Thursday, December 4, 2014

TAARIFA MAALUM KWA WATEJA WA NBC KUHUSU PESA ZAO

Kaimu Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jimmy Myalize (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo akitoa ufafanuzi wa tatizo la huduma za kibenki kupitia mtandao wa simu za mkononi (Mobile Banking) ambapo alisema licha ya tatizo hilo hakuna hata senti moja ya mteja wao iliyopotea. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Rukia Mtingwa.

Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Rukia Mtingwa (kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu tatizo lililojitokeza jana katika huduma zao za kibenki kupitia mtandao wa simu za mkononi (Mobile Banking) ambapo alisema licha ya wateja kutoona salio katika akaunti zao hakuna hata senti moja iliyopotea. Kushoto ni Kaimu Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC, Jimmy Myalize.
Baadhi ya wanahabari wakiwa kazini kurekodi mkutano wa menejimenti ya Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) jijini Dar es Salaam leo walipokuwa wakitoa ufafanuzi juu ya tatizo lililojitokeza jana Desemba 3, 2014 ambapo wateja wa benki hiyo walishindwa kutumia huduma za kibenki kupitia mtandao wa simu za mkononi (Mobile Banking).

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Uongozi wa NBC umebaini kuwepo kwa ujumbe kupitia mitandao ya jamii unayohusisha NBC na wizi wa fedha za wateja kwa kupita mashine za kutolea fedha (ATM). Ujumbe huo huo unahamasisha wateja kutoa fedha kwenye akaunti zao.
NBC tunapenda kuwafahamisha wateja wetu na umma kwa ujumla kwamba ujumbe huo hauna ukweli wowote. Papo hapo, matukio ya miamala ya wizi ni tatizo ambalo linaendelea kutafutiwa utatuzi na mabenki yote yaliyo chini ya Chama cha Mabenki Tanzania (TBA).
Tunapenda kuwahakishia wateja wetu na umma kwamba NBC inaendelea kudhamiria kuwapatia wateja wetu huduma bora na ya kisasa.

Imetolewa na uongozi

 

No comments: