.

EXCLUSIVE--SINEMA YA UKAWA NA CCM INAENDELEA,HAYA NDIO YANAYOENDELEA SASA


Na  Karoli Vinsent

         HUJUMA zinazodaiwa kufanywa na viongozi wa chama cha mapinduzi CCM kwenye mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya na kupelekea  Wajumbe wanaounda umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA kususia vikao vya Bunge la Katiba ,sasa hali hiyo  imeanza kuwa chungu kwa viongozi hao  Mtandao umebaini.

     
          Vyanzo vya Uhakika  kutoka ndani ya chama cha Mapinduzi CCM, zinasema chama hicho kinafikilia kuukubali muundo wa Serikali tatu ambao unatokana na Rasimu ya maoni ya wananchi,kuachana na Rasimu ya kipropaganda ya chama hicho inayozungumzia muundo wa Serikili mbili.
       

        Chama hicho kikongwe kulichopo kusini mwa jangwa la Sahara ambacho kipo madarakani,kimeamua kulegeza kamba na kufuata maoni ya wananchi kutokana na kupata shinikizo kubwa kutoka kwenye Madhehebu ya Dini nchini pamoja msimamo mkali uliowekwa na Muungano wa Kutetea Katiba ya Wananchi,UKAWA.
      
         Licha ya Rais Jakaya Kikwete,kutumia kila njia ili wajumbe kutoka UKAWA,kurudi kwenye bunge la Katiba,kwenye vikao vyake vinavyotarajiwa kuendelea tena mwezi ujao,kugonga mwamba baada ya kumtumia msajili wa vyama vya kisiasa nchini Jaji Francis Mutungi,ambaye ameonekana kushindwa kazi hiyo ya kuwashawishi warudi kwenye bunge hilo lilokuwa likibeza maoni wananchi.
      
      Kwa mujibu wa mjumbe wa kamati kuu ya CC kutoka CCM,anasema”kwa hali iliyopo kwa sasa hakuna jinsi lazima tukubali muundo wa serikali tatu ambao umetokana na maoni ya wananchi,kwani tumemshauri mwenyekiti wetu Rais Kikwete, akubaliane na hawa wajumbe wa UKAWA,kwani  serikali tatu  ndio kila kitu”alisema mjumbe huyo wa juu kamati ya chama cha mapinduzi ya ccm.
         
          Mwandishi wa mtandao huu  amedokezwa,Rais Jakaya Kikwete tayari ameipiga chini kauli yake aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Vikao vya Bunge la Katiba,ambayo alitoa maelekezo kwa wajumbe wa Bunge hilo wakubaliane na muundo wa Serikali tatu na kupiga chini maoni ya Wananchi.
        
         Ambapo Rais Jakaya Kikwete tayari  amekutana Faragha na wajumbe wanaunda Umoja wa katiba ya Wananchi UKAWA,ikulu jijini Dar Es Salaam ili kupata mwafaka juu ya kukwamua mchakato wa katiba ambao aliuvuruga mwenyewe.
        
          Chanzo hicho kilisema Mkutano kati ya Rais kikwete na Mjumbe mwandamizi wa UKAWA,mkutano huo ulifanyika usiku wa wiki iliyopita kutokana na ombi la Rais .wito wa Rais Kikwete kwa UKAWA ulifanyika kwa njia ya Simu.
      
         Kuhaha huku kwa Rais Kikwete kuukwamua mchakato huu kumekuja baada  siku mbili tangu Halmashauri kuu ya 48 bya jumuiya ya kikristo Tanzania (CCT)iliyokutana tarehe 2 na 3 mwaka huu ,kuelekeza waumini  wake kupigania kuwepo serikali tatu ambayo inapingwa vikali na CCM,
         
            Duru za Kisiasa zinasema mwenye uwezo wa kukwamua mchakato huu wa katiba ni Rais Jakaya Kikwete ambaye ndio aliuharibu mwenyewe,licha ya Jitihada alizofanya mwenyekiti wa Bunge la katiba, waziri Sitta kutumia nguvu zake zote kuwasihi wajumbe hao wa UKAWA wanaotetea maoni ya Wananchi kurudi Bungeni.
          
           Teyali wajumbe hao wa UKAWA wakiwa wametoa sharti moja tu ili wajumbe hao waweze kurudi kwenye vikao vya bunge la katiba ni kwa Wajumbe wa chama cha Mapinduzi CCM,kuacha kujadili Rasimu ya kwao badala yake wajadili Rasimu iliyotokana na Maoni ya wananchi.ambacho sharti hilo limekuwa ngumu sana kwa chama hicho kubaliana na hali hiyo.
           
         Duru hizo zilisema kama Rais Jakaya Kikwete akishindwa kukwamua mchakato huu wa Katiba basi atakuwa amejiharibia katika Nyanja mbalimbali za Siasa nchini,endapo akiondoka madarakani mwakani mwezi wa kumi,na kujijengea sifa mbaya ya kiongozi aliyepelekea nchi kupoteza mabilioni ya fedha kwenye mchakato wa katiba ambao aliuharibu mwenyewe kwa kauli zake.


About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.