Sunday, August 17, 2014

MAN CITY NA LIVEPOOL WAANZA VIZURI ENGLAND

1408290610691_lc_galleryImage_Manchester_City_s_David_SMnyumbulikaji wa Kihispania: David Silva akifunga bao la kuongoza
MABINGWA watetezi wa ligi kuu soka nchini England, Manchester City wameanza vyema kampeni za kutetea taji lao baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Newcastle United katika dimba la St. James Park.
1408285385380_lc_galleryImage_LIVERPOOL_ENGLAND_AUGUST_Daniel Sturridge (kushoto) akishangilia bao la ushindi la Liverpool na nahodha Steven Gerrard
LIVERPOOL imeanza vizuri maisha mapya ya ligi kuu soka nchini England bila ya Luis Suarez kwa kuifunga Southampton mabao 2-1 ndani ya dimba la Anfield jioni hii.
Majogoo wa jiji ndio walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 23 kupitia kwa kinda wake, Raheem Sterling kabla ya Nathaniel Clyne kuisawazishia Sounthampton katika dakika ya 56 kipindi cha pili.

No comments: