Tuesday, December 2, 2014

LHRC WATAKA KAULI YA SPIKA MAKINDA ISIPUUZWE,NI ILE YA WABUNGWE KUHONGWA ILI KUITETEA ESCROW,STORY NZIMA IKO HAPA


 Mkurugenzi  wa utetezi na maboresho ya sera wa  LHRC HAROLD SUNGUSIA akizungumza na wanahabari leo jijini dar es salaam juu ya sakata hilo

Baada ya spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ANNA MAKINDA juzi wakati akifunga bunge kutoa kauli kuwa kuna baadhi ya wabunge waliopitishiwa  fedha wakati wa mdadala wa sakata la ESCROW kwa lengo la kusema uongo na kutetea wizi huo kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC wameibuka na kusema kauli hiyo sio ya kupuuzwa ni ya kuchunguzwa na kufahamu ukweli uko wapi.


Hoja hiyo imeibuliwa leo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini dar es salaam ambapo mkurugenzi wa wa utetezi na maboresho ya sera wa LHRC amesema kuwa hoja hizi kuwa kuna baadhi ya wabubge sio wasafi ni hoja nzito na hazifai kupuuzwa na kupitwa hivi hivi hivyo kituo chao kinazitaka mamlaka zinazohusika kuanza uchunguzi mara moja kujua kama kuna wabunge waliofanya kitendo hicho na wakipatikana waunganishwe katika sakata la ESCROW kwani nao ni wezi mali za watanzania.

 Mkurugenzi  wa utetezi na Maboresho ya Sera wa  LHRC HAROLD SUNGUSIA katikati,kulia kwake ni HAMIS MKINDI ambaye ni Afisa Program dawati la uangalizi wa Bunge na uchaguzi huku kushoto akiwa ni afisa programu dawati la uangalizi na serikali HUSSEN SENGU wote kutoka LHRC wakizungumza na wahabari leo jijini Dar es salaam

Aidha kituo hicho kimelitaka bunge kuichukulia kwa uzito wa aina yake kauli hiyo ya spika ili kama kuna baadhi ya wabunge waliochukua pesa ili kutetea wezi wa pesa za escrow wawachukulie hatua za kinidhamu wabunge hao.

Mbali na kauli aliyoitoa spika MAKINDA vile vile mbunge wa sikonge mh SAID MKUMBA akichangia katika mjadala ule pia alisikika akisema kuwa “Nasikia kuna watu wanapita pita wakigawa fedha mbona kwangu hawapiti”kauli ambayo inawapa wasiwasi wananchi kuwa kuna baadhi ya vitendo vya rushwa ndani ya bunge ili kuwaficha waovu ndani ya bunge.
Katika mjadala uliomalizika wiki jana ulishuhudia baadhi ya wabunge wakibishana kwa maneno huku wengine wakijaribu kutetea kile ambacho kinaitwa ni wizi wa wazi wa hela za account ya tegeta ESCROW huku wengine wakitaka wahusika wawajibishwe.

Katika hatua nyingine LHRC wameipongeza kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za serikali chini ya mwenyekiti wake mh ZITTO KABWE kwa kazi nzuri waliyoifanya hadi hapa walipofikia nikazi kubwa na wanapaswa kupongezwa kwa kuwafichuo watu wanaotafuna mali za watanzania.

No comments: