Wednesday, November 19, 2014

SERIKALI YAFANYA KWELI BANDARINI

Pichani ni  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Shaaban Mwinjaka akikagua mabehewa mapya leo jijin Dar es Salaam
NA Karoli Vinsent
Serikali ya Rais Jakaya Kikwete imedhamilia kuliboresha Shirika la Reli ya kati TRL ili liweze kujiendesha lenyewe na kuacha kutegemea bajeti ya Serikali kwenye mipango yake,baada ya leo kampuni hiyo imepokea Mabehewa 50 ya kubebea makasha (Containres), ikiwa ni sehemu ya mradi wa serikali wa ununuzi wa mabehewa mapya 274 kutoka nchini India.
Kupokelewa kwa mabehewa hayo, kunatarajia kuongeza kasi ya utoaji wa makasha ya mizigo kutoka  Bandari ya Dar es Salaam kwa njia ya reli kwenda nchi jirani za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda na kutimiza malengo ya Big result yaani matokea makubwa sasa.
       Akipokea Mabehewa hayo leo Kwenye bandari ya Jijini Dar es Salaa na kushuhudiwa na waandishi wa habari pamoja v, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Shaaban Mwinjaka, alisema  serikali inaendelea kutekeleza miradi 12 kupitia Mpango wa Matokeo Makubwa sasa (BRN), yenye lengo la kuimarisha huduma ya usafirishaji kwa njia ya reli.
Hapa ndipo Mahebewa hayo yakiwasili leo Jijin Dar es Salaam kwenye bandari
Alisema serikali imeshalipa zaidi ya bilioni 45 ikiwa ni gharama za ununuzi wa mabehewa 274 ambayo ni wastani wa milioni 166 kwa kila behewa.
        Vilevile Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa , lengo la serikali ni kuiwezesha TRL kusafirisha mizigo tani milioni 1.5 kwa mwaka na kuiwezesha kampuni hiyo kujiendesha kwa faida.
Vilevile akatabainisha kuwa, baada ya kukamilika kwa mradi huo kutapunguza uharibifu wa barabara kutokana na mizigo mingi kusafirishwa kwa njia ya barabara.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TRL, Mhandisi Kipallo Kisamfu, alisema katika mabehewa 274  yaliyokwisha nunuliwa na serikali  yatakuwa ya aina tatu tofauti.
Alizitaja ainia hizo kuwa ni mabehewa ya kubebea makasha, mizigo kichele na mafuta ambapo ifikapo mwezi Februali mwakani, mabehewa yote yatakuwa yameshawasili nchini.

Mwezi Julai mwaka 2011, serikali iliamua kuiendesha TRL baada ya mwekezaji kutoka kampuni ya RITES ya India kubainika kushindwa kuiendesha kampuni hiyo kama ilivyotarajiwa.

No comments: