Tuesday, December 2, 2014

WAFAHAMU KWA SURA ZAO NA SIFA ZAO WABUNGE WALIOSIMAMA KUWATETEA WATUHUMIWA WA ESCROW BUNGENI

                                  Huyu  ni   Amina   kisangi 

Huyu ni miongoni mwa wabunge waliochangia hoja ya ESCROW alhamisi jioni. Kwanza alijisahau kama pale alikuwa bungeni na kuishia kutoa mipasho inayoonyesha dhahiri kuwa alikuwa amelewa pombe!


Hata pale alipopewa taarifa na Deo Filikunjombe alisema haipokei na kuishia kusema eti Deo na wenzake wa PAC wachunguzwe kama wanafaa kuwepo CCM na kuwa kamati ya PAC ni UKAWA.


Baadhi ya maneno yake namnukuu "Mheshimiwa mwenyekiti, hawa watu wa PAC wachunguzwe kama ni wana CCM kweli.Hii ripoti ya PAC inaonyesha kuwa PAC ni UKAWA. Hizo pesa za ESCROW ni za IPTL wakila au wakigawa nyie inawauma nini?"


Huyu  ni   ASUMPTA  Mshana  ni  kati ya  wabunge  waliongoza  kwa  kuongea  mambo  ya  siyo  ya  msingi  ndani  wakati  wa   mjadala  wa   EScrow  yeye  bila  aibu  alisimama  na  kuwatetea  wezi  wa  Escrow  lakini  cha  kusikitisha  jimbo  analoongoza  la  NKENGE  huko  mkoani  kagera   ni    jimbo  ambalo  linakabiliwa  na  umasikini  mkubwa  sana  tena  wa  kutisha  lakini  yeye  bila  mshipa  wa aibu  anasimama  na  kuwatetea  watumiwa  waliyochota  mabilion   ya  fedha.wabunge  kama  hawa   ni  mizingo   mitupu  isiyokuwa  na
 faida  kwa  wananchi !!!!  wakati  wananchi  wake  wanakunywa  maji    machafu   huko  jimboni  kwake  yeye  yupo  bungeni  anatetea  wezi  kwa  nguvu  zote
  Anaitwa Mhe  Simbachawene  huyu   mbunge  alikuwa  anawtetea  watuhumia   kwa  kutumia akili  sana  na   wakati mwingine  kujenga hoja  ili watuhumiwa  waweze  kupenya  mfano  alikuwa  yupo   mstari  mbele  kupendekeza  maazimio  dhaifu  ambayo  yasinge  toa  adhabu  kali  kwa watuhumiwa  hao  wa  ESCROW  ,Tunaweza  kusema  kuwa  ametumia fani yake  ya  sheria  kutetea  wezi  wakati  wa  mjadala  wa  Escrow  ndani  ya  bunge

Huyu  anaitwa  Lusinde  ni  kati  ya  wabunge  waliongoza  kwa  kuongea  mambo  yasiyokuwa  na  maana  ndani  ya  bunge  kwa  kiswahili  kizuri  aliongoza  kwa  kuongea  pumba  zaidi  bila  kujali  kuwa  kulikuwa  na  watu  wengi  wanamtazama  siku  hiyo!!!!  huyu  LUSINDE  kwa  upande  fulani  alitetea  watuhumiwa   wa   ESCROW  kwa  kupitia  hoja  dhaifu  sana  bila  kuweka  uzalendo  mbele

Huyu  anaitwa  Richad   Ndasa  wakati  wananchi  wake  wanakabiliwa  na  umasikni  mkubwa  kutokana  na ufisadi  unaofanywa  na  baadhi  ya  viongozi  yeye  bila  mshipa   wa  aibu  anasimama  na  kuwatetea  mafisadi  bungeni!!!!!
 ndugu  wasomaji  wabunge  kama  hawa tusiwe  tunawapa  nafasi  ya  kwendaa  bungeni  kwasababu  hawana  faida  yoyote  kwa  wananchi  maana ya  kazi  ya  mbunge  ni  kutetea  wananchi  na  siyo kutetea  viongozi  wezi  kama   wanavyofanywa  hakika  wametia  aibu  sana  na  wamesaliti   wananchi  wao  ambao  ndiyo  masikini zaidi

No comments: