Tuesday, September 23, 2014

LHRC-BADO WANANCHI HAWANA UELEWA WOWOTE WA MCHAKATO WA KATIBA MPYA

Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu Bi HELEN KIJO BISIMBA akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam
             Ikiwa mchakato wa katiba mpya ukiendelea kwa bunge maalum la katiba kufikia hatua ya kuipigia kura rasimu iliyopendekezwa na kisha kuletwa kwa wananchi,imeelezwa kuwa bado watanzania wengi hususani wale ambao wapo pembezoni mwa nchi hawana uelewa wowote juu ya mchakato huo na hatua unaopitia.
         
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC  Bi HELEN KIJO BISIMBA wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu awamu ya pili ya kampeni ya kusambaza uelewa wa rasimu ya pili (KAMPENI GOGOTA),kampeni iliyofanyika katika mikoa ishirini ya tanzania.
        
      Bi HELEN amesema kuwa katika mikoa mingi waliopita moja ya changamoto kubwa waliyokutana nayo ni wananchi wengi kukosa uelewa kabisa wa katiba mpya jambo ambali amesema kuwa linazua hofu kubwa  kama wakipelekewa rasimu iliyopendekezwa kama watakuwa tayari kuipitisha hata kama  hawajaelewa na si ile iliyotokana na tume ya mabadiliko ya katiba tanzania.


     Aidha LHRC wamesema kuwa wakati wakiwa kwa wananchi wamebaini kuwa wananchi wengi wanakosa fursa ya kufwatilia mchakato wa katiba mpya kutokana na kutokuwa na nyenzo kama television,umeme,radio na nyinginezo huku akitolea mfano kuwa wilaya ya ngara inasikika vizuri radio moja tu iitwayo redio kwizera.

 Aidha katika hatua nyingene bi HELEN amesema kuwa wananchi wengi wamekuwa na hofu kubwa ya kutopatikana kwa katiba mpya huku akisema sababu ni pamoja na kutokuwa na imani na tume ya uchaguzi itakayosimamia zoezi la upigaji kura ya maoni na sababu nyingine ikiwa ni bunge la katiba kuacha kujadili rasimu iliyotokana na maoni ya wananchi na badala yake kujadili mambo yao,pamoja na kuwepo kwa mgawanyiko mkubwa kati ya wajumbe wa bunge hilo.

Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC kilifanya kampeni ya kutoa uelewa kwa wananchi juu ya rasimu ya pili ambapo mikoa ishirini ilipitiwa ikiwa ni kutoka Tanzania bara na Zanzibar.




No comments: