.

HABARI ILIYOTIKISA JIJI--UKAWA WATANGAZA MAANDAMANO,MIGOMO NCHI NZIMA,SOMA ALICHOKISEMA MBOWE LEO

Mwenyekiti wa chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA mh FREMAN MBOWE akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho jijini Dar es salaam leo
              Mwenyekiti wa chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA mh FREMAN MBOWE ambaye pia ni mwenyekiti wa wa umoja wa katiba ya wananchi UKAWA  ametangaza maandamano na migomo ya nchi nzima ambayo haina ukomo kwa kushiriakiana na umoja wa katiba ya wananchi UKAWA yenye lengo la kupinga mchakato wa katiba mpya unaoendelea kwa sasa kwa madai kuwa ni ubadhilifu mkubwa wa pesa za watanzania.
            
Akizungumza jijini Dar es salaam Mapema leo wakati akifungua mkutano wa mwaka wa CHADEMA mkutano ambao pia utamchagua mwenyekiti mpya wa chama hicho mh MBOWE amesema kuwa umoja wa katiba ya wananchi ukawa wamechoshwa na mambo yanayoendelea ndani ya bunge la katiba na sasa wameamua kuingia katika maandamano ili kushinikiza wananchi kudai haki hao ambayo inachezewa na watu wachache.
        

“naomba mnisikilize makamanda,sasa tumechoka na mazungumzo ambayo hayana mwisho,tunadanganyana mchana kweupe,na mwisho wa siku tunamaliz a hela za watanzania bila kupata muafaka wa maana,hivyo natoa maagizo kwa makamanda wangu wa kila mkoa,sasa tunakwenda kufanya kitu ambacho kitaishtua dunia,tutaandamana,tutafanya migomo ya kila namna,iwe kwa kibali cha polisi au bila kibali ila yatafanyika”amesema mh MBOWE
           
   Mh MBOWE amesema kuwa lengo la maandamano hayo ni kumshinikiza mwenyeikiti wa bunge la katiba Tanzania pamoja na serikali kulisitisha bunge hilo mara moja kwa kile ambacho amedai kuwa linaendelea kuwaibia watanzania mali zao huku wakijua kuwa bunge hilo haliwezi kuwapatia watanzania katiba.

Aidha mwenyekiti huyo amewashiomba wanachama wa vyama vya upinzani wanaotoka mikoa jirani na DODOMA kuandamana na mabango kuelekea bungeni kuzuia shughuli za bunge hilo,huku akiwaomba viongozi wa vyama hivyo kuhakikisha kuwa wanaratibu maandamano hayo ambayo amesema kuwa yataanza siku yoyote.

Aidha katika hatua nyingine mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF  mh IBRAHIM HARUNA LIPUMBA amesema kuwa umoja wa katiba UKAWA ni mpango wa mungu na lengo lao ni kuwafungua macho watanzania ambapo amesema lengo lao ni kuimarisha ushirikiano wao na ikibidi wasimamishe mgombea mmoja katika chaguzi zijazo.

Mkutano mkuu wa chama cha CHADEMA unafanyika leo jijini dare s salaam ambapo lengo kubwa ni uchaguzi wa viongozi wa ngazi za juu za chama hicho ikiwemo nafasi ya uenyekiti wa chama hicho ambayo inashikiliwa na mh MBOWE.

Katika mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kisiasa akiwemo makamu mwenyekiti wa CCM mh PHILIPO MANGULA,mwenyekiti wa NCCR MAGEUZI mh JAMES MBATIA,mwenyekiti wa CUF mh IBRAHIM LIPUMBA pamoja na mabalozi kutoka nchi mbalimbali duniani kwa hapa Tanzania.

 

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.