UJERUMAN BINGWA WA DUNIA


Shujaa; Mario Gotze akifunga bao la ubingwa
NI Ujerumani. Ujerumani imetwaa ubingwa wa dunia, baada ya kuiangusha Argentina kwa bao 1-0 katika mchezo wa Fainali Uwanja wa Maracana mjini Rio de Jeneiro, Brazil.  
Shukrani wake, Mario Gotze aliyeingia kuchukua nafasi ya Miroslav Klose dakika 88, aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 112.
Hilo linakuwa taji la tano la Kombe la Dunia kwa Ujerumani na sifa zimuendee kipa Manuel Neuer aliyeokoa mabao mengi ya wazi na kuwakatili Argentina walioongozwa na nyota wao, Lionel Messi.
Mario Gotze akishangilia baada ya kufunga bao la ushindi kwa Ujerumani

Refa Nicola Rizzoli wa Italia alikataa bao la Gonzalo Higuain dakika ya 32 akimalizia krosi ya Lavezzi, kwa kuwa mchezaji huyo aliotea, ingawa tayari alikwishaanza kushangilia.
Kikosi cha Ujerumani kilikuwa; Neuer, Lahm, Boateng, Hummels, Howedes, Kramer/Schurrle dk32, Schweinsteiger, Muller, Kroos, Ozil, Klose/Gotze dk88.
Argentina: Romero, Zabaleta, Demichelis, Garay, Rojo, Biglia, Mascherano, Perez/Gago dk86, Higuain/Palacio dk78, Messi na Lavezzi/Aguero dk46.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.