Saturday, August 9, 2014

CHAMA KIPYA CHA ACT CHAMGEUKIA RAIS KIKWETE,WAMTAKA AVUNJE BUNGE MARA MOJA,SOMA HAPA

Na Karol vicent          

 CHAMA cha Kipya cha Kisiasa Nchini Alliance for Chage and Transparence-Tanzania ACT kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kulivunja Bunge Maalum la katiba,kwa madai bunge hilo limekosa Uhalali wa Kisiasa.

           Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar Es Salaam,na Katibu Mkuu wa Cha hicho Samson Mwigamba wakati wa mkutano na waandishi wa Habari,ambapo alisema Chama cha ACT Tanzania kinasikitika kwamba bunge maalum kuendelea ilihali kundi kubwa la wajumbe nje ya Mchakato.

         Amesema bila kujali sababu ya kundi la Ukawa kuwa nje ya Bunge maalumu la Katiba,ACT haiamini kwamba mchakato huu utazaa katiba bora na yenye kubalika kwa upana bila kujali makundi yote muhimu kushiriki katika mchakato huo katika ukamilifu wake mwanzo hadi mwisho.


            “Ni maoni ya ACT Tanzania tukiendedlea na mchakato kama ulivyo sasa inawezekana tukapata katiba mpya yenye Uhalali kisheria lakini itakuwa katiba isiyo na uhalali wa kisiasa wala Jamii na kwamaana hiyo itakuwa tofauti ya maana na katiba ya sasa na hivyo na kuifanya nchi kuingia kwenye hasara kubwa ya Fedha za Umma”alisema Mwigamba.

           Aidha,chama hicho kimesekitisha sa

na na viongozi wa vyama vya siasa wa CCM na vile vinavyounda kundi la UKAWA kwa kushindwa kwao kupata muhafaka na maridiano kuhusu muunda wa muungano wa nchi na hata kusababisha kuvurugika kwa mchakato wa katiba .

      Vilevile Mwigamba ametaja kuwa ni Aibu kwamba mchakato Mzima katiba bunge Maalum umetekwa na sera za vyama vya Kisiasa kuhusu muundo wa serikali ya Muungano badala ya kutafakari na kujadili Rasimu ya katiba kwa upana na kwa maslai ya nchini na taifa kwa ujumla.

         Katika hatua nyingine chama cha ACT-Tanzania kimetoa mapendekezo kwa bunge maalum la katiba lisimamishwe ili kuendelea kutoa fursa ya mazungumzo ya kutafuta muhafaka na maridhiano hadi baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 pamoja na kufaifanyia marekebisho katiba  iliyopo  kwenye vipengele kadhaa.

        Ikiwemo kuwepo kwa tume huru ya uchaguzi kuwa huru na ya kuonekana,kuruhusu mgombea Binafsi,kushusha umri wa mgombea wa urais ili kuwapa fursa vijana,kuondoa suala la mafuta na gesi katika mambo ya muungano ili kuruhusu Zanzibar kuendelea utafutaji mafuta ya gesi kwa uhuru bila kuingiliwa na Tanzania bara pamoja kuruhusu Zanzibar kuwa na mahusiano na ushirikiano na kimataifa.

        Halikadhalika,Chama cha ACT-Tanzania kimewataka wadau wote wakatiba kuungana na kushinikiza mchakato wa katiba unaoendelea kusimamishwa na kuruhusu mabadiliko hayo machache ya katiba ya sasa ili kupisha uchaguzi na kuhakikisha taifa linapata muda wa kutosha wa kuandika katiba bila shinikizo na katika hali ya utulivu    

No comments: