Saturday, July 12, 2014

HABARI KUBWA LEO--BAADA YA WAZIRI NYALANDU KUFUTA LESENI YA KAMPUNI YA UWINDAJI JANA,MCHUNGAJI MSIGWA AIBUKA NA KUFUNGUKA TENA,SOMA ALICHOSEMA HAPA


Na Karoli Vinsent.

       SIKU moja kupita baada Waziri wa Maliasili na utalii ,Lazaro Nyalandu kuifutia Leseni ya Uwindaji Kampuni Green Miles Safari Limited(GMS) kutokana na
kuendeleza vitendo vya kutesa wanyama pamoja na kuvunja sheria za Uwindaji,

        Naye,Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii,Mchungaji Peter Msigwa,ameibuka na kumtaka Waziri Nyalandu kupitia Upya Kampuni zote za Uwindaji hapa nchini kwani nazo zimekuwa zikifanya kazi kinyume na sheria.

      Kauli hiyo ya Msigwa ameitoa Mda huu wakati alipokuwa anafanyiwa Mahojiano na Mwandishi wa Mtandao huu kwa Njia ya Simu kutoka Iringa,ambapo Mwandishi wa Mtandao huu alitaka kujua anachukuliaje Hatua iliyochukuliwa na Waziri nyalandu kufungia kampuni hiyo ya Uwindaji.


        Ndipo, Msigwa alisema ni mda umefika kwa Waziri Nyalandu kupita upya kampuni zinazofanya Ujangili hapa nchini kwani zimekuwa zikifanya kazi kinyume na taratibu.

       “Katika hili nampongeza kwa kuchuka Hatua,cha msingi namtaka asiishie kwenye Kampuni hii,inabidi kuyachukulia makumpuni mengine ya uwindaji, tena inabidi achunguze kwa makini kampuni zengine ambazo zimekuwa zinafanya ubabaishaji kwenye uwindaji hapa nchini”alisema Msigwa

        Mchungaji Msigwa,ambaye ni Mbunge wa Iringa Mjini CHADEMA,alimpongeza Waziri Nyalandu kwa kitendo chake cha kutoa itikadi zake za Chama na kuweka Maslahi ya Taifa mbele kwani suala la Uwindaji haramu linapaswa kupigwa vita na kila mtu mpenda maendeleo katika Taifa hili.
Katika Hatua nyingine Mwandishi wa Mtandao huu alipomtaka atoe ufafanuzi kuhusu Taarifa zinazoandikwa kwenye Magazeti mbalimbali hapa nchini .

       Kwamba kitendo chake cha kupinga kampuni hii iliyofungiwa ya  Uwindaji Kampuni Green Miles Safari Limited(GMS) inatokana na Yeye kufanya Njama ili Kampuni ya Wengbert Windrose Safari (WWS)inayomilikiwa na Wamarekani ipewe kitalu hicho cha Uwindaji kilichipo Ziwa Natrion?

       Msigwa akijibu kwa Hasira alisema anashindwa kuwaelewa Waandishi wa Habari wa nchi hii, kushindwa kujibu hoja ya yeye aliyoibua kuhusu unyama huo unaofanya na Kampuni hiyo uwindaji Green Miles Safari Limited(GMS).

       “Mimi ningetegemea Mwandishi makini wa Habari angeibuka nakupinga ushahidi ule na kujibu hoja kwamba niliyosema yana uongo au la kwamba Wanyama wale hawapigwi,lakini kusema kwamba mimi naipendelea kampuni hiyo sio za Kweli”

       “Kwahiyo kama wao wana ugomvi na Kampuni nyingine mimi hayanihusu,mimi hapa nazungumzia ukiukaji wa haki na kwamba kama ipo kampuni nyingine ikifanya kinyume na taratibu mimi nakufa nayo”alisema Msigwa.

      Mwandishi wa Mtandao huu alipotaka kujua kama hatayachukulia hatua zozote za kisheria Magazeti haya ambayo yamekuwa yakimshutumu kwamba amehongwa na kampuni hiyo ya Wengbert Windrose Safari (WWS)inayomilikiwa na Wamarekani ?

      Mchungaji,Msigwa ambaye ni Mwanasiasa Machachari kutoka Chadema alisema Hawezi kubishana na Watu waliokosa maana, yeye anakazi nyingi za kufanya.

      “Mwandishi kuna kazi nyingi sana za kufanya siwezi nikabishana na watu wasiojielewa kwani mtu akiandika kama mimi ni mwanamke harafu eti mimi nianze kubishana na mtu aliyeandika hivyo  wakati mimi ni mwanaume,mimi nawaacha waandike najua wataacha”

        “Mimi kukaa na Wajinga ambao wanatumiwa na watu binafsi ili waweze kukwamisha kasi yangu ya kulinda wanyama pori hapa nchini”alisema Msigwa.

         Mchungaji Msigwa ndiye mtu aliyeibua hujuma inayofanywa na Kampuni uwindaji Green Miles Safari Limited(GMS) kupitia mkanda wa Video ambapo msigwa alisema Kampuni hiyo imekuwa ikifanya uwindaji kinyume na taratibu.

        Ndipo,jitihada hizo za Mchungaji Msigwa zilimuibua Waziri wa Maliasili,Lazaro Nyalandu,na kuifutia Leseni kampuni hiyo,
Akisoma maazimia hayo jana mbele ya Waandishi wa Habari waziri Nyalandu alitaja makosa hayo kuwa ni wageni wa kampuni hiyo kuwinda wanyama ambao hawakuruhusiwa kwenye leseni ya uwindaji wakiwemo nyani na ndege, jambo ambalo ni kinyume na kifungu cha 19(1)(2).
Pili, wageni wa kampuni hiyo kuchezea watoto wa pundamilia na ngiri kinyume na kifungu cha (19)(1), wageni kufukuza wanyamapori kwa magari na kisha kuwapiga risasi wakiwa ndani ya magari kinyume na kifungu 65(1) (a) 1, kuwinda wanyama walio chini ya umri (watoto), kinyume na kifungu cha 56(1).
“Kuruhusu watoto chini ya miaka 16 kuwinda kinyume na kifungu cha 43(2) (a), na wageni kuwinda huku wakipiga kelele, jambo ambalo ni kero kwa wanyama na kinyume na kifungu cha 19(1) na (2),” alisema.
Nyalandu alikiri kampuni hiyo kuvunja sheria ya wanyamapori ya mwaka 2009, sambamba na kanuni za uwindaji, na kwamba kwa kuzingatia mamlaka aliyopewa chini ya sheria hiyo ya kuhifadhi wanyamapori No.5, amechukua hatua.
“Kwa kuzingatia matakwa ya kanuni ya 17(1), 8(2), nafuta umiliki wa vitalu vyote vilivyo chini ya Kampuni ya Green Miles Safaris Ltd, hii ikiwa ni pamoja na vitalu vya Lake Natron GC East, Gonabis/ Kidunda-WMA na MKI-Selous.

“Pia, hatua hii inafuta vibali vyote vya uwindaji vilivyotolewa katika msimu huu wa uwindaji na hii iwe onyo kwa kampuni za uwindaji wa kitalii nchini kuhusu ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu za uwindaji,” alisema

No comments: