Tuesday, July 22, 2014

HUU NDIO UKWELI KUHUSU VIUNGO VYA BINADAMU VILIVYOKAMATWA JANA BUNJU

Na karoli Vinsent

         JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewatoa Hofu wakazi wa Jiji hili,na kusema viungo vya binaadamu vilivyogundulika katika maeneo ya Mbweni Mpiji ni Vimetoka kwenye  Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (International  Medical and Technological University –IMTU,ambapo vilikuwa vikitumika katika kujifunzia na sio Maeneo mengine.


        Hofu imetolewa  leo na Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleman Kova wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari ambapo Alisema kuwa, Jeshi la polisi lilipokea taarifa 21 Julai mwaka huu, majira ya jioni kutoa kwa wasamaria wema na ndipo jopo la wapelelezi likiongozwa na Mkuu wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ACP Camilius Wambura kufika maeneo hayo majira ya jioni.

         “Katika hatua za awali baada ya kufika eneo la tukio waligundua mifuko 85 meusi yenye viungo vya aina mbalimbali vya binaadamu kama vile Vichwa, Miguu, Mikono, Mioyo, Mapafu, Vifua na Mifupa ya aina mbalimbali ya binaadamu”

      Alieleza kuwa, katika hali iliyoshangaza kuwa viungo hivyo havikuwa na uvundo wala haraufu ya aina yoyote na vilionekana kwamba vimekaushwa na kukakamaa.

         “Katika eneo hilo pia vilikutwa vifaa vinavyotumikaa hospitalini kama vile mipira ya kuvaa mikononi (gloves) mifuko miwili iliyotumika, nguo maalum (apron) zipatazo 20 na karatasi mbili zenye maswali ya kujibu”

         Alisema kuwa licha ya eneo la tukio kuwepo wananchi waasiopungua 1000 lakini hakuna  aliyekuwa na taarifa saahihi juu yaa sakata hilo.
“Viungo viliweza kuchukuliwa na kupelekwa Hospitali ya  Taifa ya Muhimbili na kufanyiwa uchunguzi, chini ya Jopo la Wapelelezi likiongozwa na Mkuu wa Upelelezi Kanda ya Maalum ACP Japhari Mohamed akisaidiana na Daktari wa Jeshi la Polisi anayehusika na miili ya binaadamu” alisema.

           Kamishna Kova alieleza kwamba, baada ya uchunguzi wa kina kufanyika ilibainika kwamba viungo hivyo kwa mara ya mwisho vilikuwa katika Maabara ya IMTU jijini Dar es Salaam.

        Katika hali nyingine isiyokuwa ya kawaida Kamishna Kova alisema, wananchi wa eneo hilo waliopata taarifa waliamua kulishikilia gari ndogo aina ya Canter ambalo lilikuwa limebebaa uchafu uliokuwa unatoa harufu kali na kulihisi kuwa limebeba mifuko mingine ilkiyokuwa na miili ya binaadamu.

        “Gari hilo lilibainika wazi kwamba halikuhusika na tukio hilo, pia tulipolipekewa ikagundulika limebeba mabaki ya kuku ikiwemo Utumbo, miguu, vichwa na manyoya pamoja na uchafu mwingine uliokuwa umeoza” alisema.

          Katika kuhakikisha unapatikana ushahidi wa kina Kamishna Kova alibahinisha kuwa Jeshi la Polisi litamuhusisha Mkemia Mkuu wa Serikali na baada ya kukamilika kwa uchunguzi jalaada litaapelekwa kwa Mwaanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua zake ili sheria ichukue mkondo wake.



No comments: