Tuesday, September 16, 2014

TIGO YADHAMINI MAONYESHO YA KUINUA TASNIA YA FILAMU TANZANIA

Mkurugenzi wa kanda ya Kaskazini wa Tigo, Bw. David Charles akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza udhamini wa kampuni ya Tigo kwa maonesho ya filamu za Kiafrika Arusha (AAFF) yatakayofanyika Septemba  20 mpaka 27 jijini Arusha. Kushoto kwake Meneja wa maonesho ya AAFF, Bi. Mary Birdi.
 Tigo Tanzania leo imetangaza udhamini wake kwa maonesho ya filamu barani Afrika yatakayofanyika mkoani Arusha kuanzia Jumamosi wiki hii. Maonesho hayo ya wiki moja yanayojulikana kama maonesho ya filamu za Kiafrika Arusha (AAFF) yataonesha filamu mbali mbali za wasanii nchini na kimataifa.

Akitangaza udhamini huo kwa waandishi wa habari kutoka ofisi za Tigo Arusha, Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini wa Tigo, David Charles alisema kwamba udhamini huo wa Tigo katika maonesho hayo ya filamu ni dhamira ya dhati ya kampuni hiyo katika kuendeleza tasnia ya filamu nchini ambayo kwa sasa inatoa ajira kwa maelfu na maelfu wa vijana nchini na kuwainua kimaisha.

“Tasnia ya filamu nchini imebadilika kutoka kuwa tasnia ambayo inaburudisha wapenzi wake na kuwa sekta inayotoa ajira kwa vijana. Tunaamini kwamba AAFF ni fursa nzuri kwa waigizaji na waandaji wa filamu kuonyesha vipaji vyao na kutangaza pia utamaduni wa Tanzania kimataifa,”alisema Charles.
Meneja wa Mawasiliano wa Tigo Bw. John Wanyancha(aliyesimama) akiongea na waandishi wa habari jijini Arusha leo wakati wa mkutano kuhusu udhamini wa Tigo maonesho ya AAFF.

Meneja wa maonesho ya filamu za Kiafrika Arusha(AAFF), Bi.Mary Birdi akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa kutangaza mdhamini wa maonesho hayo kampuni ya Tigo, maonesho yatakayofanyika Septemba  20 mpaka 27 jijini Arusha., kulia kwake Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini wa Tigo Bw. David Charles.
Ukitoa kutazama filamu, kutakuwa pia na warsha na semina ambazo zitaongelea mada mbali mbali kuhusu maendeleo ya tasnia ya utengenezaji filamu barani Afrika kama ushirikishwaji wa vijana, mshikamano wa kijamii na kiutamaduni, na jinsi ambavyo hayo yanahusiana na maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika jamii zetu. Warsha na semina hizo zitawahusisha washiriki kutoka nchini Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi, nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), alisema Birdi.


Mkurugenzi wa maonesho ya AAFF Akpor Otebele, “Napenda kuwaalika wapenzi wote wa filamu kutoka Tanzania na nchi jirani za Afrika Mashariki kuweza kuungana nasi katika maonesho haya ya AAFF kuanzia Jumamosi tarehe 20 mpaka Jumamosi tarehe 27 Septemba waweze kushuhudia vipaji vya wasanii nchini na wa kimataifa na kusikia simulizi nzuri kutoka barani Afrika.”

No comments: