.

HABARI ILIYOTIKISA JIJI LEO--WAZIRI NYALANDU ACHARUKA,AFUTA KAMPUNI MOJA YA UWINDAJI,SOMA SABABU HAPA

Na Karoli Vinsent
         
LICHA ya kushutumiwa kwenye Magazeti mbalimbali hapa nchini kwa kushindwa kudhibiti vitendo vya Ujangili,Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu sasa amekuwa  Mbogo Baada ya leo kufuta Leseni ya Kampuni ya Uwindaji  Green Miles Safaris Limited (GMS) kutokana na kufanya vitendo vya kinyama kwa Wanyamapori.

         Uamuzi huo Umetangazwa Muda huu, Jijini Dar es Salaam,na Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu,wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari,ambapo amesema amefikia uamuzi huo, kutokana na kuridhishwa na ushahidi kuhusu kampuni hiyo kufanya vitendo vya kuwatesa wanyama pori.

           “Kwanzia sasa nimefuta leseni na kuamuru iache kabisa kazi ya uwindaji hapa nchini kampuni ya uwindaji  Green Miles Safaris Limited(GMS) kutokana kukiuka sheria za uwindaji hapa nchini kutokana kufanya kinyume na sheria ikiwemo kuwatesa wanyama pamoja na kuwakimbiza ambapo inapelekea wanyama kuchoka na kuteseka hadi wengine kufa“alisema Nyalandu.


         Waziri Nyalandu amesema  Kampuni hiyo ya Uwindaji ilikiuka sheria hiyo ya Uwindaji kutokana na kuzidi kuwatumia watoto wadogo chini ya miaka 18 kwenye shughuli za Uwindaji ambapo ni kinyume na taratibu,vilevile waziri huyo alisema ushahidi wizara yake aliotumia kutoa hukumu hiyo inaonyesha wazi jinsi kampuni hiyo inavyouwa wanyama kikatili,pasipo sababu ya msingi na kupelekea wanyama hao kupungua katika mbuga zetu.

      Aidha,Waziri Nyalandu alisema hajatumia upendeleo wowote katika kuinyanganya Leseni kampuni hii ya uwindaji,  Green Miles Safaris Limited,ambayo kampuni hiyo inayomilikiwa na Mtanzania anayeitwa Salum Awadh,kutoka na kuunda tume ya watu wailiobobea katoka Wizara hiyo kwenda kuichunguza kampuni hiyo,

         “Nataka niseme kitu kimoja maamuzi haya yako sahihi,kwani hatuja tumia upendeleo wowote kutokana na mimi kuunda tume ya watu waliobobea kutoka Wizara yangu kwenda kuichunguza kampuni hii pamoja na kazi yake,na katika uchunguzi wetu tumewashirikisha hata wao wa Kampuni hii”alisema Nyalandu.

        Ikumbukwe  Maamuzi haya Aliyotoa Waziri Nyalandu,yamekuja siku chache Baada ya Waziri Kivuli wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Mchungaji Peter Msigwa kutoa ushahidi wa mkanda wa Video kuhusu vitendo viovu vinavyofanya na  kampuni ya Green Miles Safaris Limited GMS,

       Msigwa,ambaye ni Mbunge wa Iringa Mijini CHADEMA alisema Pamoja na ukiukwaji wa Sheria ya Wanyamapori ya mwaka 2009 ambao kampuni hiyo imekuwa ikiufanya, Serikali imeshindwa kuwachukulia hatua. Suala hili linadhihirisha moja ya hoja zetu kuhusu sababu za ujangiri unaozidi kushamiri hapa nchini kuwa ni kuwepo kwa makampuni mengi ambayo yanamiliki vitalu vya uwindaji kwa mgongo wa wazawa huku ukweli ukiwa ni kwamba umiliki wa vitalu vingi vya uwindaji nchini upo kwenye mikono ya wageni na Serikali imeshindwa kuchukua hatua zozote.

Kutokana ubutu wa Serikali hii katika kusimamia rasilimali zetu, kuzuia uwindaji holela, unaokuza ujangili na kutishia hatma ya maliasili na utalii nchini, Kampuni ya Green Miles Safaris, kama inavyoonekana kwenye picha za video, imekiuka Kifungu Namba 42 cha sheria ya wanyamapori ya mwaka 2009, ambacho kinaeleza kuwa mtu yeyote atakayemjeruhi mnyama atatakiwa kutumia juhudi zote kadri ya uwezo wake kumuua mnyama huyo ndani ya muda mfupi iwezekanavyo.

      Aidha,Msigwa aliyataja makosa yanayofanywa na kampuni hiyo ambayo ni 
Mosi, Kampuni ya Miles Safari Limited imekuwa ikiwakimbiza na kuwakamata watoto wa wanyamapori pindi wanapozaliwa kinyume na kifungu cha 19 (1) cha sheria ya wanyamapori ya mwaka 2009.

Pili, kampuni hii ilishapewa zuio na mahakama la kufanya uwindaji kutokana na uwindaji usiozigatia sheria. Hata hivyo kampuni hii kupitia mlango wa nyuma iliomba kibali cha uwindaji kwa Mkurugenzi wa wanyamapori na Mkurugenzi akatoa kibali hivyo kupuuza amri halali ya mahakama.

Tatu, kampuni hii imekiuka kifungu namba 24 (2) cha sheria ya uhifadhi wa wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009 kosa la kuwakimbiza, kuwasumbua na kuwajeruhi wanyama kwa magari. Kwani sheria inasema kuwa mtu yeyote hataruhusiwa kujeruhi au kusumbua wanyama yeyote anayehifadhiwa.

Nne, kampuni hii imekuwa ikiruhusu watoto chini ya umri wa miaka 18 kuwinda ndege ambao hawajaidhinishwa kuwindwa na watalii, tena watalii wasio na leseni. Katika ithibati yetu ya video mtoto chini ya miaka 18 ameonekana akiwinda ndege aina ya Tandawala mweusi na mweupe ambao hawajaidhinishwa kuwindwa na watalii wasio na leseni.

Tano, kampuni hii imekuwa ikiruhusu wateja wake kukamata watoto wa wanyama wadogo hususani pundamilia ambacho ni kinyume na kifungu namba 50 (1) inayosema kuwa mtu yeyote hataruhusiwa kukamata myama bila kibali halali cha kukamata wanyama.

Sita, kampuni imekuwa ikiruhusu wateja wake kupiga risasi wanyama hususani nyumbu wa kike, mtoto wa nyati na wengine kinyume na kifungu namba 56 inayokataza kuwinda au kuua watoto wa wanyama wowote.Saba, kampuni hii imekuwa ikiruhusu utumiaji wa silaha inayojiendesha yenyewe aina ya semi-automatic shortgun na silaha zilizowekewa vifaa vya kuzinyamazisha zisitoe mlio ambazo ni haramu ambapo ni kinyume na kifungu namba 64 (2) yenye zuio za silaha zisizoruhusiwa kutumika
                                                                               


About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.