Wednesday, September 17, 2014

FAIDI MATOKEO NA PICHA ZA MICHEZO YA UEFA JANA USIKU HAPA

CHELSEA imelazimishwa sare ya nyumbani ya kufungana bao 1-1 na Schalke ya Ujerumani katika mchezo wake wa kwanza wa hatua ya makundi, Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu Uwanja wa Stamford Bridge, London.
Kiungo Cesc Fabregas alitangulia kuifungia The Blues dakika ya 11  ingawa pia alionekana kuchezewa faulo kabla ya kufunga. 
Klaas Jan Huntelaar aliisawazishia Schalke dakika ya 60 na kumfanya kocha Mreno, Jose Mourinho aondoke ameinamisha kichwa uwanjani.
Kikosi cha Chelsea kilikuwa: Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Filipe Luis, Matic, Fabregas, Ramires/Oscar dk69, Willian/Remy dk74, Hazard na Drogba/Costa dk74.
Schalke: Fährmann, Höger, Ayhan, Neustädter, Fuchs, Boateng, Aogo, Sam, Meyer/Choupo-Moting dk74, Draxler na Huntelaar.

MECHI YA BARCELONA
 
BAO pekee la Gerard Pique limeipa Barcelona ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Cypriots Apoel Nicosia ya Cyprus usiku huu katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Pique alifunga bao muhimu akimalizia mpira wa adhabu wa Lionel Messi katikati ya kipindi cha kwanza, lakini Apoel iliwabana vilivyo Barca licha ya kuongozwa na nyota wake Messi na Neymar mbele.
Katika mchezo mwingine, Luka Zahovic alitokea benchi kuinusuru Maribor kulala Sporting kwa kupata safe ya 1-1 kwa bao la dakika ya mwisho baada ya Luis Nani kutangulia kuwafungia wapinzani wao.

KUHUSU MAN CITY



BAO pekee la Jerome Boateng dakika ya 89, limeipa ushindi mwembamba wa nyumbani, Bayern Munich wa 1-0 katika mchezo wake wa kwanza makundi Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu.
Man City ilizuia vizuri mashambulizi ya Bayern kwa dakika 89 Uwanja wa Allianz Arena kabla ya kuachia dakika za mwishoni. Kocha Pep Guardiola aliyekuwa mnyonge muda wote wa mchezo, alitimka kwa kasi kutoka kwenye benchi kumfuata Boateng kushangilia naye bao hilo.
Kikosi cha Bayern kilikuwa: Neuer, Rafinha/Pizarro dk84, Boateng, Benatia/Dante dk84, Bernat, Alaba, Lahm, Alonso, Muller/Robben dk76, Gotze na Lewandowski
Man City: Hart, Sagna, Demichelis, Kompany, Clichy, Fernandinho, Yaya Toure, Navas, Silva, Nasri (Milner 58), Dzeko/Aguero dk74.
KUHUSU AC ROMA


MSHAMBULIAJI Gervinho na Nahodha mkongwe wa umri wa miaka 37, Francesco Totti wamefanya kazi nzuri usiku huu AS Roma ikiifumua CSKA Moscow mabao 5-1 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Olimpico.


Gervinho amefunga mabao mawili na kuseti lingine moja lililofungwa na mchezaji mpya, Juan Iturbe wakati mabao mengine yamefungwa na Maicon na Totti, wakati bao pekee la CSKA limefungwa na Ahmed Musa. Bahati mbaya kwao Roma, Iturbe aliumia kipindi cha kwanza na kutoka.

Katika michezo mingine, Athletic Bilbao imelazimishwa safe ya 0-0 na Shakhtar Donetsk wakati Porto iliichapa 6-0 BATE jana.


No comments: