Monday, September 15, 2014

HII NDIO STORY ILIYOMFANYA KAMISHNA KOVA LEO KUKUTANA NA WANAHABARI,ISOME HAPA


Na Karoli Vinsent

  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, limewakamataa majambazi wawili kwa kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria na kuitumia katika matukio ya ujambazi na kuwaletea Adha wakazi wa jiji hili.
Akithibitisha kuyakamata majambazi hayo sugu,Kamanda wa kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishna Suleiman Kova wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam,ambapo alisema Kabla ya kukamata kwa bunduki hiyo watuhumiwa walikuwa wamepanga kufanya tukio la ujambazi katika maduka ya MPESA na TIGO PESA yaliyopo maeneo ya Sinza Madukani. Majambazi hao waliahirisha kufanya tukio baada ya kushtukia mtego wa polisi.  
           

       Kamishna Kova alizidi kusema Mnamo tarehe 10/09/2014 majambazi hao walikamatwa baada ya Polisi kupata taarifa kuwa yamejipanga kufanya tukio la uhalifu maeneo ya YOMBO DOVYA na kisha kuweka mtego katika nyumba ya ASIA D/O ALLY KASHINDE anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 70 iliyopo maeneo ya Yombo Makangarawe (M) wa Kipolisi wa Temeke.

 Baada ya kuwakamata majambazi hao walipekuliwa katika chumba wanacholala ndipo ilipopatikana silaha aina ya SMG yenye namba IC 5740 ikiwa na risasi 07 ndani ya magazine. Bunduki hiyo imekatwa mtutu na kitako. Watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa ili kuwezesha kuwakamata wengine wanaoshirikiana katika genge hili la ujambazi

  Kamishna Kova aliwataja kwa Majina Majambazi hao ni  KHAMIS S/O AMBA, Miaka 40, Mkazi wa Yombo Makangarawe na OMAR S/O KHAMIS, Miaka 43, Mkazi wa Masasi Nyasa Mtwara

 Katika hatua Nyingine jeshi hilo kanda Maalum ya Dar Es Salaam limejipanga kupambana na Mitandao inayoandika na kuweka picha za Matusi kwa kusema Jeshi hilo la polisi linashikiriana na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kuwabaini wamiliki wa mitandao hiyo na kuwachukulia hatua kali za kisheria.


No comments: