Thursday, November 20, 2014

KIMENUKA HELA ZA ESCROW,HUYU NDIYE KIGOGO WA KWANZA KUTAJWA KUSHIRIKI KUZITAFUNA


Na Karoli Vinsent


            HUKU ikiwa bado Jinamizi  la ufisadi wa zaidi Bilioni 400 kwenye Akaunti ya Escrow likiwa bado lipo mikononi mwa Kamati ya Bunge ya Hesabu ya Serikali PAC ili  kuikagua Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali CAG kuhusu ufisadi huu,sasa Mazito yaibuka,MTANDAO HUU UNARIPOTI.

            Taarifa za kuaminika ambazo mtandao huu unazo zinaonyesha jinsi watu mbalimbali walivyonufaika na ufisadi huo Mkubwa kuwai tokea tangu nchi kupata Uhuru.

          Watu hao wakiongozwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering Bwana James Rugimalira ambayo kampuni yake ni mbia wa Kampuni ya IPTL,ambapo taarifa  hizo zinamuonyesha jinsi Bwana Rugimalira akigawa mapesa ya walipa kodi wa taifa hovyo hovyo kama hazina mwenyewe.
Waraka huu umekuwa ukisambazwa sasa ukionyesha alivyokuwa anagawana pesa hizo.
   

         Taarifa mbalimbali zinamuonyesha bwana Rugimalira ndiye anayoitumia akaunti ya Banki ya Mkombozi  na kuwagawa pesa kupitia Akaunti yake ni 00120102523901 iliyoko Banki ya Mkombozi Jijini Dar Es Salaam.
     
            Rugimalira kampuni yake ya VP Engineering ndio ilikuwa inamilikia hisa asilimia 30 na baada ya mgawanyo wa hisa hizo Rugimalira alipata zaidi ya bilioni 98.
  
            Chanzo hicho cha Kuaminika kinamuonyesha jinsi Mkurugenzi huyo alivyowanufaisha marafiki zake hususani kabila la Wahaya kutoka mkoani Bukoba.

         Mhaya wa kwanza aliyetajwa na vyanzo mbali mbali ambaye amenufaika na mgawanyo huo ni Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo na Makazi Profesa Anne Tibaijuka ambaye alipewa zaidi ya Bilioni 1.6 na Rugimalira ambazo yeye Tibaijuka anasema alipewa kwa ajiri kuziokoa shule zake.
Shule hizo Barbro Johanssen iliyoko Jijin Dar es Salaa na Kajumulu iliyoko Bukoba.
    
           Mhaya Mwengine aliyenufaika na mapesa hayo ya Kifisadi ni Jaji Aloysius Mujulizi ambaye naye alipewa Sh 40.4 milioni na Rugimalira.
     
            Naye Prof Eudes Ruhangisa naye mhaya huyu kapewa Sh.404.2 milioni huku mipesa yote hiyo yawalipa kodi imepitia kwenye akaunti Na 00120102544301 katika benki ya Mkombozi.
    
         Mtu mwingine kutoka Mkoa huo wa Bukoba ambaye naye ni pia Mhaya ni Jaji Mujulizi ambaye naye alipewa mamilioni ya pesa kupitia kwenye Akaunti Na 00110253580 kutoka benki ya Mkombozi
Neema ya watu wa Bukoba kuvuna pesa za kifisadi ilienda pia kwa Bwana Rweyongeza Afred Bitungwa ambaye naye alipewa na Rugimalira milioni 40 na alipotafutwa alikili kupewa pesa hizo na Rugimalira na kudai eti alipewa kwa ajiri ya kusaidia matatizo madogodogo.

             Mtu Mwingine ni bwana mmoja ambaye naye ni mhaya alitambulika kwa jina moja la Kyabukoba naye alipewa kiasa cha pesa ambacho bado mtandao huu unajakifahamu.
Wengine Jaji Ruangisa ambaye naye pia vyanzo mbalimbali vinamtaja kuwa lipewa mgawanyo huo

           Zali hilo la kuvuna mipesa lilikwenda kwa Mhaya Mwingine ni Rugozombwa Theophil ambaye ni mwanasheria wa RITA kupitia Akaunti Na 00120102602001,bwana Rugimalira alimuuingizia kiasi cha Milioni 323.4 milioni pasipo bila sababu yeyote fedha hizo ziliingia Februali 5 mwaka huu

            Akaunti ya kampuni ya VIP Engineering and Management (VIPEM), ilifunguliwa na mmoja wa wabia wa IPTL, James Rugemalira, ambaye alikuwa akimiliki asilimia 30 ya IPTL huku kampuni ya Mechmar Bhd ya Malaysia ikiwa na hisa asilimia 70.
Kutokana na kiasi hicho cha hisa, Rugemalira amelipwa kiasi cha dola milioni 75 (Shilingi Bilioni 123), zikionyesha kwamba alilipwa kiasi cha dola milioni 7.5 (Shilingi bilioni 12.4) mwaka jana na kiasi kilichosalia alimaliziwa mwaka huu.

            Kiasi hicho cha fedha kililipwa kwa Rugemalira na kampuni ya PAP inayomilikiwa na Harbinder Singh, ambaye kwa sasa ndiye mmiliki pekee wa IPTL baada ya kununua hisa za Mechmar na zile za VIP.

         Akaunti hiyo ya Tegeta, ilianzishwa kwa sababu ya kuhifadhi fedha zote zilizopaswa kulipwa na Tanesco hadi hapo mgogoro baina ya pande hizo mbili umalizike.
Hata hivyo, Septemba mwaka jana, serikali kupitia Wizara ya 

         Nishati na Madini, iliagiza BoT kulipa fedha hizo kwa kampuni ya PAP mara baada ya kuridhishwa na uamuzi wa Mahakama Kuu uliosema kwamba mgogoro baina ya wamiliki wa IPTL na 

No comments: