Thursday, August 21, 2014

MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA INATARAJIA KUKABIDHI MADAWATI 2000 KWA SHULE ZA MSINGI 10

IMG_8357Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano toka Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi Sylvia Lupembe akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu jitihada wanazofanya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kukabiliana na changamoto katika sekta ya elimu,wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Masoko na Uhusiano toka benki ya KCB Bi. Christina Manyenye. 
IMG_8369Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wakiwasikiliza wawasilishaji toka Mamlaka ya Elimu Tanzania, KCB, TOTAL, Social Action Trust Fund (SATF) leo Jijini Dar es Salaam.
IMG_8380Mkuu wa kitengo cha Masoko na Uhusiano toka benki ya KCB Bi. Christina Manyenye akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mipango waliyoiweka kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania katika kuendeleza na kuinua sekta ya Nchini.kushoto ni Meneja Sheria na Uhusiano toka kampuni ya uuzaji na usambazaji wa mafuta ya TOTAL Bi. Masha Msuya. IMG_8401Afisa Rasilimali Fedha toka taasisi isiyo ya kiserikali ya Social Action Trust Fund (SATF) Bw. Timotheo Tenga akiwaeleza jambo waandishi wa habari( hawapo pichani) wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Sheria na Uhusiano toka kampuni ya uuzaji na usambazaji wa mafuta ya TOTAL Bi. Masha Msuya

No comments: