Wednesday, December 3, 2014

KATIBU MKUU WA WIZARA YA UCHUKUZI AFUNGUA MAONESHO YA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA YANAYOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA OFISI ZA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA BANANA LEO ASUBUHI

unnamed1Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) Bw. Charles Chacha akiongea na waandishi wa habari kuhusu hali ya usalama wa anga Tanzania na namna Tanzania ilivyofanikiwa kupunguza idadi ya ajali za ndege.
CCCCC 5Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka, akimsikiliza Ofisa Utawala, kutoka Baraza la Ushauri la Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA-CC), Ms Catherine Monarya, wakati alipotembelea banda hilo kujua shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo, Katibu Mkuu ameishauri taasisi hiyo kutoa elimu zaidi
CCCCCCCC 4
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka, akimsikiliza Kaimu Meneja wa Huduma za Hali ya Hewa katika Usafiri wa Anga na Maji kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA), wakati alipotembelea banda hilo katika maonesho ya sekta ya Usafiri wa Anga, ambayo yanafanyika katika viwanja vya Ofisi za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), leo asubuhi.CCCCCCCCCCCC 1
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaaban Mwinjaka(mwenye tai nyekundu), akimsikiliza Muongozaji Ndege katika kiwanja cha Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), Bi. Mossy Kitang’ita, wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), leo asubuhi katika viwanja vya Ofisi za Mamlaka hiyo.

No comments: