Monday, July 7, 2014

AZAMTV YAPELEKA MAWAKALA WAKE BRAZIL KUSHUHUDIA KOMBE LA DUNIA

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Rhys Torrington (kulia) akikabidhi tiketi kwa mawakala waliochaguliwa kwenda kushuhudia michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea Brazil ambapo anaemkabidhi ni Hasham Lardhi wa kampuni ya  SS Hassan, huku nyuma yake ni Al-Farham Dewji wa kampuni ya Regal Solar na anaengali mwenye fulana ya bluee ni Jacob Mwalyolo wa kampuni ya Maranatha Electronics ya Mbeya (Picha na Mpigapicha Wetu)
MAWAKALA watatu wanaojishughulisha na mauzo ya visimbuzi vya AzamTV wamesafiri kuelekea Brazil kushuhudia michuano ya Kombe la Dunia.
Mawakala hao ni pamoja na Hasham Lardhi wa kampuni ya SS Hassan, Al-Farham Dewji wa kampuni ya Regal Solar ya Dar es Salaam na plus Jacob Mwalyolo wa  Maranatha Electronics ya Mbeya.
Washindi wakiwa katika picha ya pamoja
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisa Operation Mkuu wa Azam Media alisema kuwa kampuni hiyo inatambua mchango wa mawakala wake katika kuendeleza biashara ya visimbuzi hivyo.

Alisema kuwa watakaa Brazil kwa siku kumi kuanzia tarehe 4 mwezi huu na watapata nafasi ya  kuangalia mechi hiyo ya nusu fainali itakayofanyikia  Belo Horizonte, Julai 8.


Alisema kuwa tangia kuanza kwa biashara ya visimbuzi vya AzamTV mawakala hao wamefikia kiwango cha juu cha mauzo ya huduma kwa wateja wa Azamtv.
Casse alisema kuwa wakiwa nchini humo watatembelea miji kadhaa kama vile Rio de Janeiro na Belo Horizonte.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Rhys Torrington alisema kuwa kwa kipindi hiki cha michuano ya kombe la dunia mauzo ya visimbuzi vyake yamekuwa makubwa.

Alisema kuwa kwa kutambua mchango wa mawakala katika kufanikisha mauzo ya visimbuzi vya AzamTV kampuni hiyo itaendelea kuwazawadia mawakala wote watakaokuwa wakifanya vema.

“Mafanikio yamekuwa makubwa kabisa tangu tumeanza biashara hii ya kuuza visimbuzi mnamo Desemba mwaka jana na kutokana na mchango wa makawala tumejitaidi kufanya vema sokoni”.


“Tunawashukuru sana  Azam Media pamoja na mtandao mzima wa biashara ya Bakhresa bila kumsahau Eric  Casse ambae tumekuwa tukifanya kazi naye bega kwa bega kuhakikisha tunafikia malengo yetu kwa ujumla"; kwakweli hii ni safari ya kipekee katika maisha yetu na tumefurahi sana kupata nafasi ya kwenda kushuhudia kombe la dunia nchini Brazil, hakika hii ni ndoto iliyokamilika”…kwa pamoja walisema mawakala hao waliobahatika kupata nafasi hiyo.

No comments: