Wednesday, April 30, 2014

FAIDI MAAZETI YOTE YA LEO ALHAMIC TAREHE 1,MAY 2014


 

UKAWA ZANZIBAR INATISHA WAITEKA ZANZIBAR KIWANJA CHA KUBANDA MAITI LEO


WAKAZI WA KUTOKA KISIWA CHA TUMBATU WALIFIKA KWENYE UKAWA NA MABANGO YAOKIWANJA CHA KIBANDA MAITI


MUASISI MZEE NASORO MOYOALIFIKA KWENYE UKAWA


MAKAMU WA KWANZA WA ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARIFF HAMADI AKIKUMBATIANA KATIBU MKUU WA CHADEMA DR WILBROD SLAA KULIA KATIBU MKUU WA NCCRMAGEUZI MUSONA

BREAKING NEWS; AZAM FC YAIMALIZA YANGA--FRANK DOMAYO ASAINI MIAKA MIWILI AZAM LEO


KIUNGO mkabaji wa Yanga SC, Frank Domayo amesaini Mkataba wa miaka miwili kujiunga na mabingwa wapya wa Tanzania Bara, Azam FC jioni ya leo mjini Mbeya.
 
     Domayo amesaini Azam FC baada ya kumaliza Mkataba wake wa miaka miwili na Yanga SC, ambayo alijiunga nayo akitokea JKT Ruvu miaka miwi iliyopita.
 
Katibu wa Azam FC, Nassor Idrisa Mohamed ‘Father’ amesema katika kuendelea kukiimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao wamepiga hatua nyingine kwa kumsaini Domayo.

   “Kama unavyojua, baada ya kumaliza msimu vizuri tukiwa mabingwa wa Bara, tuligundua mapungufu kwenye kikosi chetu na kwa ushauri wa mwalimu wetu (Joseph Marius Omog) ndiyo tunayafanyia kazi,”alisema Father.
 
  Domayo anakuwa mchezaji wa wa pili ndani ya siku mbili kusajiliwa na Azam FC kutoka mabingwa wa zamani na mabingwa wa kihistoria Tanzania Bara, Yanga SC baada ya jana klabu hiyo kumsaini mshambuliaji Mrundi Didier Kavumbangu.   

MAJAMBAZI WAVAMIA OFISI ZA GAZETI LA MAJIRA,WAKOMBA KOMPYUTA ZOTE

Na Karoli Vinsent
      
          Kundi la watu wanaosadikiwa kuwa Majambazi wamevamia  makau makuu ya ofisi za Gazeti la majira,zilizopo Jijini Dar Es Salaam na Kuiba Kompyuta zilizopo kwenye Chumba cha Habari.
        
         Kwa Mujibu wa Waandishi wa Gazeti hilo waliozungumza na Mwandishi wa Mtandao huu ambao hawakutaka kutajwa Majina yao kwenye Mtandao huu wakisema wao sio wasemaji wa Gazeti hilo,walithibitisha wezi kulivamia Gazeti hilo na kuiba vitu vyenye Thamani isiojulikana.

SERIKALI YAENDELEA KUTOA ONYO KALI KWA GAZETI LA MAWIO,SASA WAWATAKA KUFWATA MAAGIZO YALIYOTOLEWA,LA SIVYO----

Na Karoli Vinsent
        
      MKURUGENZI wa Idara ya Habari MAELEZO amelitaka Gazeti la Mawio kufuata maagizo aliyatoa ,Lasivyo wakiendelea kukaidi Basi wasubili hatua kali zaidi.
        
       Kauli  hiyo ya mkurugenzi wa idara hiyo Asah Mwambene,imekuja siku chache kupita baada ya Gazeti la mawio kwa kupitia mkurugenzi wake kusema kwamba hawajapata barua kutoka kwenye Idara hiyo ya Habari maelezo iliyowataka waombe Radhi na kusema hawana barua hiyo ili wao waweze kuchukua  hatua  hiyo wanayoitaka.
          

KATIBU MKUU WA FIFA KUWASILI NCHINI KESHO

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Jerome Valcke anawasili nchini kesho (Mei 1 mwaka huu) ambapo atafungua semina ya mawasiliano kwa nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Valcke ambaye atafuatana na maofisa wengine saba wa FIFA baadaye kesho hiyo hiyo (Mei 1 mwaka huu) atakuwa na mkutano na waandishi wa habari. Mkutano huo utafanyika saa 4 kamili asubuhi kwenye hoteli ya Double Tree by Hilton iliyopo Oysterbay, Dar es Salaam.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

KUWA WA KWANZA KUFAHAMU HUDUMA MPYA ILIYOZINDULIWA LEO NA BENKI YAKO YA NMB

Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NMB,Mark Wiessing
  Na Karoli Vinsent
        BENKI  ya NMB katika kuonyesha inawajali wateja wake sasa Imezindua huduma itakayowafanya Wateja wake kufurahia Ubora wa Benki hiyo,Baada ya Kuzindua Huduma mpya ijulikanayo “JIHUDUMIE”
         
        Akizindua Huduma hiyo,leo hii Jijini Dar Es Salaam, mbele ya Waandishi wa Habari na Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NMB,Mark Wiessing alisema Kampeni inayojulikana “Jihudumie ni huduma mpya ambayo itakayowafanya Wateja Wa Benki hiyo kufurahia ubora na Ufanisi.

Tuesday, April 29, 2014

MAGAZETI KADHAA YA LEO JUMATANO APRIL 30,2014 YAPO HAPA


REAL YAIKUNGUTA ‘ BAYERN MUNICH, YAITANDIKA 4-0 NA KUIVUA UBINGWA WA ULAYA

Tumewaangamiza; Ronaldo kushoto akishangilia baada ya kufunga bao la tatu lililoikata maini kabisa Bayern Munich
KWISHA habari yao! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kuhusu Bayern Munich baada ya usiku huu kutandikwa mabao 4-0 na Real Madrid katika Nusu Fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa nyumbani kwao, Allianz Arena mjini Munich, Ujerumani.
All sewn up: Cristiano Ronaldo scores with a free-kick to complete a 4-0 victory for Real Madrid against Bayern
Job done: Real Madrid are through to this year's Champions League final after beating Bayern Munich    Maana yake- Bayern wamevuliwa ubingwa wa Ulaya kwa kipigo cha jumla cha mabao 5-0, baada ya awali kuchapwa 1-0 Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid katika Nusu Fainali ya kwanza na Real inaingia Fainali kwa mara ya kwanza baada ya miaka 12, ambako itakutana na ama Chelsea au majirani zao Atletico Madrid ya Hispania pia.On the attack: Cristiano Ronaldo fires the ball past Bayern goalkeeper Manuel Neuer to score Real's third
     Shujaa wa Real alikuwa ni Sergio Ramos aliyefunga mabao mawili, la kwanza dakika ya 16 pasi ya Luka Modric na la pili dakika ya 20 pasi ya Pepe kabla ya Mwanasoka wa Bora Dunia, Cristiano Ronaldo kumaliza kazi kwa kufunga mabao mawili dakika ya 34 pasi ya Gareth Bale na dakika ya 90.
       Kipindi cha pili, Bayern inayofundishwa na kocha Mspanyola, Pep Guardiola ilijikaza na kukataa kuruhusu mabao zaidi, hivyo kukubali kutema taji kwa kichapo cha 5-0. 
      Real inayofundishwa na Mtaliano Carlo Ancelotti sasa inasubiri mshindi wa jumla wa Nusu Fainali ya pili kesho Uwanja wa Stamford Bridge kati ya wenyeji Chelsea na Atletico Madrid, baada ya sare ya O-O katika mchezo wa kwanza Hispania ili kukutana nayo katika fainali Jumamosi ya Mei 24, mwaka huu Uwanja wa Sport Lisboa mjini Benfica Ureno.
     Kikosi cha Bayern Munich kilikuwa: Neuer, Lahm, Dante, Boateng, Alaba, Schweinsteiger, Kroos, Ribery/Gotze dk73, Muller/Pizarro dk73 na Robben, Mandzukic/Martinez dk46.
   Real Madrid: Casillas, Carvajal, Pepe, Ramos/Varane dk75, Coentrao, Alonso, Modric, Di Maria/Casemiro dk84, Ronaldo, Bale na Benzema/Isco dk80.

MTANGAZAJI MAARUFU TSAKA SSALI AMTEBELEA MH LOWASA OFISINI KWAKE LEO

http://1.bp.blogspot.com/-YwqOFrY1mc0/U1-35jghU_I/AAAAAAAFeAY/jnjP-GExX3k/s1600/photo+3.JPG
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa (kushoto) akifurahi jambo wakati akiwa katika mazungumzo na mtangazaji maarufu wa Kituo Cha runinga Cha Serikali ya Marekani (VOA),Tshaka Ssali.
http://2.bp.blogspot.com/-SEqUbhvnVg8/U1-35SjdnzI/AAAAAAAFeAU/OM-EYd9QCiA/s1600/photo+1.JPG

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa (kushoto) akizungumza na mtangazaji maarufu wa Kituo Cha runinga Cha Serikali ya Marekani (VOA),Tshaka Ssali aliemtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.Ssali ambaye amejijengea umaarufu duniani kwa kuwahoji viongozi maarufu hususan wa Afrika, alimtembelea Mh Lowassa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje.

MALAWI KUWASILI MEI 1 KUIVAA STARS

malawi-teamTimu ya Taifa ya Malawi (Flames) inatarajiwa kuwasili nchini Mei 1 mwaka huu kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Mei 4 mwaka huu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

         Flames yenye msafara wa 31 utakaoongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Mpira wa Miguu cha Malawi (FAM) utaingia Mbeya kwa usafiri wa barabara. Wachezaji katika msafara huo ni 20.

        Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ikiwa chini ya Kocha mpya, Mart Nooij tayari ipo jijini Mbeya kujiwinda kwa mechi hiyo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya mashindano dhidi ya Zimbabwe itakayochezwa jijini Dar es Salaam kati ya Mei 16 na 18 mwaka huu.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

DILI LIMEKAMILIKA! DIDIER KAVUMBAGU AMWAGA WINO AZAM FC

kavumbagu3                       Na Baraka Mpenja , Dar es salaam

 DIDIER Kavumbagu kwaheri Yanga. Hii ni baada ya mchana wa leo kusaini mkataba wa mwaka mmoja na mabingwa wapya wa ligi kuu soka Tanzania bara, klabu ya Azam fc.

 Taarifa hii imethibitishwa na meneja wa Azam fc, wana Lambalamba, Jemedari Said.

“Kavumbagu tumemalizana nae na amesaini rasmi mkataba wa mwaka mmoja, so tutakuwa nae msimu ujao kwenye kampeni ya kutetea ubingwa wetu pamoja na michuano ya klabu bingwa ya Afrika,” alifunguka Jemedari
kavumbangu na nassor
   Mshambuliaji huyo hatari na nahodha wa timu ya Taifa ya Burundi ameamua kumwaga wino Azam baada ya Uongozi wa Yanga kusuasua kumpa mkataba mwingine baada ya ule wa miaka miwili kumalizika.

UJANJA UJANJA WA TAASISI ZA MIKOPO NCHINI WAWAKERA LHRC,SASA WAIGEUKIA SERIKALI,WATOA OMBI NZITO,SOMA HAPA

Kaimu mkutugenz wa uradi huo kutoka LHRC wakili FLAVIANA CHARLES akizungumza na wanahabari mapema leo jijini dar es salaam juu ya mradi huo
Kituocha sheria  na haki za binadamu Tanzania LHRC kimeitaka serikali kuunda mamlaka rasmi ya kusimamia taasisi zinazijuhusisha katika kutoa mikopo kwa wajasiriamali nchini ili zitoe mikopo yenye riba nafuu na tija kwa watanzania tofauti na sasa ambapo taasisi nyingi za utoaji wa mikopo zimekuwa zikutoa mikopo kwa riba kubwa ambayo imekuwa ikiwafanya watanzania kukata tamaa katika kupata mikopo hiyo.
        
           Hayo yamesemwa leo jijini dar es salaam na kaimu mkurugenzi wa mradi maalum wa kazi za staha unaoendeshwa na kituo hicho wakili  FLAVIANA CHARLES  wakati akizungumza na wanahabari kuhusu mradi unaoendeshwa na kituo  hicho  kwa kushirikiana na shirika la ujerumani linalohusika na idadi ya watu la DSW mradi wenye lengo la kuendeleza miradi ya kazi za staha kwa wananchi walioajiriwa katika sekta zisizo rasmi.

Mmoja wa watanzania anayenufaika na mradi huo BAKARI ALLY MOHAMED akizungumza na wanahabari

   Wakili FLAVIANA amesema kuwa baadhi ya taasisi zimekuwa sio rafiki kwa wajasiriamali ambapo wamekuwa wanalenga zaidi kuwafilisi wajasiriamali hao kwa kutoa mikopo yenye riba kubwa na hatimaye kuuza vitu ambavyo watu wanakuwa wameweka kama dhamana jambo ambalo limekuwa likiwafanya watu kushindwa kwenda kukopa katika taasisi hizo ambapo ameitaka serikali kuhakikisha inaunda mamlaka maalum ya kushughulikia tatizo hilo

         Aidha amesema kuwa tasisi nyingi za utoaji wa mkopo zimekuwa hazijasajiliwa kisheria jambo ambalo limekuwa likileta  matatizo pale ambapo linapowakopesha watu na mwisho wa siku kubaini kuwa wametapeliwa na taasisi hizo,ambapo amesema kuwa kesi zaidi ya 26 zimeripotiwa katika kituo hicho kwa mwaka huu juu ya utapeli na ukiukwaji wa sheria unaofanywa na taasisi hizo za mikopo,ambapo wengi wanalenga tu kutaifisha tu mali kwa kuweka masharti ya ujanja ujanja ujanja.

Wanahabari mbalimbali wakisikiliza kwa makini mapema leo

Mradi huo unaoendeshwa na kituo hicho cha sheria umekuwa ukifadhiliwa na umoja wa ulaya EU ambapo mradi huo umekuwa ukiendeshwa katika halmashauri tatu zilizopo kanda ya kaskazini ambazo ni MERU,ARUSHA NA BABATI,