na Bunge Hilo la Katiba Wakati wakijadili na Kupitisha Kanuni za Bunge Hilo.
Mwenyekiti wa Bunge Hilo Mh Samweli Sitta Aliingilia Kati kujaribu Ufafanuzi  Pamoja na Wajumbe Wengine Akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mh  Jaji Fredrick Werema  Lakini hali ya Kuzomea Iliendelea Ndipo Mwenyekiti wa Bunge Hilo Alipolazimika Kuliahirisha Bunge Hilo Mpaka Kesho na Kuamuru Mapendekezo ya Mabadiliko HayoMabadiliko hayo Yapelekwe kwenye Kamati Ya Kanuni Kajili ya Maamuzi ili Yaweze Kuwasilishwa Katika Bunge Hilo.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.