.

HABARI KUBWA JIJINI LEO--CHADEMA YATANGAZA RASMI RATIBA YA MAANDAMANO YAKE KUANZIA KESHO,NI WIKI NZIMA ,WASEMA WATAANDAMANA BILA KIBALI CHA POLISI


    Na Karoli Vinsent

 CHAMA  cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kimetangaza rasmi kuanza maandamano pamoja na Migomo nchi nzima kuanzia kesho mpaka Jumamosi kushinikiza Bunge la Katiba lisitishwe kwa madai Bunge hilo limekuwa likitekezea pesa za Watanzania huku  Katiba haipatikani.
     
       Maandamano hayo yametangazwa leo jijini Dar Es Salaam na Mkurugenzi wa Mafunzo na oganizasheni Benson Sengo Kigaira wakati wa Mkutano na Waandishi Habari ambapo alisema licha ya Jeshi la Polisi kuwanyima Kibali cha kufanya Maandamano pamoja na Migomo ambayo ni haki ya kikatiba kwa kila mtanzania,basi chama hicho kitaanza maandamano rasmi kwaania kesho Jumatatu mpaka Jumamosi.
           
         “Jeshi la Polisi nchini limetunyima haki ya kufanya Maandamo  ambayo kimsingi ni haki ya kila Mtanzani kudai haki yake ambayo katiba imetamka wazi,basi Kwaanzia kesho mpaka Jumamosi Tunatangaza Maandamano nchi nzima kupinga wizi huu unafanyika Bungeni Dodoma na hatutamuogopa mtu yeyote,tena nawataka watanzania wajitokeze kila walipo wajumuike katika kufanya Maandamo nchi nzima”alisema Kagaira
           
        Kagaira alizidi kusema Maandamano haya yatafanyika nchi nzima na kila mkoa maandamano hayo yataanzia kwenye ofisi za Chadema kwenye Mikoa hadi kwenye Ofisi za Mkuu wa mkoa,
         
      “Maandamano haya yatafanyika kwa kwa awamu katika wiki zima,kwa upande wa Mkoa wa Dar Es Salaam tutafanya Jumatano wiki hii na tutaelekea Ofisi za Waziri Mkuu  na kwa upande wa Dodoma wataelekea Ofisi za Bunge na mikoa mingine watachagua lini hasa katika wiki hii wataanza maandamamo ila nimetoa maagizo kwa Viongozi wa Chadema wa Mikoa kuhakikisha wanachagua siku yeyote ndani ya wiki hii kuanza maandamano,tena wasiogope polisi wala nani kwasababu Polisi wamekuwa upande wa Chama cha Mapinduzi na Kuacha kazi yao kikatiba”alizidi kusema Kagaira,
          
           Vilevile Kagaira aliwataka watanzania popote walipo kujiweka tayari kwa maandamano kwani maandamano hayo ni ya amani na kusema Chadema haitoweza kukubali kuyumbishwa na Jeshi la polisi ambalo limekuwa likifanya mambo kibabaishaji
      
         Kwa Upande wake Wakili wa Chama hicho John Mallya alisema wamejipanga kisheria katika kuhakikisha haki ya msingi ya maandamano inapatikana na kuwataka wanachama pamoja na wapenzi wa chama hicho kujitokeza kwa wingi kwenye maandamo hayo’
        
         “Tumeomba kibali cha maandamano Jeshi la polisi linatukatalia na kusema Bunge la katiba liko kisheria kama ndio hivyo mbona bunge lenyewe limekiuka sheria ya mabadiliko ya katiba kwa kitendo chake cha kujigeuza na kuanza kuchukua maoni kutoka kwa wananchi ambayo sio kazi yake,kwahiyo nawaomba watanzania wote kujitokeza kwa wingi kwenye maandamano”alisema Mallya.
         
         Katika hatua nyingine chama hicho kimelaani vikali kitendo cha Jeshi la polisi kupiga waandishi habari wiki iliyopita wakati wa walipokuwa wakichukua taarifa juu ya mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.