Thursday, August 14, 2014

SAKATA LA KATIBA SASA LACHUKUA SURA MPYA,MWINGINE ATANGAZA KUWAPANDISHA UKAWA MAHAKAMA YA THE HUGUE

Karoli Vinsent

    KILE kichooneka
na Siasa za Tanzania zimefikia mahali pabaya,Baada ya leo Wanaharakati kuibuka na kusema wanajipanga kuwaburuza wanasiasa Wanaounda Umoja wa Kuteta katiba ya Wananchi UKAWA pamoja na makada wa Chama cha Mapinduzi CCM  kwenye Mahakama ya Kimataifa makosa ya Uhalifu The Hugue iliyoko nchini Uholanzi .
          
             Wanasiasa hao ambao ni Freeman Mbowe Chadema,Ibrahimu Lipumba CUF,Tundu Lissu CHADEMA,Ismail Jussa CUf,Capten John Komba CCM,sababu ya kuburuzwa mahakamani kwa wanasiasa hao inatokana wao kutoa kauli walizozitoa ambazo zinashilia uvunjifu wa Amani wa Nchi.

          
            Akizungumzia Maamuzi hayo Leo Jijini Dar Es Salaam mbele ya mkutano na waaandishi wa Habari, Mwenyekiti wa wa Kamati ya Amani Tanzania,Risasi Mwaulanga,alisema kwasasa hawafanyi mzaha na kwa sasa wako teyari wamewasiliana na Mwendesha Mastaka Mkuu Madame Fatou Bensuda wa mahakama ya kimataifa ya Uhalifu The Hugue ili kwenda kuwashitaki  wanasiasa ambao wataka kuhalibu amani ya nchi.
            
            “Hatuwezi kuvumilia uvunjifuu huu wa Amani ambao unataka kufanywa na hawa wanasiasa  Freeman Mbowe Chadema,Ibrahimu Lipumba CUF,Tundu Lissu CHADEMA,Ismail Jussa CUf,Capten John Komba CCM,kutokana na kauli zao za kuhalibu amani ya nchi,kwasababu ya tamaa zao za madaraka na sasa tunaandaa ushahidi ili tukawashitaki kimataifa wanasiasa hawa wanafiki”alisema Mwaulanga.
            
        Mwaulanga ambaye ni Miongoni mwa Watanzania wapenda amani alisema sababu inayowalenga wanasiasa hawa inatokana na baadhi ya maneno ambayo wamekuwa wakitaamka ambayo yanalenga kabisa kuvuruga amani ya Nchi ,
           
         Maneno hayo ni Katiba mpya itapatikana kwa Ngumi na mateke kauli hii aliitoa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema,kauli nyingine aliitoa Capt John Komba aliyoisema Serikali Tatu ikipita atakwenda msituni,
             
       Kuhusu wanasiasa wengine wakiwemo Ibrahimu Lipumba CUF,Ismahili Jussa CUF,wanawapeleka kutokana na wao kuungana katika kutoa matamko machafu ambayo nayo yanalenga kuchafua Amani ya nchi.
      

No comments: