Friday, August 15, 2014

DK SLAA ATEMBELEA MSIKITI WA MTAMBANI ULIOUNGUA JUZI

 
Pichani ni Katibu Mkuu  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dk. Slaa atoa pole Msikiti wa Mtambani, ajionea athari .

            Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk. Slaa amefika Msikiti wa Mtambani kutoa pole kwa waumini na viongozi wa msikiti kwa niaba ya chama kutokana na tukio la moto lililotokea juzi jioni.

            Katibu Mkuu ambaye aliambatana na Mwenyekiti wa Chama Kanda ya Pwani, Prof. Abdalah Safari mbali ya kutoa pole pia alipata fursa ya kuzunguka maeneo mbalimbali kujionea madhara ya ya moto huo ambao hadi sasa kwamujibu wa Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam unakadiriwa kusababisha uharibifu mkubwa wa mali zenye thamani ya Tshs. Mil. 600.

           Baada ya kuambiwa na Shehe Katimba mahitaji ya dharura kwa wakati huu, Dk. Slaa aliguswa na suala la wanafunzi wa Seminari ya Mvumoni kukosa vitu muhimu kwa ajili ya masomo yao hasa walioko Kidato cha Nne ambao wanajiandaa na mitihani yao ya kuhitimu, ambapo aliomba apewe tathmini ya mahitaji kwa wanafunzi hao ili chama kiweze kushirikiana na shule na wadau wengine kuwasaidia waendelee na masomo


No comments: