Saturday, September 13, 2014

MATUKIO YOTE MUHIMU KWENYE MECHI KUBWA ENGLAND LEO YAKO HAPA,COSTA KIBOKO YAO


Lingekuwa la ushindi; Alexis Sanchez akishangilia baada ya kuifungia bao la pili Arsenal 

BAO la dakika ya 83 la Martin Demichelis limeinusuru Manchester City kulala mbele ya Arsenal baada ya kupata sare ya kufungana mabao 2-2 Uwanja wa Emirates katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo.

Sergio Aguero alitangulia kuifungia City dakika ya 28 akimalizia kazi nzuri ya Jesus Navas kabla ya Jack Wilshere kuisawazishia Arsenal kipindi cha pili akimalizia kazi nzuri ya Aaron Ramsey

Alexis Sanchez akaifungia Arsenal bao la pili dakika ya 74 kabla ya Debuchy kuisawaishia City. Mshambuliaji mpya wa Arsenal, Danny Welbeck alikaribia kufunga dakika ya 11 baada ya kugongesha mwamba, wakati kiungo mpya wa Man City, Frank Lampard alionyeshwa kadi ya njano.

Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Szczesny, Debuchy/Chambers dk81, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Flamini/Arteta dk95, Wilshere, Ramsey, Alexis, Ozil na Welbeck/Oxlade-Chamberlain dk88.

Man City: Hart, Zabaleta, Kompany, Demichelis, Clichy, Fernandinho/Kolarov dk77, Lampard/Nasri dk45, Navas, Silva, Milner, Aguero/Dzeko dk67.

Sergio Aguero akishangilia baada ya kuifungia Manchester City
MECHI YA CHELSEA
Kuna maswali? Diego Costa amepiga hat trick Chelsea ikiua 4-2 Ligi Kuu England



MSHAMBULIAJI Diego Costa ameendeleza mwanzo mzuri katika Ligi Kuu ya England baada ya kuifungia Cheslea mabao matatu peke yake katika ushindi wa 4-2 dhidi ya Swansea City Uwanja wa Stamford Bridge, Londo.

Wakati mchezaji huyo bora wa Agosti, akipiga hat trick yake ya kwanza England na kufikisha mabao saba ndani ya mechi nne, bao lingine la Chelsea lilifungwa na mchezaji mpya, Loic Remy aliyeingia kuchukua nafasi ya Coasta kipindi cha pili. Beki John Terry alijifunga kuipatia Swansea ambayo bao lake lingine lilifungwa na Jonjo Shelvey.

MECHI YA LIVERPOOL

Mwanzo magumu; Mshambuliaji mpya wa Liverpool, Mario Balotelli akimtoka beki wa Aston Villa leo Uwanja wa Anfield. Liverpool ililala 1-0





BAO pekee la Gabby Agbonlahor dakika ya tisa siku tatu tangu asaini Mkataba mpya wa miaka minne, limeipa Aston Villa ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Liverpool Uwanja wa Anfield jioni ya leo.



Hicho kinakuwa kipigo cha pili msimu huu kwa Liverpool, baada ya awali kufungwa mabao 3-1 na Manchester City Uwanja wa Etihad.


Mshambuliaji mpya, Mario Balotelli aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 16 kutoka AC Milan, alichezea kwa mara ya kwanza Liverpool lakini hakuweza kuiepusha na kipigo hicho.


Kikosi cha Liverpool kilikuwa: Mignolet, Manquillo, Lovren, Sakho, Moreno, Gerrard, Henderson, Markovic/Borini dk71, Coutinho, Lallana/Sterling dk61 na Balotelli/Lambert dk71.


Aston Villa: Guzan, Hutton, Senderos, Baker, Cissokho, Cleverley/Sanchez dk86, Westwood, Delph, Agbonlahor/Bent dk90, Weimann/N'Zogbia dk72 na Richardson.

No comments: