Friday, December 12, 2014

HUU NDIO UZALENDO--LHRC WAJITOA KUFANYA UANGALIZI UCHAGUZI WA JUMAPILI KWA NJIA ZA KISASA,TIZAMA WATAKAVYOFANYA KAZI HAPA

Mkuu wa dawati la uangalizi wa chaguzi na bunge LHRC KHAMIS MKINDI akizungumza na wnahabari juu ya mfumo huo ambao watautumia katika uchaguzi huo unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki huu siku ya jumapili

Story na Exaud mtei

Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa nchini Tanzania uchaguzi unaotarajiwa kufanyika siku ya jumapili ya mwisho wa wiki hii,kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC leo kimetangaza kufanya uangalizi wa uchaguzi huo kwa njia ya TEHEMA yaani ICT-election monitoring katika mikoa yote nchini Tanzania baada ya kufanya hivyo kwa mafanikio makubwa mwaka 2009.


Akizungumza na wanahabari muda huu makao makuu ya LHRC mkuu wa dawati la uangalizi wa changuzi na bunge bwana KHAMIS MKINDI amesema kuwa kituo chao kimesambaza waangalizi nchi nzima katika mikoa 25 na wilaya 165 za Tanzania bara na visiwani ambapo hadi kufikia sasa wawakilishi wao wapo kila kona ya Tanzania kwa uangalizi wa hatua kwa hatua ya uchaguzi huo,ambapo amesema kuwa uchangalizi huo umeanza kipindi cha kampeni na utaendelea kipindi cha uchaguzi na baadae baada ya uchaguzi.

Wataalam mbalimbali wakiwa tayari kufanya uangalizi wa uchaguzi huo 
Aidha pamoja na wawakilishi hao katika mikoa na sehemu mbali mbali nchini kituo hicho kimeweka timu maalum ndani ya makao makuu ya LHRC ambapo ndio taarifa zote za uchaguzi zitafikia na kupokelewa na wataalam mbalimbnali waliobobea katika Nyanja mbalimbali.

Amesema kuwa pia wako na kitengo maalum cha kupokea taarifa kupitia mitandao yote ya kijamii ikiwemo facebook ambapo account yao ni www.facebook/chaguzitanzania pamoja na mitandao yoote ya kijamii kama twitter ambapo ni @chaguzitanzania pamoja na namba ya simu ya 0684472896 ambayo mtu yoyote anawezakutuma taarifa mbalimbali kuhusu matuio ya chaguzi katika maeneo yao.
Huu ndio mfumo utakao kuwa unatumika kuleta taarifa zoote za uchaguzi huo wa serikai za mitaa ambapo taarifa zote zitakazoripotiwa zitaonekana hapa
Pamoja na hayo amesema kuwa kituo cha sheria LHRC ni commanding center ambapo lengo lao ni kupokea taarifa za uchaguzi na kuzifikisha katika mamlaka husika kwa lengo la kuzifwatilia
Wataalam wakiwa kazini kuhakikisha mambo yote yanakuwa sawa

 Akitaja baadhi ya taarifa ambazo wanaendelea kuzipokea katika maeneo mbalimbali ni pamoja na uandikishwaji wa wapiga kura kuwa wa muda mfupi na wengi kushindwa kujiandikisha,kuenguliwa kwa wagombea kinyume cha taratibu,pamoja na matatizo mengine ambao wamezitaka mamlaka husika kuzifanyia kazi taarifa hizo





No comments: