WATOTO YATIMA WAANDALIWA FUTARI

Afisa habari wa NEW HOP FAMILY GROUP, FLORA METHEW akizungumza na wanahabari leo 
Kituo cha kulelea watoto yatima nchini Tanzania cha NEW HOPE FAMILY GROUP kilichopo kigamboni jijini Dar es salaam kimeandaa futari kwawatoto hao siku ya chungu cha 20 itakayofanyika katika fukwe za Islamic club gezaulole kigamboni.
       Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam afisa habari wa kituo hicho FLORA METHEW Amesema kuwa lengo la kuandaa futari hiyo ni kuendeleza mahusiano mema miongoni mwa makundi mbalimbali ya kijamii pamoja na kuangalia namna ya kuwasaidia.
        FLORA Amesema kuwa futari hiyo itaongozwa na sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ambapo itafanyika siku ya mfungo wa 20 futari ambayo itawashirikisha watoto yatima kutoka vituo mbali mbali pamoja na watu wenye ulemavu.
     Kituo hicho kimewataka wadau mbalimbali kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili kuangalia kwa pamoja jinsi ya kuwasaidia watu wenye mahitaji mbalimbali wkiwemo watoto yatima na walemavu.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.