Wednesday, September 17, 2014

SIRI ZA MKUTANO WA RAIS KIKWETE NA TCD ZAANZA KUVUJA,DK SLAA AWALIPUA CHEYO,DOVUTWA NA MREMA,SOMA HAPA


Na Karoli Vinsent

          SIRI za mazungumzo ya Mkutano kati ya Rais Jakaya Kikwete pamoja na Viongozi wa Vyama vya kisiasa vilivyo chini ya Kituo cha Demokrasia (TCD),sasa siri za Kikao hicho zaanza kuvuja.

         Mkutano huo ndio ulitoa maazimio ya kulisitisha bunge la katiba na kuifanyia marekebisho katiba iliyopo ya mwaka 1977 kwa madai bunge la katiba la sasa aliwezi kutengeneza Katiba,
               
         Naye, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dk Wilbroad Slaa ameibuka  na kufichua siri za Mkutano huo na kusema  Mwenyekiti wa Kitoa cha Demokrasia (TCD) John Cheyo pamoja  naMwenyekiti wa Chama cha UPDP Mhe Fahmi Dovutwa  walikuwa wakimuomba Rais jakaya Kikwete asilisitishe Bunge la katiba kwa madai watakosa posho katika Bunge hilo,
  
         Siri hizo zimefichuliwa leo Jijini Dar Es Salaam na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dk Wilbroad Slaa wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari,ambapo Dk Slaa alisema anasikitishwa na siasa za hovyo walizokuwa nazo John Cheyo na Fahmi Dovutwa kwani wanasiasa hao ni wapenda posho.

       
          “Mimi nawashangaa watu wanaopoteza mda kuwasikiliza wanasiasa wahovyo kama hao kwasababu wakati wa mkutano na Rais  Kikwete na TCD,Katibu Mkuu wa CCM , Abdulrahman Kinana aliandaa Tamko lilosainiwa na Prosesa Lipumba,James Mbatia,pamoja na mimi mwenyewe kwenda kwa Rais Kikwete tena Tamko hilo likuwa likimtaka Rais Kikwete alisitishe bunge la katiba kwa madai bunge hilo aliwezi kutengeneza katiba”

      “Na Rais Kikwete alikubaliana na sisi kwamba bunge maalum la katiba haliwezi kutengeza katiba,hawa wakina Dovutwa,cheyo na Mrema wakasema kwamba Rais ukilisitisha bunge la katiba mwezi huu tutakosa posho,na Rais huyo alivyokuwa ni muoga akubaliana nao na kukubali bunge litafune pesa mpaka tarehe 4 octoba”alisema Slaa,
      
          Dokta Slaa alizidi kusema Umoja wa katiba UKAWA hauwezi kubishana na Wanasiasa hao kwakuwa vyama hivyo ni miradi ya chama tawala cha CCM.
        
          “Hivi leo chama cha CUF,NCCR-mageuzi-Chadema tupoteze mda wetu kubishana na vyama vilivyosajiliwa zaidi ya Miaka kumi na tano kwa msajili wa vyama vya kisiasa lakini mpaka leo hakina hata mwenyekiti wa serikali za mtaa wala mbunge kitatuambia nini,harafu mwenyekiti wao wanaibuka kwenye bunge hilo la katiba na kusema Upinzani hupo Bungeni,huu si uozo mtupu”alizidi kusema Slaa,
         
           Vilevile Dokta Slaa akusita kumzungumzia Mwenyekiti wa TLP Mhe Augustine Lyatonga Mrema na kusema mwenyekiti huyo wakati wa kikao hicho cha TCD na Rais Kikwete kila alipokuwa akipewa nafasi na Rais Kikwete alikuwa akiishia kusema Rais Jakaya Kikwete amzuie James Mbatia asikwenda kugombania kwenye Jimbo lake la Vunjo badala ya kuzungumzia masuala ya katiba,ndipo ikamfanya Rais Kikwete awambie wajumbe wakikao hicho kwamba wachukulia hari hiyo ni ya Utani kwa kitu anachosema,

       Katika Hatua nyingine chama hicho Kikuu cha upinzania nchini kimesema Maandano na Migomo iliyotangazwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe juu ya kushinikiza Bunge la katiba lisitishwe kwa madai bunge hilo linapoteza pesa za wanannchi bure, iko pale pale na wala chama hicho akiogopi kauli zenye lengo ya kuwatisha tama zinazotolewa na Jeshi la polisi.

          Hayo aliyesema Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Tundu lissu,ambapo alisema hoja wanazosema jeshi la polisi kwamba Maandamo pamoja na Migomo nchi nzima hazina ukweli kwani maandamo ni haki za Msingi kikatiba,

           Vilevile Tundu Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki CHADEMA alisema chama hicho kimesikitishwa na ufanyi kazi wa hovyo wa Jeshi la polisi nchini,kutokana na Jeshi hilo kumwandikia barua Mwenyikiti wa chama hicho Freeman Mbowe kwenda kwenye mahojiano huku kikishindwa kuweka kosa wanalomuitia,

        “Jamani wanahabari huu ndio upuuzi wa jeshi letu la polisi ambalo lipo Kikatiba lakini ni la hovyo kutokana na  kutojua sheria,maana Jana tarehe 17 tulipata barua kutoka Jeshi la Polisi likimtaka Mwenyekiti wetu aende polisi makao makuu kwa mahojianao cha kushangaza barua yenyewe haina hata kosa la wanalomwitia”



       “Tukashaurina jana kwenye kamati kuu tukakubaliana aende tu kwenye hayo mahojiano,maana tunajua,Hawa wahuni wasije wakatuletea matatizo”alisema Gwiji huyo wa Sheria kutoka  Chadema.
     
            Naye Naibu Katibu Mkuu bara John Mnyika alisema wakati Mwenyekiti wa Chama hicho anavyokwenda Polisi kuitikia wito alioitiwa chama hicho kimejipanga kutoa wanasheria waliobobea kwenda kumtetea mwenyekiti wa Chama hicho.
       
         “Wakati ,wenyekiti wetu wa Chadema atakapokuwa anakwenda kutoa maelezo Jeshi la polis hatasindikizwa na jopo la wanasheria waliobabea maana chama chetu ndicho kinaongoza kuwa na wenye sheria waliobobea na pia tunawataka wanasheria wate wanaoishi mkoa wa Dar es Salaam,kujitokeza kwa wingi polisi makao makuu kwa lengo la kwenda kumtetea mwenyekiti wetu”alisema Mnyika

No comments: