.

TIGO YAJITOSA KUDHAMINI MAONYESHO YA WAFANYA BIASHARA COCO .SOMA


Afisa mahusiano wa kampuni ya tigo tanzania JOHN WANYANCHA akizungumza na wanahabari leo jijini dar es salaam

       Tigo Tanzania leo imetangaza udhamini wake kwa maonyesho ya biashara yajulikanayo kama ‘Kariakoo @ Coco Beach Shopping Festival’ yenye malengo ya kuinua biashara za wafanyabiashara kutoka Kariakoo.

        Akitangaza udhamini huo kwa waandishi wa habari kutoka ukumbi wa Coco Beach jijini Dar es Salaam, Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha, alisema maonyesho hayo ambayo yatafanyika kila mwisho wa mwezi yana malengo ya kuleta bidhaa zenye gharama nafuu kutoka Kariakoo mpaka ufukwe wa bahari wa Coco kwa ajili ya kuwaondolea wateja usumbufu wa kwenda mpaka mjini na kero ya msongamano wanayoipata wakiwa huko.

        “Ukiondoa mazingira mazuri ambayo maonyesho haya yatawapatia wateja, pia tunaamini ya kwamba kupitia maonyesho haya wafanyabiashara wakati na wadogo wote watafaidika na kutokana na wateja watakaokuja kununua bidhaa zao, hivyo kuwasaidia kuongeza mauzo yao na hatimaye kukuza biashara zao,”alisemaWanyancha.

         Wanyancha aliendelea kusema kwamba wauzaji na wanunuzi watapata urahisi wa kuuza au kulipia bidhaaa huduma mbalimbali kupitia Tigo Pesa na kwa gharama ileile ya bila makato yoyote.

        Kutoka na na maelezo ya waandaji wa maonyesho hayo, Hazina Capital, uzinduzi utafanyika Jumamosi na Jumapili wikendi ijayo ya tarehe  29 na 30 Machi 2014, na kufuatiwa na maonyesho kama hayo yatakayofanyika kila wikiendi ya mwisho wa mwezi.

meneja wa mradi wa hazina capital RECHO NDAUKA akizungu mza

          Ndauka alisema maonyesho yataambatana na burudani mbalimbali wakiwemo wasanii wa kizazi kipya,Sanaa za kitamaduni na michezo mbalimbali kwaajili ya watoto. Tukio hili la kifamilia linatarajiwa kuwa desturi ya kitaifa katika kufanya ununuzi wabidhaa kwaofa kabambe kabisa kila mwezi kuanzia Machi 2014.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.