Wednesday, December 3, 2014

HABARI HII KUTOKA DAR ES SALAAM LEO HUTAKIWI KUIKOSA


Maandamo ya Wanafuzni Pamoja na Wanaharakati wakipinga unyanyasaji wa Kijinsia wakiwasili makao makuu ya TGNP Jijini Dar es Salaam picha na Suleiman Magari
 Na Karoli Vinsent
         WITO umetolewa kwa Jamii kupinga vikali Vitendo vya Ukatili wa Kijinsia kwa wanawake, Vijana  pamoja na watu wenye ulemavu ili kuikomboa Jamii kutoka kwenye Vitendo hivyo.
     
Rai hiyo imetolewa mda huu Jijini Dar Es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)  Bi Lilian Liundi wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Wiki ya kupinga Vitendo vya Ujangili iliyoanza mwezi Novemba 25 mwaka huu ambapo Be Liundi alisema kwa sasa jamii inachangamoto kubwa sana kuhusu vitendo vya  ukatili wa Kijinsia ambayo inaifanya jamii kuishi katika hofu kubwa hususani wakina wanawake na vijana pamoja na watu wenye Ulemavu .  
Mkurugenzi mkuu wa TGNP akifafanua jambo mbele ya ummati wa wanaharakati katika viwanja vya vyao,
  Bi Liundi alizidi kusema  kuzinduliwa kwa kampeni hii  inayoitwa Funguka,fichua ukatili kwa afya ya Jamii,itatoa mwanya kwa jamii kuvunja ukmya kila wanaposhuhudia Vitendo vinavyoanyilia unyanyasaji wa Kijinsia basi wachukue hatua.
     
 Pia Alitabainisha kuwa hali ya vitendo vya unyasaji wa kijinsia nchini vimeongezeka kwa kiasa kikubwa kwani kati ya wanawake 2 kati ya 5 wamefanyiwa viendo vya ukatili wa kijinsia.
     
   Vilevile Bi Liundi alisema Sababu ya kuongezeka  Vitendo hivyo vimetokana na kuongezeka wa Shughuri hizo ambazo ni maeno ya usafirishaji   haramu kwa wasicha,Tatizo la Ajira,Biashara ya ngono pamoja na ndoa za utotoni .
Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la UNFPA nchini 
        Kwa upande wake Kaimu mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na utawala Bora Tanzania Bi Mary Massay aliitaka jamii kutovivumilia Vitendo vya Ukatili wa Kinjisia kwa kukalia  na taarifa zinazohusu vitendo hivyo kwa kutoa Taarifa kwenye Madawati ya Vitendo vya Kijinsia pamoja na Polisi.

No comments: