KILE kinacho tafsiliwa kwamba
wapambe wa waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa wameanza kumgeuka na kuanza
kujiondoa katika harati zake za kuchukua usukani wa Juu wa uongozi wa nchi
kwenye uchaguzi mkuu mwakani 2015 ndani ya CCM,zimeanza kuonekana Mtandao huu
umebaini.
Mtandao huu umedokezwa kwamba aliyekuwa
mpambe wa kiongozi huyo Edward Lowassa,ambaye ni aliyekuwa Katibu Mkuu mstaafu wa Chama cha Mapinduzi
CCM,Yusuf Makamba tayari amejitoa kwenye kundi la kumpigania Waziri mkuu huyo
aliyejiuzuru.
Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika
ambazo mwandishi wa Mtandao,amezipata zinasema awali Mzee Makamba alikuwepo
katika upande ambao ulijitosa kuhakikisha Lowassa anachukua Urais katika
uchaguzi mkuu mwakani 2015,lakini sasa ameamua kujiondoa.
Chanzo hicho makini kinasema sababu ya
Katibu huyo wa Mstaafu wa CCM,kujiondoa ni Kutokana na Mwanae January
Makamba,ambaye tayari ametangaza nia y a kuwania nafasi hiyo Urais na tayari baadhi ya watu wameanza
kumuunga mkono kutokana na uamuzi wake wa kujitosa katika nafasi hiyo.
January makamba ambaye ni Naibu
waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,alitangaza uamuzi huo wiki
iliyopita wakati akifanyia mahojiano na Shirika la Utangazaji la BBC,aliitaja
nia yake kugombania nafasi hiyo ya Amiri Jeshi mkuu,na kusema sasa ni wakati wa
Vijana kushika nafasi hiyo.
Mtoa taarifa huyo aliuambia mtandao
huu kwamba Mzee Makamba tayari amejitoa katika
upande wa Lowassa na ameacha pigo kwenye
harakati hizo.
“Sikufichi hizo taarifa ni za kweli
mpambe mwenzetu tuliyekuwa naye wakati
tukipigania mzee wetu huyo lowassa kuingia ikulu,eti naye amejitoa na kuanza
kumsapoti mwanae Janury makamba,ambaye naye ameanza kukubalika kiasi chake kwa
watu mbalimbali ikwemo wachambuzi wa kisiasa”
“Na hili nakuhakishia ni pigo kubwa sana
kwa Mzee wangu Lowassa kwasababu nafasi aliyekuwa anaifanya ni kubwa sana
katika harakati hizo ndugu”alisema mtoa taarifa huyo.
Naye Mjumbe Halmashauri kuu ya chama
cha Mapinduzi CCM NEC,kutoka mikoa ya Kanda za juu kusini aliyezungumza na
Mwandishi wa Mtandao huu kuhusu hali
hiyo,kwa sharti la kutoandikwa Jina mtandaoni alisema lowassa anawakati mgumu
sana katika harakati zake kwani tayari nguvu yake kwa kundi lake inaanza kumeguka.
“Mzee yusufu Makamba tayari amejiondoa sasa katika upande wa kundi la
lowassa .sasa utagemea nani anaushawishi katika kundi la lowassa,kwa hili
tusitegemee jipya kwenye Nafasi yake,hebu ona jinsi anavyopigwa vita na kila
Kada wa CCM,”alisema Mjumbe huyo.
Kwa upande wake Msomi wa Masula ya
Kisiasa kutoka chuo Kikuu Dodoma,Seiph Yahaya alisema waziri mkuu aliyejiuzuru
Edward Lowassa anawakati mgumu sana kuingia Ikulu kwani kila msaka urais
anayeibuka anampinga yeye ,na kwa mtazamo huu chama cha CCM,uwenda kikapasuka vibaya wakati
wa kumteua mtu anatakayeshika nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu mwakani 2015.
No comments:
Post a Comment