Tuesday, September 16, 2014

HOT NEWZZ--BAVICHA WAWAJIBU JESHI LA POLISI KUHUSU MAANDAMANO,WAITISHA KIKAO CHA DHARURA KUANZA MIPANGO YAO

Mwenyekiti wa baraza la vijana BAVICHA bw PATROBAS KATAMBI akizungumza na wanahabari muda huu hapa katika mkutano wa chadema unaoendelea
 Kufwatia jeshi la polisi Tanzania jana kupiga marufuku maandamano yaliyotangazwa kufanyika na chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA,umoja wa vijana wa chama hicho BAVICHA umeibuka na kusema kamwe hawatishiki na kauli ya jeshi hilo na wapo tayari kwa lolote.
         
Akizungumza na wanahabari muda huu nje ya mkutano wa kamati kuu ya chama hicho mwenyekiti wa vijana taifa PATROBAS KATAMBI amesema kuwa kauli iliyotolewa na mwenyekiti wao sio kauli yake kwani ni kauli ya chama na wanachama wote hivyo polisi wasihangaike kumkamata mwenyekiti wao na badala yake wajiandae kulinda amani wakati wa maandamano  hayo.
   
“tumezoea kusikia kauli za vitisho vya jeshi la polisi wakati chadema inapotaka kufanya kitu cha kuwatetea wananchi wao,ila siku ccm ikitangaza kufanya maandamano ya amani huwezi kusikia kauli kama hizo,sasa tumechoka na mambo hayo na tupo tayari kwa lolote lile”amesema mwenyekiti wa BAVICHA TAIFA
      
Aidha amesema kuwa ofisi yake imeitisha kikao cha dharura kwa ajili ya kupanga mikakati imara ya kuanza maandamano hayo ambapo amesema kuwa yatafanyika nchi nzima bila kikomohuku akisema  yataanza muda wowote kuanzia sasa.
Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa chama hicho  WILFRED  LWAKATARE akizungumza na wanahabari muda huu
Katika hatua nyingine mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa chama hicho  WILFRED  LWAKATARE  amesema kuwa wao kama watu wa ulinzi wa chama hicho wanatekeleza lile ambalo limetotangazwa na viongozi wao wa juu hivyo ni jukumu lao kuhakikisha kuwa maandamano hayo yanafanyika kwa amani na kama itatokea vurugu itakuwa imeletwa na polisi wenyewe.

No comments: