Sunday, July 20, 2014

MAADHIMIO MAZITO YA KAMATI KUU CHADEMA ILIYOKETI SIKU MBILI HAYA HAPA


Kamati  kuu ya chama cha dem
okrasia na maendeleo chadema kilifanya mkutano ndani ya siku mbili kuanzia tarehe 18 julai hadi 20 julai ikijadili na kufanya maamuzi kuhusu masuala mbali mbali yanayoikabili nchi yetu na chama chao kwa ujumla
Pamoja na hayo kamati kuu ilikuwa ikijadili ushiriki wa wajumbe wa CHADEMA kama sehemu ya umoja wa katiba ya wananchi UKAWA katika bunge maalum na mustakabali wa mchakato wa katiba mpya

Aidha  kamati kuu imepokea na kutafakari hali ya kisiasa ya nchi yetu kwa ujumla wake na hali ya kisiasa ndani ya chama chao ,uchaguzi unaoendelea katika ngazi mbali mbali  n ndani ya chama na masuala yote yanayohusu uchaguxi wa vijiji  na mitaa uliopangwa kufanyika  nchini baadae mwaka huu na kujadili taarifa ya fedha na mali za chama
MAAZIMIO JUU YA MCHAKATO WA KATIBA MPYA

CHADEMA kama sehemu ya UmojaWa Katiba Ya Wananchi UKAWA iendeleze mazungumzo na mheshimiwa Rais ambye ni msimamizi mkuu wa mchakato wa Katiba Mpya kwa upande serikali kuhusu namna ya kunasua mchakato huo ndani ya Bunge Maalum

Wajumbe wa Bunge Maalum wanaotokana na  CHADEMA kama sehemu ya UKAWA watarudi bengeni kwenye vikao vya bunge maalumendapo tu mamlaka ya benge hilo yatafafanuliwa kuwa ni ya kuboresha na sio kuibomoa au kuifuta misingi mikuu basic feature ya rasmu ya katiba mpya uiliyotokana na maoni ya ya wananchi na kuandaliwa na tume ya mabadilko ya katiba iliyoteuliwa na rais kwa ajili hiyo

Wajumbe wa bunge maalum wanaotokana na CHADEMA kama sehemu ya UKAWA watarudu bungeni endapo tu na baada ya ufafanuzi uliotajwa katika aya ya 2 utahusisha marekebisho ya kifungu cha 25 cha sheria ya mabadiliko ya katiba, sura 83,inayohusu mamlaka ya bunge maalum,pamoja na kanuni husika za bunge maalum

Wajumbe wote wa CHADEMA katika bunge maalum la katiba hawatashiriki katika kikao chochote cha bunge maalum au kamati zake hadi hapo ufafanuzi wa mamlaka ya bunge maalumuliotajwa katika aya za 2 au 3 utakapofanyika kwa mujibu wa maazimio ya kamati kuu

Endapo bunge maalum litapitisha rasmu ya katiba mpya isiyotokana na maoni ya wananchini kama yalivyoakisiwa kwenye rasimu ya katiba mpya iliyoandaliwa na tume,CHADEMA kama sehemu ya UKAWA ,itafanya kampeni nchi nzima kuwashawishi wananchi kuikataa katiba hiyo katika kura ya maoni

Kwa sababu yoyote ile,bunge maalum litavunjika kabila ya kupitisha Rasmu ya Katiba Mpya ,CHADEMA kama sehemu ya UKAWA itafanya mapambano ya kupata katiba mpya ya kidemokrasia kuwa sehemu kuu ya kampeni na operesheni zote za chama kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao na hata baada ya uchaguzi

MAAZIMIO KUHUSU HALI YA KISIASA NDANI YA CHAMA CHAO HAYA HAPA..................
Kamati kuu imekuwa ikipokea taarifa mbalimbali  za baadhi ya viongozi wa CHADEMA wa mikoa ya KIGOMA ,KATAVI,na TABORA hivyo kamati kuu ina taarifa za mipango ya ya viongozi wengi kuandaliwa kujiuzulu katika mikoa mingine kwa lengo la kutoa taswira potofu kwa umma kwa chama chao kinabomoka na kina migogoro mikubwa wa kiuongozi kufuatilia kufukuzwa kwa waliokuwa viongozi wa chama hicho na wajumbe wa kamati kuu ZITTO ZUBERI KABWE ,DkKITILLA MKUMBO,na SAMSON MWIGAMBA .Kamati kuu inafahamu kwamba mipango hiyo inaratibiwa na USALAMA WA TAIFA pamoja na CHAMA CHA MAPINDUZI CCM .
KUHUSU VIONGOZI WA MKOA WA KIGOMA WALIOJIUZULU Aliyekuwa mwenyekiti wa mkoa mzee JAAFAR KASISIKO,mwenyekiti wa Kanda ya Magharibi SHAABAN MAMBA,katibu wa mkoa MSAFIRI WAMALWA na katibu wa baraza la wanawake wa CHADEMA BAWACHA mkoa wa kigoma MALUNGA SIMBA wamekuwa kwenye uongozi wa chama katiks nafasi hizo kwa muda mrefu na katika kipindi hicho chote wameshindwa kukuza chama katika mkoa

Tangu mwaks 1993,chama kimekuwa na wabunge 1 tu wa kuchaguliwa kati ya wabunge tisa wa kuchaguliwa wa mkoa wa Kigoma.Kwa ulinganisho, chama cha NCCR-Mageuzi kimeongeza idadi ya wabunge wake wa kuchaguliwa kutoka sifuri mwaka 2005 hadi kufikia wanne mwaka 2019

Chama kimepunguza idadi ya madiwani wake katika Halmashauri ya wilaya ya Kigoma Vijijini kutoka madiwani watano mwaka 2005 hadi diwani mmoja mara baada ya uchaguzi mkuu 2010

Hii siyo mara ya kwanza kwa mkoa wa Kigoma kukabiliwa natatizo la vyama vya upinzani kusalitiwa na viongozi wao na kuchaguliwa kujiunga na CCM au kuwa mawakalawa chama hichoMifano ya nyuma ni pamoja na DK AMANI WALID KABOUROU aliyekuwa katibu mkuu na baadae kuwa makamu mwenyekiti wa CHADEMA na mbunge wa jimbo la kigoma mjini KIFU GULLAMHUSSEIN KIFU na DANIELNSANZUGWANKO waliokuwa wabunge wa majimbo ya kasulu na kigoma kusini kwa tiketi ya chama cha NCCR-Mageuzi.Wasaliti wote hao wa nyuma hawajawahi kuzima nguvu ya mageuzi katika mkoa wa kigoma na wasaliti wa sasa na wajao hawatazima nguvu hiyo


Kuhusu viongozi wa mkoa wa TABORA waliojuzulu katibu wa mkoa ATHMANI BALOZI mwenyekiti wa baraza la vijana wa CHADEMA BAVICHA wa mkoa HUSSEIN KUNDECHA na wengine katika uongozi wa wilaya kadhaa za mkoa huo hao pia wamekuwa katika uongozi wa chama kwa muda mrefu bila kuongeza tija yeyote kwa chama .Licha ya chama kutoa vifaa vya kazi kama vile magari kwa nkoa huo kwa muda mrefu


hata hivyo kamati kuu imewataka viongozi,wanachama ,wapenzi na mashabiki wa chama chao pamoja na wananchi kwa ujumla kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha mapambano makali dhidi ya chama chao kamati kuu itachukua hatua zote stahiki kuhakikisha kwamba kama ambvyo wasaliti na makawala wa CCM WA MIAKA MINGI YA NYUMA HAWAKUATHIRI KUKUA NA KUJIIMARISHA KWA CHAMA CHAO,WASALITI NA MAWAKALA WA CCM wa sasa na wasaliti na mawakala watarajiwa hawataweza kuathiri kukua na kujiimarisha kwa chama hicho katika kipindi hiki ambacho chama kinajiandaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2015

No comments: