Thursday, August 14, 2014

UTAFITI--HAWA NDIO WAANDISHI WATANO BORA WA MAKALA TANZANIA


 KWA mda miezi mitatu sasa Mtandao huu umefanya utafiti katika sekta ya Habari hususani magazeti na kutaka kujua ni Waandishi gani wa Habari kwenye magaeti ambao  makala zao zinapendwa sana.
           
      Mtandao huu katika utafiti wake uliangazia magazeti zaidi ya 20 ambayo yamesajiliwa na msajili wa magazet nchini,utafiti huo ulijikita zaidi katika kuangalia hamasa za watanzania katika kutaka kuzisoma habari za waandishi hao.
            Katika utafiti huo walishirikishwa hadi wauza magazeti pamoja na wasmaji wa magazeti.
          
Wafuatao ni ndio Waandishi watano Bora ambao Makala zao zinasomwa sana nchini Tanzania.
               1..Jenerali Ulimwengu

Huyu ndio miongoni mwa Waandishi wa Makala bora kabisa nchini Tanzania,ambaye anaandika makala ambapo wananchi hawataki hata wiki ipite bila kusoma makala zake.
             
  Ulimwengu ambaye ni anaandikia makala zake kwenye Gazeti la Raia mwema na Raia Tanzania,katika magazeti hayo amekuwa akiandika makala mbalimbali ikiwemo za Kisiasa pamoja na kijamii,na kufanya Gazeti la Raia Mwema kuwa ni miongoni mwa gazeti linalopendwa zaidi,
             
 Gazeti la Raia Mwema ni Gazeti linalotoka maramoja kwa Wiki limekuwa likipendwa sana kutokana na mchango anaoufanya mwandishi huyo.
           
   Ulimwengu makala zilizompa heshima kubwa sana ni –Acha kelele toa hoja,pamoja Hapa kwetu tunakimbilia wapi ,na makala nyingine.
          2..Saed Kubenea

Huyu naye ameshika nafasi ya pili ya Waandishi bora wa Makala nchini Tanzania,Kubenea jina lake sio geni sana kwenye masikio ya watanzania kutokana na kazi kubwa anayofanya hapa nchini kwenye sekta ya Habari.
             
     Kubenea anasifika kutokana na Ujasili aliokuwa nao,mwandishi huyo makala zake nyingi anaandikia kwenye gazeti La Mawio.
            
  Kabla ya kuandikia Mawio kubenea pia alikuwepo kwenye Gazeti la lilofungiwa kwa mda usiojulikana la Mwanahalisi.
                Katika gazeti la Mwanahalisi kubenea alikuwa ni mkurugenzi wa gazeti hilo,baada ya kufungiwa gazeti hilo,kubenea hakutaka kipaji chake kupotea cha kuhabalisha watanzania ndipo akajiunga kwenye Gazeti la Mawio.
             
   Uwepo wa wake kwenye Gazeti hilo la Mawio ndipo amelifanya limekuwa gazeti linalopendwa zaidi sana nchini Tanzania,gazeti la Mawio linatoka kila alhamisi.
          Kwa Mujibu ya wauza magazeti wanasema katika magazeti yanayofanya Vizuri gazeti la Mawio lipo.
     3---Edo Kumwembe.

                  Huyo naye ameshika nafasi ya Tatu kati ya Waandishi wa Habari ambao wanaandika makala zinazopendwa zaidi.
               
 Kumwembe,ambaye ni tofauti na Ulimwengu,kubenea kwani Kumwembe yeye anaandika makala za habari za Michezo kwenye gazeti la Mwanaspoti.
                
 Kabla ya kuandika mwanaspoti Kumwembe alikuwa anaandika makala kwenye Gazeti la michezo Dimba,ambapo alipokuwa huko kumwembe alisifika sana kwa kuandika makala nzuri zenye kuwafanya wasomaji wasikubali hata wiki kupita bila kusoma makala zake na hata alivyoamia Mwanaspoti huko ndipo alipozidi kupata umaharafu sana kwa makala zake zenye ubora.
            
   Kitu kinanchomtofautisha kumwembe na waandishi wengine wa makala za michezo kumwembe amekuwa mtu anayefanya utafiti kabla ya kuandika makala zake ikiwemo hata kwenda hata nchi za nje.
            4—Edson Kamukara
             Huyu naye ameshika nafasi ya Nne kati ya Waandishi wa Habari wanaoandika makala zinazowafanya wasomaji wazipende zaidi.
           
   Edsoni Kamukara ambaye anatoka kwenye Gazeti la kila siku la Tanzania Daima naye anasifika sana kwa kuandika makala zenye kupendwa zaidi amekuwa akiandika makala bila ya uoga wowote.
        
          Kamukara ambaye pia ni Mhariri wa Gazeti hilo ,amekuwa akiandika makala zenye kutoa elimu pamoja na kuwakosoa vongozi walioko Makadarani  ambao wanakwenda kinyume.
          Umakini wa Kamukara umelifanya Gazeti la Tanzania Daima kuwa ni miongoni mwa magazeti linalopendwa zaidi.
                     5---Jabir Idrissa
                 Huyo naye ameshika nafasi ya Tano kati ya Waandishi wanaongoza kwa undikaji wa Makala zinazowafanya wasomaji walipende Gazeti kulisoma kila siku.
         
      Jabir ambaye anatoka kwenye gazeti la Mawio naye amekuwa ni miongoni mwa Waandishi wanaongoza kwa uandishi makini wa Habari pamoja na Makala zenye kuifanya Jamii ilipende kusoma gazeti hilo.


No comments: