.

MTEJA WA NBC TANZANIA AKABIDHIWA ZAWADI YA GARI LEO,NI KATIKA KAMPENI YA WEKA UPEWE.SOMA ZAIDI


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Bi Mzinga Melu (kushoto) akikabidhi zawadi ya gari jipya aina ya Suzuki Swift kwa Bi. Mary Malifedha Popote mkazi wa Kigoma, aliyeibuka mshindi wa zawadi kubwa ya promosheni ya Weka Upewe iliyokuwa ikiendeshwa na NBC. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jijijini Dar es Salaam jana. Wengine kutoka kulia ni Mkuu wa Huduma za Rejareja za Kibenki wa benki hiyo, Mussa Jallow, Mkuu wa Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa, Andrew Massawe na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Bi. Mwinda Kiula Mfugale. Gari hilo lina thamani ya dola za kimarekani 17,000.   
Na Mwandishi Wetu.

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imekabidhi zawadi ya gari jipya aina ya Suzuki Swift kwa mshindi wa kampeni ya Weka Upewe iliyomalizika hivi karibu kwa mkazi wa Kigoma B. Mary Malifedha Popote jijini Dar es Salaam jana.

Akizungumza wakati akikabidhi gari hilo lenye thamaninya dola za kimarekani 17,000, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bi. mizinga Melu alisema, kama benki wamefurahi kuona kampeni hiyo ikimadiisha maisha ya wasindi 13 waliobahatika kujishindia zawadi mbalimbali.

"Tunaamini zawadi hii gari itamsaidia huyu mteja wetu kubadilisha maisha yake kwani itamsaidia kupunguza kero za usafiri au kulitumia kama njia ya ku uongezea kipato", alisema.

Naye Mkuu wa Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa wa NBC, Andrew Massawe alisema kampeno hiyo iliyokuwa ikiwashiriksha wateja wao wenye akaunti ya Malengo imepata mafanikio makubwa kutokana na muitikio kutoka kwa wateja wao.

Alisema kila mteja aliyekuwa na kiasi cha shs 50,000 au kuweka kiasi hicho cha fedha  katika akaunti yake ya Malengo aliweza kuingia katika kampeni ambayo washindi walishinda zawadi mbalimbali kama pikipiki, jenereta za umeme na zawadi hiyo kubwa ya gari.

"Kampeni ya Weka Upewe imepata mafanikio makubwa kwani tumeshuhudia wateja wengi wa akaunti ya malengo wakiongeza amana zao na wengine kujiunga, muda si mrefu tutakuja na kampeni nyingine kabambe zaidi ili kuwafanya wateja wetu wafurahi kuweka fedha zao katika benki yetu", alisema.

Naye mshindi aliyejinyakulia gari hilo Mama Mary Malifedha Popote alisema anaishukuru sana Ben ya NBC kwa zawadi hiyo kwani hakuweza kutegemea yeye mkazi wa maeneo ya vijijini huko Kigoma kushinda.

"Naishukuru sana benki na natoa wito kwa wananchi wengine wajiunge na NBC kwani hawana upendeleo na huduma zao ni bora",alisema.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.