Sunday, September 21, 2014

HOT NEWZZ --CUF WATANGAZA KUWAUNGA MKONO CHADEMA KWA MAANDAMANO YAO NCHI NZIMA


Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF mh PRF IBRAHIM LIPUMBA akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam
 Chama cha wananchi CUF leo kimetangaza kuunga mkono harakati zinazofanywa na chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA za kuandaa maandamano nchi nzima kupinga kuendelea kwa bunge maalum la katiba na kusema kuwa chadema kipo sawa na maandamano hayo ni halali na watatoa ushirikani wote katika maandamano hayo.

Akizungumzaa jumapili hii na wanahabari jijini Dar es salaam mwenyekiti wa chama hicho profesa IBRAHIMU LIPUMBA amesema kuwa CHADEMA kama chama cha siasa ni jukumu na ni haki yao kufanya maandamano pale ambapo wataona kuna ubadhilifu wa fedha za wananchi unatokea katika nchi.

Wanahabari wakiwa kazini leo ndani ya makao makuu ya CUF
 Aidha LIPUMBA akizungumzia sakata la kuitwa na kuhojiwa kwa mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni mh FREMAN MBOWE amesema kuwa hakuna sababu yoyote ya msingi ya kumhoji kjiongozi huyo kwani maandamano yote yanayoitishwa na CHADEMA yanafwata taratibu zote  ila kinachotokea ni polisi kutokujua sheria za maandamano. Na kusema kumwita mh MBOWE  ni kumdhalilisha kiongozi huyo mkubwa wa upinzania wakati anatekeleza haki yake ya kikatiba.

“kazi ya polisi sio kuruhusu maandamano ya chama chochote,sisi tunatoa taarifa tu kwa polisi ili watulinde,na hatuombi kibali cha polisi kiufanya kibali,polisi wanadhani kuwa sisi tunaomba kibali cha maandamano wakati ni haki ya kikatiba kabisa ya kuandamana na kufanya mikutano ya adhara.
 Mh LIPUMBA amesema kuwa CHADEMA sio chama cha kwanza kutangaza maandamano ya nchi nzima kuhusu jambo la katiba kwani mapema baada ya hotiuba ya Rais KIKWETE aliyoitoa wakati anafungua bunge la katiba chama cha mapinduzi nao walitangaza mikutano na maandamano nchi nzima ambayo hayakupingwa na polisi ila anashangaa upinzani kunyimwa haki hiyo ya msingi.
Katika hatua nyingine chama hicho cha CUF kimelaani vikali kitendo cha kupigwa na kudhalilishwa kwa wanahabari nje ya makao makuu ya polisi wakati wakifwatilia sakata la kuitwa mh MBOWE mwishoni mwa wiki jana.




No comments: