CHAMA cha Walimu nchini (CWT) kimesema
kitapinga kwa nguvu zake au kuitisha mgomo wa walimu nchi nzima,endapo kama
serikali itapitisha sheria ya mpya ya Kupunguza mafao ya wastaafu wanachama wa
Mifuko ya pesheni ya watumishi (PSPF) na watumishi wanachama wa LAPF.
Tishio hilo limetolewa Leo Jijini Dar
es Salaam,na Rais wa Chama cha Walimu (CWT) Gratian Mukoba wakati wa Mkutano na
Waandishi wa Habari,ambapo alisema chama hicho baada ya kupata pendekezo kutoka
Wizara ya Kazi na Ajira kwa kushirikiana na Mamlaka ya mifuko ya Jamii (SSA)
khusu punguzo hilo kwa watumishi wa umma ikwemo walimu.
Ambapo chama cha walimu katika kikao
chake cha kamati ya utendaji ya Taifa(KUT) kilichokaa mjini Morogoro
walijadili pendekezo hilo na kuja maamuzi ya kupinga kwa nguvu zote mpango huo
ambao unalenga kuwadhulumu walimu pamoja wafanyakazi wengine mafao ya kustaafu
kama utapitishwa kutungiwa sheria.
Mukoba,alizidi kusema
mpango huo ukipitishwa na kuwa sheria utapunguza kinua mgongo cha walimu na
watumishi wengine wa umma.
“Hatuwezi kukubali mpango huu,kwani
utazidi kumfanya mwalimu awe masikini zaidi,mpango huu utamaliza kiiunua mgongo
cha walimu,kwani zaidi ya nusu kile wanachokipata kwa sheria iliyopo
sasa,wakati wanajua watumishi hawa wanaishi katika hali ya umasikini wa
kutisha”alisema Mukoba.
Mukoba ambaye kitaaluma ni
Mwalimu,aliyataja maeneo hayo ambayo watayapinga kwa nguvu zote ikiwemo
Kupunguza malipo
ya Pesheni ya mkupuo yanayolipwa na mifuko ya PSPF na LAPF kutoka asilimia 50
ya sasa hadi asilimia 33.3 ya mshahara wa mwezi wa Mtumishi kabla ya
kustaafu,
Vilevile alizidi ya
kuyataja maeneo mengine ni kupunguza makadirio ya Umri wa kuishi kwa
mwanachama baada ya kustaafu toka miaka 15.5 baada ya kustaafu hadi miaka 12.5,
Katika hatua nyingine chama hicho cha
walimu kimesema wamegundua sababu ya Serikali kufanya Rafu hiyo mbaya kwa
Watumishi wa umma ni kutokana na Serikali kudaiwa pesa nyingi sana.
“Tumechunguza
tumegundua sababu ya Serikali kuendelea kuwakandamiza watumishi hawa wa Umma ni
kutokana na serikali zaidi ya Trilioni 7,”
“Kwa pamoja tunaiomba sana serikali
isitishe mpango huu wanaotaka kuleta,na kama wanatafuta njia nyingine kuiokoa
mifuko hii,basi watafute njia nyingene”alisema Mukoba
No comments:
Post a Comment