Tuesday, September 16, 2014

HABARI KUBWA JIJINI LEO--UFISADI WA ESCROW,KAFULILA AIBUKA NA KUMVAA CAG LEO,SOMA KAULI ZAKE HAPA


Na karoli vinsent

       HUKU kukiwa bado wingu zito limetanda kwa Watanzania kuhusu hatma  ya Ufisadi wa Fedha Sh200 bilioni zilizohifadhiwa kwenye akaunti ya Escrow zilitolewa na kulipwa kwa Kampuni ya Pan African Power (PAP),ambapo Fedha hizo inasemekana zimeliwa na watendaji wa Serikali.
        
        Naye Mbunge wa Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila amekuja juu na kumtaka Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kutoa ripoti mara moja ya uchunguzi aliyotumwa na Bunge ili umma ufahamu ukweli kuhusu sakata hilo,
          
          Kauli ya Kafulila imekuja huku kukiwa na Taarifa juu ya kustaafu kazi kwa Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali Ludovick Utoh wiki hii kikatiba,mkaguzi huyo ambaye Bunge lilimuagiza  yeye CAG na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza tuhuma hizo za uchotaji wa fedha hizo.

         
       Wasiwasi huo umesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mbunge wa Kigoma Kusini (NNCR-Mageuzi) David Kafulila  wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari,ambapo Kafulila alitoa masikitiko yake kwa Mkaguzi Mkuu wa Serikali kushindwa kupeleka Taarifa Bungeni ya uchunguzi huo, badala yake ameipeleka Serikalini halafu yeye mwenyewe akijua mda wake wakustaafu ta

yari umefika.

         
         “Jamani inasikitisha sana CAG anashindwa kupeleka taarifa za uchunguzi kwenye Bunge ndio lilomtuma kisheria,sasa leo nimesikia taarifa ya ripoti nzima ameipeleka serikalini ambapo sio kulikomtuma, Hata  hiyo (report) taarifa ya (Takukulu) ilipaswa kuwasilishwa kwa Bunge kwani ni azimio la Bunge lilioagiza (Takukulu) kuchunguza baada ya Spika kukataa hoja yangu ya kuunda kamati teule. 

       Sasa PCCB amekabidhi Taarifa kwa Rais Alhamisi kimyakimya.sasa kama si njama za kutoka kuuzima ukweli nini:”alihoji Kafulila
      
         Kafulila alizidi kusema  Kitendo cha Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali CAG,kustaafu bila hata kupeleka taarifa ya uchunguzi wake kwenye bunge  kunazidisha mashaka juu ya uchunguzi wenyewe,kwani ingebidi CAG apeleke taarifa zima ya uchunguzi wake na ukweli.
           
              “Ndugu zangu wanahabari hizi ni fedha nyingi sana zaidi ya bilioni 200,ni fedha zingewekeza kwenye masula ya maendeleo Taifa lingefika mbali lakini leo Fedha hizi zimeibwa watendaji wachache,sasa kitendo cha CAG kustaafu bila hata kamati yake ijatoa taarifa ya uchunguzi wake kunanipa mashaka sana na tunasikia mara taarifa imepelekwa serikalini jamani mbona kuna utendaji mdogo hapa wa Viongozi wetu, ”Alizidi kusema Kafulila.
     
          Mbunge Kafulila ambaye anakesi mahakama kuu iliyofunguliwa na Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Pan Afrikan Power Solutions Limited (PAP) na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni hiyo, Harbinder Sigh Seth, ambapo amefungua  kesi hiyo kwa madai ya Sh. bilioni 310 kwa  Mbunge wa Kigoma Kusini kwa kile anachokiita ni kuchafuliwa .
         
            Alipoulizwa na Waandishi wa Habari kwamba kuzidi yeye kuendelea kulizungumzia suala hilo haoni anaingilia upande wa mahakama kutoka na kesi yenyewe kuwapo mahakamani,Kafulila alisema Kesi iliyopo mahakamani hawezi kumzuia yeye kusema ukweli kwani pingamizi lilowekwa na kampuni hiyo kwamba mahakama inamzuia Kafulila asingumzia suala hilo kwenye vyombo vya Habari,bado mahakama haijatoa hukumu la pingamizi hilo.
            
           Aidha Kafulila aliwataka wanasiasa,Watanzania pamoja na Vyombo vya habari kutoufumbia macho Ufisadi huu wa pesa uliofanywa na Watendaji wa Serikali ya Rais Kikwete,kwani kunahaja ya kushinikiza kila kona mpaka taarifa hii isomwe kwenye Bunge ili ukweli ugundulike,

No comments: