REPORT NZIMA YA MICHEZO YA UEFA JANA USIKU IKO HAPA,MATOKEO NA PICHA


Danny Welbeck kushoto amekosa mabao matatu ya wazi Jana Ujerumani
ARSENAL imeanza vibaya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya usiku huu kuchapwa mabao 2-0 na Borrusia Dortmund nchini Ujerumani. 

Mabao yaliyozamisha timu ya Arsene Wenger usiku huu yametiwa nyavuni na Ciro Immobile na Pierre-Emerick Aubameyang. Mshambuliaji mpya wa Gunners, Danny Welbeck alipoteza nafasi tatu za kuifungia Arsenal.

Kikosi cha Dortmund kilikuwa; Weidenfeller, Durm, Subotic, Sokratis, Schmelzer/Jojic dk79, Bender, Kehl/Ginter dk46, Aubameyang, Mkhitaryan, Grosskreutz, Immobile/Ramos dk86.
Arsenal; Szczesny, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Arteta/Podolski dk77, Sanchez, Ramsey/Cazorla dk62, Wilshere, Ozil/Oxlade-Chamberlain dk62 na Welbeck

.Mario Balotelli celebrates opening his Liverpool account
Balotelli broke the deadlock late in the second half
Mario Balotelli akishangilia baada ya kuifungia Liverpool
Mario Balotelli amefunga bao lake la kwanza leo Liverpool ikianza na ushindi Ligi ya Mabingwa Ulaya

LIVERPOOL imerudi vizuri katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya usiku huu kutoka nyuma kwa bao 1-0 na kushinda 2-1 dhidi ya Ludogorets Uwanja Anfield.
Mshambuliaji wa Italia, Mario Balotelli amefunga bao lake la kwanza leo Liverpool dakika ya 81, kabla ya Dani Abalo kuisawazishia Ludogorets.

Nahodha Steven Gerrard aliihakikishia Liverpool kushinda mechi ya kwanza ya makundi kwa bao la penalti dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90 za kawaida za mchezo.

Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Mignolet, Manquillo, Lovren, Sakho, Moreno, Henderson, Gerrard, Lallana/Borini dk67, Sterling, Coutinho/Lucas dk67 na Balotelli.

Ludogorets: Borjan, Caicara, Moti, A Aleksandrov, Minev, Dyakov, Abel, M Aleksandrov, Marcelinho, Misidjan na Bezjak.

KUHUSU MADRID 
Gareth Bale akipongezana na Ronaldo baada ya kufunga katika ushindi wa 5-1
MABINGWA wa Ulaya, Real Madrid wameanza kwa kishindo kutetea taji, baada ya usiku huu kuifumua mabao 5-1 Basle Uwanja wa Bernabeu.


Marek Suchy alijifunga dakika ya 14 kuipa Real bao la kuongoza kabla ya Gareth Bale kufunga la pili akimalizia pasi ya Luka Modric dakika ya 30.


Bale akamtilia krosi maridadi Cristiano Ronaldo kuifungia Real bao la tatu dakika ya 31 kabla ya James Rodriguez kufunga la nne dakika ya 36 na Derlis Gonzalez kuifungia Basle bao la kufutia machozi dakika ya 37. Karim Benzema alihitimisha shangwe za mabao za Real Madrid kwa bao la tano dakika ya 79.Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Casillas, Pepe, Sergio Ramos, Marcelo, Nacho, Kroos, Rodriguez, Bale, Modric, Ronaldo na Benzema. 
Basle: Vaclik, Samuel, Schar, Suchy, Safari, Zuffi, Frei, El-Nenny, Xhaka, Streller na Gonzalez

.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.