Friday, September 5, 2014

HII NDIO KAULI YA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO LEO JUU YA MGOMO WAO


Na Karoli Vinsent
          
      HUKU kukiwa bado wingu likiwa limetanda kuhusu Hatma ya mgomo wa Wafanyabiashara wanaouza maduka maoneo ya Kariakoo kutokana na mgomo huo kuzidi kuendelea,nao Umoja wa Wafanya Biashara wadogo wadogo nchini umeibuka na kuivaa Mamlaka ya ukusanyaji kodi nchini TRA na kusema ndio wanaosababisha Mgomo huo,
             
      Kutokana na Mamlaka hiyo kuanzisha mfumo mpya wa kukusanya kodi pasipokuwa kuwa na ujuzi wa mfumo waliouanzisha.
                  
     Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanya Biashara Wadogo nchini,Joseph Minja wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari,kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo mgomo huo,ambapo alisema kuhusu mgomo wa maduka hapo kariakoo usilaumiwe umoja huo,kwani watu wanaosababisha matatizo ni Tra,
            

        “Kusema kweli mgomo huu,sisi umoja wa wafanya biashara hatuhusiki kabisa kwani Tra ndio wanahusika kwa kitendo chake cha kuanzisha mfumo mpya wa ukusanyaji kodi  wa kietroniki ambao hawana ujuzi kabisa kwani tufahamu kwamba Tanzania ni nchi ya kwanza Duniani kutumia mfumo huu wa ukusanyaji kodi”

       “ kwa kutumia mashine za kietroniki ndio maana wanashindwa kutatua kero wanazozidai wafanyabiashara wa maduka kuhusu mfumo huu kutoka na wao kushindwa  hata pakwenda pakujifunza”alisema Minja

         Minja alizidi kusema kauli anayoitoa Mkurugenzi huduma ya mlipa kodo kutoka  Tra,Richard Kayomba kuhusu mgomo huo sio kweli kwani umoja huo hahusiki kwenye mgomo huo kwani Mamlaka hiyo ndio chanzo cha mgomo huo kutokana na wao kuwafungia maduka wafanyabiashara hao,
         
        Aidha Minja aliitaka mamlaka hiyo kutatua changomoto zinazotokana na mfumo huo,kwani ndio  chanzo cha matatizo.
     
       Katika hatua nyingine jumuiya hiyo ya wafayanya biashara imesema mkutano wao  mkuu utafanyika tarehe 6 mwezi huu mkoni Dodoma na kuwataka wafanya biashara watokeze kwa wingi ili kuja kujadili changamoto zinazotokana na mfumo mpya wa ukusanyaji kodi  na masuala mengine 

No comments: