KAULI
aliyoisema Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema kwamba Rais Jakaya
Kikwete hana Mamlaka ya kulivunja Bunge la Katiba kwa madai ya kutokuwepo na
kipengele cha sheria kitakachompa Nafasi hiyo,sasa kauli yake imezidi kupingwa
kila kona.Mtandao huu unaripoti.
Kauli hiyo ya Ukakasi kutoka Kwa
Mwanasheria huyo wa serikali imepingwa leo Jijini Dar Es Salaam,na Kaimu
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC, Harodia Sungusia
wakati mkutano na Waandishi wa Habari aliuitishwa mahususi kuzungumzi uzinduzi
wa Filamu yenye kulenga kuwapa elimu watanzania kuhusu mambo ya katiba mpya.
Sungusia
alitumia mkutano huo kutoa masikitiko yake kwa Mwanasheria Mkuu na kusema anatoa kauli zenye kuonekana ziko
kisiasa na kuacha kuzungumzia Udhaifu wake wakushindwa kupeleke kipengere
kinachompa Rais Mamlaka la kulivunja Bunge Maalum La Katiba.
“Nashangaa sana kwa kauli hiii
ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali anavyosema Rais hana Mamlaka ya kulivunja Bunge
la Katiba wakati ukiangalia Kifungu cha 25 cha sheria kinampa Rais nguvu ya
kuteua na kufukuza mtu yeyote ambaye hana sifa,kama rais ananguvu wewe unasema
Rais hana Mamlaka y a kulivunja Bunge la katiba hizo tunaweza kusema ni kauli
za Kisiasa.alisema Sungusia
Sungusia alizidi kusema Sheria
ya Mabadiliko ya Katiba mpya inanuksi kutokana na kuwepo kwa Vipengel
e
vinavyosema endapo itashindikana kupatikana na kwa Katiba Basi turudi kutumia
katiba ya sasa amb apo alisema hiyo ndio Nuksi.
Katika hatua nyingine Kituo
hicho cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC kwa mara ya kwanza Kimezindua FiLamu mpya ambayo itatumika katika kutoa
elimu kwa Watazania kuhusu katiba mpya,
FiLamu hiyo ambayo imeigizwa na Wasanii kutoka
Tanzania wakiwemo Jengua,Masele,Mrisho mpoto pamoja na Mkurugenzi Mtendaji
wa Kituo hicho DKT Helen kijo Bisimba.
Ambapo Filamu hiyo itazinduliwa
Rasmi kesho katika Ukumbi wa Senima iliyoko karibu na Chuo kikuu cha Mlimani na
Wananchi wameomba kufika bila kukosa kuja kujionea uzinduzi huo.
No comments:
Post a Comment