MATOKEO BAWACHA--HUYU NDIYE MWENYEKITI MPYA

Mbunge wa jimbo la kawe mh HALIMA MDEE leo ametangazwa rasmi kuwa mwenyikiti mpya wa baraza la wanawake la chadema nchini  BAWACHA baada ya uchaguzi uliofanyika jana na kumalizika leo asubuhi ambapo mh MDEE amepata kura 165 na kuwapita wagombea wenzake takribani saba waliokuwa wanawania nafasi hiyo.

 Viongozi wengine waliopata nafasi ya uongozi ndani ya baraza hilo makamu mwenyekiti kutoka bara ambapo amechaguliwa HAWA MWAITUNGA,HUKU makamu mwenyekiti zanzibar akichaguliwa HAMIDA ABDALA,huku nafasi ya mweka hazina ikichukuliwa na EVELINE MEENA.nafasi nyingine bado zinaendelea na

uchaguzi ambapo hadi mtandao huu unaondoka katika uchaguzi huo leo mchana tayari nafasi ya katibu wa bawacha bara ilichukuliwa na GRACE TENDEGA huku nafasi nyingine zikiendelea kupigiwa kura

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.