Sunday, December 14, 2014

PICHA ZA VITUKO VILIVYOTAWALA UCHAGUZI WA LEO TANZANIA

Watu hawa kama wanavyoonekana kwenye picha wamekamatwa na Polisi katika kituo cha kupiga kura mtaa wa Kisanga Kata ya Mwanga baada ya kuambiwa muda wa kupiga kura kuwa umekwisha wakaanza kutoa lugha za matusi kwa wasimamizi.PICHA ZOTE NA HABARI NI KWA MSAADA MKUBWA WA LHRC
Taarifa kutoka kwa Mwangalizi wetu Mr. Johnson Mbwambo kutoka Sumbawanga mjini ana ripoti:
Hatma ya vurugu kata ya kizutwe Sumbawanga mjini ofisi imechomwa moto na kuvunjwa na mpaka sasa watu wawili wameshikiliwa na polisi.
Hali ni kama unavyoiona kwenye picha.
Afisa wa kusimamia kituo cha kupigia kura mida ya saa sita mchana akiwa kafunga kituo kwa kukosa karatasi za kura. Akirudi ofisi za kata ya intonjanda wilaya ya uyui mkoa wa Tabora
Mtaa wa mkoani katika kata ya Kalangalala hawa ni wananchi waliokuwa wanasubiri Karatasi za kupiga kura na wamerudia mara ya tatu sasa, ni takribani ya wananchi 1000 hawakuweza kupiga kura mpaka mda wa kufunga upigaji kura saa 10 jioni.

Taarifa kutoka kwa
Mwanza, Geita

No comments: