.

TAZAMA MALUMBANO MAKALI YANAYOENDELEA KWENYE FACEBOOK BAADA YA ZITTO KABWE KUKUBALI MAPENDEKEZO YA CHENGE


http://4.bp.blogspot.com/-G12qcPnfL58/Uo7Uc2hz-6I/AAAAAAAAHEE/HA7tE3xE7Ks/s1600/Zitto+Kabwe.jpg Mhe  Zitto  Kabwe

ZITTO KABWE PAMOJA NA KUONESHA UNA UCHUNGU NA TAIFA NIMESHITUSHWA NA WEWE KUUNGA PENDEKEZO LA ANDREW CHENGE AMBAYE NI MTUHUMIWA.
Mara zote watu hudhani nina chuki binafsi na Zitto Kabwe ,Lahasha,Ninampenda sana Zitto Kabwe kwa kuwa ana uwezo mkubwa wa kijenga hoja Pamoja na kuwa na ushawishi mkubwa kwa umma.Lakini Pamoja na hilo,Zitto Kabwe ameliingiza taifa katika kunusuru mafisadi.
Kitendo cha Zitto Kabwe kuunga mkono hoja ya Andrew Chenge kwamba eti mamlaka zilizowateua Mafisadi kama Prof Muhongo,Pinda,Prof Tibaijuka na wenzake ndizo ziwawajibishe hivyo kukiuka kabisa mapendekezo ya PAC namba 8,9 10,11,12 ni kubariki mafisadi kujipa adhabu wenyewe.
Zitto katika pendekezo la Chenge ameunga mkono na kukubaliana huku akijua Chenge naye ni mtuhumiwa wa scandal hii ya uchotaji wa fedha katika account ya ESCROW kiasi cha Bilioni 1.6 sawa na milioni 1600 ni kulinda mafisadi.
Hivi mwizi anaweza kushauri ama kupendekeza adhabu ya kupewa??.Je ni kweli mtuhumiwa anaweza kushauri adhabu kali dhidi yake??
Ona sasa Wabunge wanasema Emmanuel Nchimbi,Hamis Kagasheki,Lowasa nk waombwe radhi kwa kuwa waliwajibishwa kwa kashfa mbalimbali iweje hawa walindwe??.Lowasa na wenzake waombwe radhi??
Zitto Kabwe Pamoja na kueleza kwa kina na kwa ufasaha mkubwa,Lakini kitendo cha kuunga mkono pendekezo la Chenge ni kutuachia maswali mengi sana yaliyokosa majibu.
Any way,ngoja tukubaliane na wengine pengine ni kutimiza PRINCIPLE OF NATURAL JUSTICE(NEMO JUDEX IN CAUSA SUA) yaani RIGHT OF RULE OF NO BIAS..Madam Spika hujautendea haki umma wa watanzania, hujaitendea haki principle of natural justice katika kipengere cha rule against bias ( nemo judex in causa sua) no one is a judge of his own course kwa kitendo chako cha kumwachia Chenge atoe pendekezo kwa hukumu inayomuhusu!!!! Historia 
itakukumbuka mama!!!
Aidha sitaki kuungana na wengine kumlaumu Zito alijitahidi sana sana sana kama kukosea hata Lisu kuna mahala alikosea sana sema hoja yake ilikataliwa, nilifiatilia kwa kiasi kikubwa bunge na nikaona kabisa wabunge wetu wamejisahau kuna mambo walikubaliana mimi nayashangaa sana. Kimsingi mapendekezo yote kuanzia namba moja hayajakaa vizuri yanahitaji uchunguzi mwingine, kimantiki saga limeshaisha. Sasa sijui polisi ama mahakama watakuwa wazuri kiasi gani zaidi ya CAG, TAKUKURU na PAC.
Am very sad hamjui tu.ZZK WHY??
Yaani unaruhusu mapendekezo ya chenge na werema. unamuachia mwizi akushauri cha kumfanya. yaani ajihukumu??
Ulichofanya ni kama kuua jeshi lote la adui akabakia commando mmoja ukamfungulia mikono na kumpa bunduki ajiue mwenyewe.
hapo ni kuchukua risk ya kupoteza maendeleo ya mchakato mzima. back to Zero.


Tunapoendelea kufuatilia bunge letu, ambalo kwa kweli limekuwa tukufu sana katika saga hili la Escrow, naomba tuzingatie mambo matatu yanayojitokeza:
i) Bunge letu limewekewa mipaka mikubwa sana kikatiba katika kuiajibisha serikali. Kikatiba, Bunge halina uwezo wa kumfukuza mtu yeyote kazi zaidi ya Rais, Waziri Mkuu na Spika. Bunge lina mamlaka ya kuwafukuza hawa kwa sababu bosi wa wananchi ni Rais na hivyo Bunge linaweza kumfukuza Rais kwa niaba ya wananchi. Bunge linaweza kumfukuza Waziri Mkuu kwa sababu ndilo lilimthibitha katika uteuzi wake. Kwa hiyo, technically, Waziri Mkuu anateuliwa na mihimili miwili-Rais na Bunge. Bunge linaweza kumfukuza spika kwa sababu ndilo lililomchagua. Kwa hiyo, tunapowakomalia wezi wetu wafukuzwe ni muhimu pia kuanza kufikiria namna ya kulipa meno zaidi Bunge katika Katiba. Kwa hiyo tuisome katiba pendekezwa vizuri na kama haina mambo haya hiyo itakuwa sababu nyingine ya kuikataa. Hii ndilo lile ambalo rafiki yanguMimi Mwanakijiji amelikazania kwamba tuwekeze katika kufix mfumo pia badala ya kuhangaika na watu tu! Lakini mie namwambia rafiki yangu huyu kwamba huu mfumo haurekebishiki bila kwanza kuifukuza CCM madarakani!! Wakati hatujafanikiwa kuitoa CCM madarakani inabidi tuendelee na kuhangaika na wabaya wetu zaidi ndani ya mfumo huu.
ii) Ni wazi kwamba wabunge hawana imani tena na waziri jeuri Profesa Muhongo kutokana na kiwango alichowadanganya. Hata Profesa mwenzake Mwandosya amekiri waziwazi kwamba kulikuwa na pesa ya umma katika akaunti ya Escrow. Na katika hitimisho lake Zitto ameonyesha tena kiwango ambacho Muhongo amelidanganya Bunge kwa kutumia takwimu za kijiolojia katika kuchambua takwimu za kiuchumi hasa pale alipojaribu kuonyesha kwamba eti Tanesco haina hela kwenye Escrow kwa sababu tu inadaiwa sana. Hili Zitto amelieleza kwa ufasaha mno kwa kiwango ambacho Muhongo alipaswa kukiri hadharani kwamba alichemsha. Sasa serikali ina hiari iendelee kubaki na Muhongo ambaye wabunge hamwamini kwa kiwango hicho. Na akiendelea kubaki katika nafasi yake ya uwaziri, ni mbunge gani atakayeamini majibu ya Muhongo bungeni? Ndiyo kusema kwa serikali kumng'ang'ania Muhongo maana yake inajiweka katika mazingira ya kuzidi kutokuaminiwa na wabunge na inajiweka kwenye mtego wa kuanzishiwa mchakato wa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani na Rais.
iii) Tusiwakatisha tamaa majemadari wetu pale wanapoteleza. Tusiwe wepesi wa kuhukumu. Raha ya majadiliano ni kwamba kuwe na hoja kinzani. Nalisema hili kwa sababu nimeona kuna watu walikwazika sana na kitendo cha Zitto Z Kabwe kuunga mkono phrasing ya Chenge. Kimsingi Zitto alikuwa mbele yetu katika kufikiri pamoja na kwamba baadaye alisema alikuwa amechoka. Kama ile phrasing ingeenda kama ilivyopendekezwa na Zitto ina maana kwamba ingemgusa hadi waziri mkuu ambaye wabunge wa CCM hawataki kabisa aguswe. Ndiyo maana Spika Makinda ghafla akabadili azimio ambalo tayari lilishapigiwa kura. Rafiki yangu mwingine Ezekiah Wenje alilishtukia hili. Kwa vyovyote vile tusiwachukulie majemadari wetu kama malaika ambao hawatafanya makosa. Watafanya makosa lazima na tuwakosoe inapokuwa wamekosea, lakini tuache tabia ya kuitana majina.

Madam Spika hujautendea haki umma wa watanzania, hujaitendea haki principle of natural justice katika kipengere cha rule against bias ( nemo judex in causa sua) no one is a judge of his own course kwa kitendo chako cha kumwachia Chenge atoe pendekezo kwa hukumu inayomuhusu!!!! Historia itakukumbuka mama!!!
Aidha sitaki kuungana na wengine kumlaumu Zito alijitahidi sana sana sana kama kukosea hata Lisu kuna mahala alikosea sana sema hoja yake ilikataliwa, nilifiatilia kwa kiasi kikubwa bunge na nikaona kabisa wabunge wetu wamejisahau kuna mambo walikubaliana mimi nayashangaa sana. Kimsingi mapendekezo yote kuanzia namba moja hayajakaa vizuri yanahitaji uchunguzi mwingine, kimantiki saga limeshaisha. Sasa sijui polisi ama mahakama watakuwa wazuri kiasi gani zaidi ya CAG, TAKUKURU na PAC.


David Kafulila,Zitto na kamati yake ya PAC,Wabunge wote wa Upinzani na wale wa CCM waliojenga hoja na kuweka ushabiki pembeni mmepambana vya kutosha
Nawapongeza viongozi wakuu wa UKAWA kumwalika Zitto kwenye kikao jana.Huu ni ukomavu wa kisiasa
Naomba baadhi ya wanasiasa sio wa CCM tu lakini kuna vijana wa Upinzania ambao wanadhani wao ni wanachama wa vyama kuliko wengine,waache ujinga maana hawana tofauti na wale manazi wa CCM waliokua wanatetea Upuuzi
Hivi kuna Mwana-CHADEMA kuliko Kamanda Mbowe,Mwana-NCCR -Mageuzi kuliko Mhe.Mbatia au Mwana-CCM kuliko Mwandosya,Wassira au Naibu Katibu Mkuu Mwigulu Nchemba? Mbona wao hawakuleta unazi wa vyama vyao leo kwa kuzingatia mapenzi na vyama vyao?Unazi wakati mwingine unatuaibisha na kulirudisha taifa nyuma.
Kwa mfano kitendo cha Zitto(tena aliyekwishatangaza amechoka kufikiria muda huo) kuunga mkono phrase aliyotoa Chenge ,maana yake alifikiria ile Phrase ilikua ya jumla kwa maana ya kuwa itumike kwa maazimio yote yaliyobaki na bahati mbaya au coincidentally spika hakushtukia kuwa ingemmaliza hadi waziri Mkuu maana ingebidi hata yeye uteuzi wake ufikiriwe na kuchukuliwa hatua stahiki
Alikubali haraka haraka na wabunge kwa unazi wao wakaitikia ndiyoo!
Wenje alikua smart sana kugundua hiyo trick na spika alivyotaka waanze tena akamkomalia kwamba tayari spika alishahoji na imepitishwa
Rais angebaki na mamlaka ya kuwafukuza kazi kwa kuwa hata spika amekiri wamegoma kujiuzulu si ina maana ingetoa mwanya kwa Bunge kuja kukusanya kura ya kutokua na Imani na Rais bunge lijalo na mgogoro ungeendelea kuliko kuumaliza kimagumashi kama wanazi wengine walivyodhamiria kuilinda serikali leo?
Siasa sio U-Simba na U-Yanga.Hebu Tusikatishane tamaa,Tuna vita kali mbele yetu bado.Tunahitaji kile tunachoita katika mapambano "Re-grouping".
Kuna watu ndani ya upinzani hawana tofauti na wale wanazi wa CCM.Badala ya kumlaumu spika kwa michezo yake ya paka na panya bungeni wanamlaumu Zitto aliyekua akitafuta tricky ya kumuweka spika na wanazi wenzie mtegoni. They sucks for really!
Tena wengine walikua pembeni siku zote na hawajawahi kuwa part of the struggle.Let's stop this blame game!
We still remain one country with desperate Partisan agendas and i can say it for umpteenth times again that we can sit down in a sovereign national colloquly to discuss the basis for our nationhood.
Anything short of this is just vacuous scahiamachy
Aluta continua,Victory Ascerta....!ZITO KABWE SIKUTEGEMEA.
Ametuangusha Watanzania tuliokua tunaanza kurudisha imani kwake. Sijaamini kilichotokea. Unaunga mkono hoja ya chenge.? Kwa lipi jema alilolifanya kwa Taifa hili. Makinda anawabeba wezi anakupa nafasi unajibu umechoka? Upo wapi uzalendo wako? Ulianza kuturudishia imani ghafla ukageuka kua shubiri? Sijaamini. Duh. Najuta kuzaliwa nchi ya mazingaombwe


About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.