MTANDAO huu bado unaendelea na
simulizi,juu ya kufungiwa kwa Gazeti mwanahalisi ambapo ifikapo tarehe 25 mwezi
huu wa saba mwaka huu linatimiza miaka miwli tangu lifungiwe na serikali kwa
mda usiojulikana.
Leo ikiwa ni siku ya pili ambapo
mtandao huu unazidi kukuketa simulizi juu ya kufungiwa gazeti hilo baada ya
jana kukupa historia fupi ya gazeti hilo pamoja na wamiliki wake na leo
tunatazungumzia habari iliyopelekea kufungiwa na serikali,.
Na leo tutaiweka habari
hiyo ambapo tutakupa mda wa kufikili na kesho katika sehemu ya tatu tutakuja
kuichambua habari hiyo na je ilikuwa inamakosa au la?
Na simulizi hii itafikia mwisho tarehe 25 mwezi huu ambapo gazeti hilo
linafikisha miaka miwili,
Habari yenyewe ni hiyo hapo
Aliyemteka
Ulimboka huyu hapa
Na Saed
Kubenea -
Ni Ighondu wa Usalama wa Taifa
RAMADHANI Ighondu, afisa wa Idara ya
Usalama wa Taifa (TISS), ndiye ametajwa kuwa mtekelezaji wa mkakati wa utekaji
wa Dk. Steven Ulimboka,MwanaHALISI limegundua.
Afisa
huyo, licha ya kutambuliwa na Dk. Ulimboka mwenyewe, ndiye simu yake ilitumika
kuandaa kikao ambako daktari alitekwa.
Ni
afisa huyohuyo wa usalama ambaye alikutana na Dk. Ulimboka dakika chache kabla
ya kutekwa.
Uchunguzi
umegundua kuwa Ramadhani Ighondu (34), ni mfanyakazi wa ikulu aliyekuwa
akifanya mawasiliano ya mara kwa mara na Dk. Ulimboka.
Ni
mfanyakazi huyuhuyu ambaye Dk. Ulimboka amenukuliwa akisema, “...alinipigia
simu na kuniita kwenye kikao ambako muda mfupi baadaye nilitekwa.”
Nyaraka
nyeti ambazo mwandishi ameona zinaonyesha kuwa Ramadhani ndiye pia huitwa
“Rama” – jina ambalo hutumia katika kujitambulisha na katika baadhi ya
mawasiliano.
Rekodi
katika simu ya Dk. Ulimboka: Na. 0713731610zinaonyesha Rama ndiye alifanya
mawasiliano ya mwisho na daktari huyo muda mfupi kabla ya kutekwa.
Aidha,
ni Rama ambaye alikutana na kiongozi huyo wa Jumuia ya Madaktari Tanzania,
maeneo ya Leaders Club, jijini Dar es Salaam, muda mfupi kabla ya kutekwa.
Dk.
Ulimboka alitekwa usiku wa 26 Juni, kusukumizwa kwenye gari, kupigwa, kufungwa
mikono na miguu, kunyofolewa kucha na kutolewa meno; na hatimaye kutupwa
katika msitu wa Mabwepande.
Rama
alifanya mawasiliano ya mwisho na Dk. Ulimboka saa 5: 52 kupitia simu yake Na. 0713
760473. Dokta alitekwa “muda mfupi” baadaye.
Rais
Jakaya Kikwete aliliambia taifa kwa njia ya televisheni, mwishoni mwa Juni,
kuwa serikali yake haihusiki na kuteka, kutesa na kutupa daktari porini.
Naye
Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliliambia bunge kuwa serikali yake haihusiki na
utekaji na utesaji; na kuuliza, “...serikali imteke ili iweje?”
Mawasiliano
katika simu ya Dk. Ulimboka yanaonyesha mtiririko wa simu za Rama wa ikulu hadi
muda wa kutekwa katika eneo la Leaders Club.
Vyanzo
vya taarifa ndani ya idara ya usalama wa taifa vinasema, kwa sasa Rama
“amehifadhiwa” kwenye jengo moja la kificho linalotumiwa na idara hiyo lililopo
eneo la Ada Estate, Kinondoni, Dar es Salaam.
MwanaHALISI limeweza
kuthibitisha, kupitia vyanzo vya taarifa na nyaraka mbalimbali kuwa, simu Na.0713
760473 iliyokuwa ikifanya mawasiliano ya mara kwa mara na Dk.
Ulimboka, ni mali ya Rama.
Huyo
ndiye Ramamadhani Ighondu (Rama). Mzaliwa wa Makole, Dodoma. Mfanyakazi wa
Idara ya Usalama wa Taifa (TISS). Idara hii iko chini ya Ofisi ya Rais (Utawala
Bora) inayoongozwa na Rashid Othman.
Gazeti
hili limepitia nyaraka mbalimbali, likiwamo daftari la kudumu la wapigakura
lililoandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ili kupata fununu zaidi juu
ya tuhuma za Dk. Ulimboka kwa Rama.
Katika
daftari hilo ambalo limetumika kwenye uchaguzi mkuu uliopita, Rama anaonekana
kujitambulisha kama ifuatavyo:
Ramadhani
Ighondu,
Nickname: Rama
Born: 28.08.1978
Place: Makole – Dodoma
Voter Registration Card: 49406879
Mobile Number: 0713 760473
Nickname: Rama
Born: 28.08.1978
Place: Makole – Dodoma
Voter Registration Card: 49406879
Mobile Number: 0713 760473
Dk.
Ulimboka ambaye anaendelea na matibabu nchini Afrika Kusini, amethibitishia MwanaHALISI kuwa
mtu ambaye alikuwa anawasiliana naye mara kwa mara na kumuita kwenye mkutano
maeneo ya Leaders Club, 26 Juni 2012, anatumia simu Na. 0713
760473.
Akizungumza
kwa kujiamini Dk. Ulimboka amesema, “Ndiyo. Hiyo namba naikumbuka vizuri.
Ni 0713
760473. Mwenye namba hiyo alikuwa akijitambulisha kwangu kwa jina la
Abeid. Huyo bwana ndiye niliyekutana naye Leaders Club muda mfupi kabla ya
kutekwa.”
Alipoulizwa
anawezaje kukumbuka namba iliyokuwa inafanya mawasiliano na yeye wakati kipigo
alichokipata kutoka kwa watekaji kilikuwa kikubwa hadi kupoteza fahamu, Dk.
Ulimboka alisema:
“Ninafahamu
ninachokisema. Huyo bwana nilikuwa ninawasiliana naye mara nyingi na niliwahi
kukuta naye katika mgogoro ule wa kwanza wa madaktari.”
Kauli
hii ya Dk. Ulimboka inafanana na ile aliyoitoa kabla ya kupelekwa Afrika Kusini
kwa matibabu, 30 Juni 2012.
Katika
mahojiano yake yanayopatikana kwenye mtandao wa kijamii wa You Tube, Dk.
Ulimboka anasema, “Huyu bwana kwa muda wa siku tatu mfululizo alikuwa anajaribu
kuwasiliana na mimi lakini kwa bahati mbaya ratiba yangu ilikuwa haiwezekani
kumuona.
“Nilishawahi kukutana naye kwenye
mgogoro ule mwingine, lakini this time of course (mara hii) alikuwa serious
(makini) akinitafuta…Huyu bwana anafanyakazi ikulu.”
Katika
mahojiano hayo, Dk. Ulimboka anasisitiza kuwa wakati anatekwa alikuwa na akili
timamu na hivyo anamfahamu aliyemteka kuwa ni mtu kutoka ikulu.
Dk.
Ulimboka anasimulia “mtu wa ikulu” alivyoingia kwa gari pale walikomwambia
wameketi na kumuuliza iwapo alikuwa na Deo (Dk. Deogratias Michael) na kwamba
walianza majadiliano yaliyohusu hali ya mgomo na jinsi wao walivyokuwa wakiona
unaweza kutatuliwa.
“Sisi
tukasema mambo yote yanafahamika. Tukaongea naye kwa muda mfupi tu; akawa
anaandika… kwa hiyo pia alikuwa very busy communicating, (akionekana
kujishughulisha zaidi na mawasiliano ya simu). Unaona?”
MwanaHALISI limegundua
kabla ya Dk. Ulimboka kutekwa, Rama alianza kufanya mawasiliano naye saa 12: 25
jioni. Mawasiliano hayo yaliendelea 3:29 usiku, saa 4: 52, saa 5: 27, saa 5:40
na mwisho ilikuwa saa 5:52 usiku.
Haya ndiyo mawasiliano ambayo Dk.
Ulimboka aliishasimulia kuwa yalielekea katika kukutana kwake na mwenye simu
Na. 0713
760473. Ni mwenye simu hii aliyeandaa mkutano, anakumbuka Dk.
Ulimboka.
Kabla
simu ya Rama kumwita Dk. Ulimboka kwa mara ya kwanza siku hiyo, saa 12:25,
ilifanya mawasiliano na Buruani Ntilongwa, mmiliki wa simu Na. 0712
359533.
Mawasiliano
hayo yalifanyika kati ya saa 2: 08 na 2: 24 usiku.
Aidha,
nyaraka zinaonyesha kila pale Rama alipowasiliana na Dk. Ulimboka, alifanya
mawasiliano pia na
Moshi Marungu Shabani anayemiliki simu Na. 0761 132663 na 0655 162663.
Moshi Marungu Shabani anayemiliki simu Na. 0761 132663 na 0655 162663.
“Nakwambia
ndugu yangu, kila pale ambapo Rama alifanya mawasiliano na Dk. Ulimboka, utaona
hapohapo alifanya mawasiliano na Abdallah Kunja na Ntilongwa. Hawa ni watu
muhimu sana kwenye sakata hili,” taarifa zimeeleza.
MwanaHALISI limegundua
kuwa siku mbili kabla ya Dk. Ulimboka kufanyiwa unyama huo (24 Juni 2012), simu
ya Rama iliingizwa salio la Sh. 252,849. Hili ni salio kubwa pekee kuingizwa
kwenye simu hiyo tangu mwanzo wa mwaka huu.
Nyaraka
zinaonyesha tarehe 4 Mei 2012 simu ya Rama iliwahi kuishiwa salio kabisa hadi
kufikia kiwango cha Sh. 1.
Kwa
mujibu wa nyaraka hizo zilizosambazwa na kituo cha sheria na haki za binadamu
sehemu mbalimbali duniani, Rama kila alipomaliza kumuita Dk. Ulimboka, haraka
alipiga simu kwa Kunja, Ntilongwa na Marungu.
Wengine
ambao walikuwa na mawasilino ya mara kwa mara na Rama kabla ya kutekwa kwa Dk.
Ulimboka ni:
Mohammed
Hassan Na. 0655 524444 Shomari Kondo Na. 0714
666304
Optat Jacob Marandu Na. 0716 611625 Mbega Hisbert Na. 0715 222778.
Optat Jacob Marandu Na. 0716 611625 Mbega Hisbert Na. 0715 222778.
Kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo kwenye daftari la wapigakura la NEC, Mohammed Hassan, ni mkazi wa Ilala, Dar es Salaam. Amezaliwa 12 Agosti 1980. Mbali na kumiliki namba hiyo, anatumia pia namba nyingine: 0717 242789.
Naye
Shomari Kondo amezaliwa 1 Januari 1976. Ni mkazi wa Dar es Salaam. Anamiliki
simu nyingine Na. 713 671640.
Marandu ametambuliwa kwenye daftari
hilo kuwa amezaliwa 1979 mkoani Dodoma; huku Mbega akionyeshwa kuzaliwa 16 Mei
1978 na mkazi wa Tabata, jijini Dar es Salaam.
Taarifa
nyingine kutoka ndani ya idara ya usalama wa taifa zinasema, tangu 26 Juni
2012, pale jaribio la kumteka Dk. Ulimboka lilipofanikiwa, Rama aliacha kutumia
simu yake hiyo.
Alianza
kutumia tena simu yake, tarehe 1 Julai kwa kutuma ujumbe mfupi (sms). Namba
alizokuwa anatumia sana kuwasiliana kuanzia 1 Julai 2012 ni:
0714 293425
0717 030405
0713 510585 na
0715 466995.
0717 030405
0713 510585 na
0715 466995.
Toleo
lililopita la gazeti hili lilimnukuu mtoa taarifa akisema, “Wakati wakimtesa
Ulimboka, ni Rama aliyekuwa akisisitiza kuelezwa kama Ulimboka ametumwa na
CHADEMA na kwamba ni nani hasa katika CHADEMA anayemtumia.”
Mmoja
wa watoa taarifa wa ndani ya idara ya usalama anasema, “Wazo lililopo Usalama
wa Taifa ni kuwa Ulimboka anatumiwa na Mnyika pamoja na Dk. Slaa.”
Wengine
ambao ni maswahiba wa Rama aliowasiliana nao mara nyingi katika kipindi hicho
ni:
Abdi Abdi Na. 0713 229919
Najma Damian Na. 0712 704908
Spa Wilson I. Sima Na. 0712 540502 na
Zulfa Swalehe Na. 0719 496505.
Najma Damian Na. 0712 704908
Spa Wilson I. Sima Na. 0712 540502 na
Zulfa Swalehe Na. 0719 496505.
Katika daftari la wapigakura, Abdi Abdi
anaonyesha amezaliwa 1977; Spa Wilson I. Sima amezaliwa mwaka 1960 na Zulfa
Swalehe amezaliwa mwaka 1950.
Rama
ni mfanyakazi wa idara ya usalama wa taifa aliyepo chini ya naibu mkurugenzi wa
idara ya usalama anayeshughulikia siasa, Jack Zoka.
Anadaiwa
kushiriki kikamilifu kumtesa Dk. Ulimboka katika moja ya majumba ya kificho na
hatimaye kumtelekeza msituni Mabwepande, nje ya jiji la Dar es Salaam.
Uchunguzi huu unakuja baada ya gazeti hili kuripoti kuwa Zoka, ndiye mtuhumiwa Na. 1 kwenye sakata la utekaji na utesaji wa Dk. Ulimboka.
Zoka
anatajwa pia katika kilichoitwa “…njama za kutaka kuangamiza” maisha ya katibu
mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, mbunge
wa Ubungo, John Mnyika na wengine waliopachikwa jina la “wakosoaji wakuu wa
serikali.”
Taarifa
mpya za uchunguzi juu ya maandalizi na kutekwa kwa Dk. Ulimboka, zinakuja wiki
moja tangu Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi mkoani Dar es Salaam, Suleiman
Kova atangaze kufikisha mahakamani mtu mmoja aliyedai amekiri kuhusika na
utekaji wa Dk. Ulimboka.
Kova
aliwaambia wandishi wa habari kuwa polisi wamekamata mtu aitwaye Joshua Malundi
kutoka Kenya ambaye amekiri kuteka na kutesa Dk. Ulimboka. Amedai kuwa
mtuhumiwa alikwenda kutubu katika Kanisa la Ufufuo na Uzima, Kawe, Dar es
Salaam.
Lakini
tayari mchungaji wa kanisa hilo, Josephat Gwajima amekana kauli ya Kova juu
mtuhumiwa wake na kusema, “Serikali lazima ieleze vizuri.”
Mchungaji Gwajima amewaambia waamini
wake, “Kwanza huyo mtu hajaja kwetu kutubu...kama kutubu, basi mtu huyo
angetubu huko kwao Kenya na kuhoji, “…kwani kwao Kenya hakuna Mungu?”
Taarifa za kuaminika zinasema, polisi hawajawahi kuwahoji Dk. Deogratias
Michael aliyeshuhudia Dk. Ulimboka akitekwa; Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha
Sheria na haki za Binadamu (LHRC) Hellen Kijo-Bisimba wala Onesmo ole Ngurumwa,
mratibu wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu nchini waliokwenda kumchukua
polisi Bunju
No comments:
Post a Comment