Monday, June 30, 2014

MAGAZETI YOTE YA LEO JUMANNE JULY 01,2014 YANAPATIKANA HAPA,HABARI,MICHEZO NA BURUDANI


breaking newzz--PICHA--NAIBU KATIBU MKUU CUF BARA ANUSURIKA KATIKA AJALI

Naibu Katibu m kuu mpya wa CUF pia Mbunge wa viti Maalum Magdalena Sakaya akimshukuru Mungu baada ya kunusurika katika ajali na Lori kwenye makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere Dar leo jumatatu ambapo ajali hiyo imetokea,magdalena sakaya amechaguliwa juzi kushika nafasi hiyo ya unaibu katinu mkuu wa CUF baada ya JULIUS MTATIZRO kutolewa katika nafasi hiyo

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA KAMPUNI YA VIETTEL IKULU

TCRA YAKABIDHIWA CHETI CHA UBORA NA TBS LEO



Na Karoli Vinsent

        KATIKA kuonyesha ubora kwa Watanzania mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA) imetakiwa kuongeza juhudi katika kuboreshaji sekta hiyo,  baada ya kukabidhiwa cheti cha kiwango cha kimataifa na Shirika la Viwango Duniani.
 
        Cheti  hicho kilikabidhiwa jijini Dar es Salaam leo, mbele ya wafanyakazi wote wa TCRA na Mkaguzi wa kimataifa kutoka Uingereza Andrew Rowe na kumpa Mkurugenzi wa TCRA Prof. John Mkoma.

    Akipokea cheti hicho, Profesa Nkoma, alisema kuwa kutokana na utendaji kazi wa mamlaka hiyo katika kudhibiti mawasiliano nchini, ndio sababu iliyopelekea kupata cheti hicho kinachoipa heshima Tanzania.

Saturday, June 28, 2014

KAULI YA ADEN RAGE KUELEKEA UCHAGUZI WA SIMBA SC HII HAPA!

http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2014/06/rage.jpg
SIMBA SC inatarajia kufanya mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Klabu Kesho Jumapili (Juni 29 mwaka huu), katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Kuelekea katika mkutano huo utapata Rais mpya, makamu wa Rais na wajumbe wapya wa kamati ya utendaji kwa mujibu wa katiba mpya Simba, mwenyekiti wa klabu hiyo, Alhaj Ismail Aden Rage awewatakia kila la heri wanachama wote katika uchaguzi huo.

Akizungumza na  Mtandao huu mchana huu, Rage amesema ana imani uchaguzi utafanyika kwa amani na utulivu ili klabu ipige hatua.

KAMPENI SIMBA ZAKAMILIKA KWA AINA YAKE,WAMBURA AJITKEZA KUMPIGIA KAMPENI TUPA,AVEVA NAYE AAHIDI MAKUBWA SIMBA.PICHA ZOTE HAPA

Mgommbea urais wa simba bw EVANCE AVEVA leo akihitimisha kampeni zake jijini dar es salaam ambapo amewaahidi mambo makubwa sana wana simba kuhakikisha simba inakuja katika ujio mwingine tena,ikiwa ni pamoja na kuwahakikishia wana simba kuwa watapata uwanja wao wenyewe wa kisasa kwa muda mfupi sana.pamoja na kuahidi kuifanya simba kuwa timu ya kimataifa tofauti na sasa

Katika upande mwingine mgombea aliyekuwa anagombea na baadaye kufutwa katika uchaguzi huo bw MICHAEL WAMBURA leo amejitokeza mbele ya wanachama wa simba akimuunga mkono mgombea mwingine wa urasi hapo simba bw ANDREW JULIUS TUPA ambaye anapambana na EVANCE AVEVA,ambapo bw WAMBURA ameataka wanasimba kutokumchagua mtu kutokana na pesa zake bali waitangulize simba kwanza kwa kumchagua TUPA na JULIO kuwa viongozi wapya wa timu hiyo katika uchaguzi ambao utafanyika kesho jijini Dar es salaam

TIGO YAWEZESHA MAFUNZO YA TECHNOHAMA KWA WASICHANA JIJINI DAR ES SALAAM

Badhi ya wasichana kutoka shule mbalimbali jijini dar es salaam wakiwa katika mafunzo hayo
 Wasichana nchini Tanzania wamepewa changamoto ya kujiendeleza katika masomo ya technohama ili kuweza kuongeza upeo wao katika matumizi ya computer na kuweza kuchangia katika maendeleo ya kijamii kwa ujumla nchini Tanzania.
 Changamoto hiyo  imetolewa leo jijini Dar es salaam na meneja wa uwajibikaji kwa jamii kutoka kampuni ya tigo Tanzania Bi WOINDE SHISAEL wakati akizungumza na wanafunzi wa kike wapatao 100 kutoka shule za secondary mbalimbali waliokuwa katika mafunzo maalum ya technohama  yaliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali linalijihusisha na technohama APPS AND GIRLS ambao pia ni mmoja wa washindi wa program maalum ya wajasiriamali wa kijamii TIGO REACH  FOR CHANGE
 Bi WOINDE amesema kuwa “mkakati wa huduma ya uwajibikaji walionao tigo ni kuwezesha jamii kupitia matumizi ya vyombo vya kidigital” ambapo ametoa rai kwa wanawake na wasichana wote kujitokeza zaidi kujiendeleza kidigital kupitia technohama huku akiongeza kuwa ni dhana potofu kuwa wasichana hawawezi kufanya vizuri katika technohama wakati wana nafasi kubwa sana.
Aidha amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga wasichana tu kwa sababu wanawake wengi wameonekana kuwa nyuma sana katika kujihusisha katika technohama.
 Meneja wa uwajibikaji kwa jamii kutoka kampuni ya tigo Tanzania Bi WOINDE SHISAEL
Muasisi wa APPS AND GIRLS bi CAROLYNE  EKYARISIIMA
Naye muasisi wa APPS AND GIRLS bi CAROLYNE  EKYARISIIMA ampaye pia ni mmoja wa washindi wa dola 25,000 za kimarekani kutoka tigo reach for change kwa mwaka huu amesema kuwa mafunzo haya yanazingatia kwapatia wasichana utaalam katika kutengeneza tovuti kama njia moja wapo ya kuwahamasisha katika maswala ya technohama.

Shule zilizohudhuria mafunzo hayo ni pamoja na kisutu,jangwani,na kibasila ambapo mafunzo hayo ni ya simku moja.

Friday, June 27, 2014

EXCLUSIVE--HUYU NDIYE MCHEZAJI WA YANGA TOKA BRAZIL (COUNTINYO) AWASILI DAR KWA MBWEMBWE

Afisa Haari wa Young Africans Bw Baraka Kizuguto (kushoto) akiwa pamoja na mshambuliaji mpya Andrey Coutinho mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa JK Nyerer leo
Kiungo mshambuliaji mpya wa timu ya Young Africans SC  Andrey Marcel Ferreira Coutinho amewasili mchana wa leo jijini Dar es salaam akitokea kwao nchini Brazil tayari kabisa kwa kuanza kazi ya kuwatumikia wana Wanajangwani katika msimu wa 2014/2015.
Countinho amewasili mchana kwa shirika la Ndege la Afrika Kusini (South African Airways) akitoka jijini Sao Paul ambapo safari ya kuja Tanzania imemkchukua takribani masaa 20 tokea katika Mji wa Berem ambapo ndipo anapoishi.

  Mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege  wa JK Nyerere, Coutinho alipokelewa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Bw. Mohamed Bhinda ambaye alimuongoza kuwasilimia washabiki na waaandishi wa habari walijitokeza kumlaki.

TIZAMA VIDEO HII--KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI AWASHAMBULIA KAFULILA NA ZITTO,ASISITIZA KAFULILA NI TUMBILI TU


      SAKATA linalohusu kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), limechukua sura mpya baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, kuwashambulia kwa maneno makali, wabunge wawili Zitto Kabwe wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) na David Kafulila wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi).

HABARI24  likuwapo wakati Maswi akitumia maneno makali kwa kuyarudia, akikejeli nyaraka zinazotajwa kuwa ni ushahidi wa jinsi IPTL ilivyouza hisa zake na fedha kutolewa kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika akaunti maalumu ya pamoja (Escrow), akisema nyaraka hizo ni karatasi za kufungia vitumbua zinazosambazwa na wabunge hao aliowaita “washenzi”.
Kauli hiyo ya Maswi imekuja siku mbili tu baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema kushambuliana na Kafulila kwa maneno makali malumbano yao yakianzia ndani ya Bunge na kuendelea walipotoka, kila mmoja akiamini kauli aliyoitoa ilikuwa ni sahihi.
Werema alimfananisha Kafulila na tumbili na yeye kumuita mwanasheria huyo mwizi. Tumbili ni mnyama wa porini wakati mwizi ni mtu anayetenda uhalifu kwa kuchukua kitu au mali isiyo yako.

PATA NAFASI YA KUSOMA KAULI TANO KALI ALIZOZUNGUMZA KOCHA MPYA WA YANGA MAXIMO MBELE YA WANAHABARI LEO

Kocha MAXIMO akizungumza na wanahabari makao makuu ya timu hiyo jijini Dar es salaam
Kocha mpya wa timu ya yanga ya dar es salaam mbarazili MARCIO MAXIMO leo amezungumza na wanahabari kwa mara ya kwanza jijini dar es salaam ambapo katika mambo mengi aliyoyazungumza ameonekana kuwaahidi mambo makubwa mashabiki wa timu ta yanga.

Naomba ninukuu kauli zake tano ambazo amezitoa na zikaonekana kuwafurahisha wapenzi wa timu ya yanga na viongozi wake 

1-Nimekuja kuifanya timu ya yanga kuwa kama timu ta TP MAZEMBE ya congo,nadhani nina uwezo huo na nadhani kwa kushirikiana na viongozi wa timu hii tutaweza.

2-Nataka kuipeleka yanga level za kimataifa zaidi tofauti na sasa

3-Nataka kutengeneza timu ya yanga kuwa timu yenye upinzani mkubwa tanzania na barani africa kwa ujumla

4-Nataka kuifanya yanga iwe timu yenye mvuto na ifike kipindi timu hii wazungu na wachezaji wa kutoka ulaya kuja kucheza hapa yanga na kwa kuanza hilo naanza kwa kumleta mchezaji mzuri toka Brazil anaitwa ANDERY CONTINYO ambaye atawasili leo jioni.

5-Swala la kaseja ni kwamba sina bifu na kipa wa yanga JUMA KASEJA nampenda sana yaliyopita yamepita sasa tugange yajayo tuwaze kuijenga timu yetu.

MAXIMO ATAKUWA AKIJIZOLEA KITITA CHA MILION 19 KWA MWEZI AKIWA YANGA

Thursday, June 26, 2014

MAGAZETI YA LEO IJUMAA - JUNI 27 YAPO HAPA

1_fbc8c.jpg
2_c95bd.jpg
3_43217.jpg

MAJONZI: MWILI WA SISTA ALIYEPIGWA RISASI NA MAJAMBAZI UBUNGO WAAGWA JIJINI DAR-R,I,P

PICHA  ZOTE KWA UDHAMINI WA GLOBAL PUPLISHER

Masista wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Sista Cresensia Kapuli aliyeuawa kwa kupigwa risasi na majambazi Juni 23, 2014.

MICHEZO--FAIDI PICHA ZA MAXIMO ALIVYOTUA YANGA LEO--ZIKO HAPA

Kocha mpya wa timu ya yanga ya Dar es salaam leo ametua jijini dar es salaam kwa ajili ya kuanza kibarua chake cha kuinoa club hiyo ya Jangwani 

breaking newzz---TUNDU LISSU AVUNJA UKIMYA WA CHADEMA KWA MARA YA KWANZA ATOA YA MOYONI KUHUSU KINACHOENDELEA CHADEMA,APANGUA HOJA ZA WAKINA YONA--USIKOSE IPO HAPA PEKEE

                                                          Na Karoli Vinsent

       SIKU moja kupita Baada ya watu, wanaojiita Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,kuandamana mpaka kwenda kwa Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali “CAG” pamoja na kwa Masajili wa vyama vya kisiasa nchini,kuwashtaki viongozi wa Juu wa chama hicho kwa madai ya matumizi mabaya ya Fedha.

       Nae,mwanasheria mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu,ameibuka na kuwataka wanachama wa chama hicho kuwapuuza watu hao,kwa madai  kuwa chadema iliwafukuza uanachama na sasa hivi wanatumiwa  na Viongozi wa kutoka chama cha Mapinduzi ili kukidhofisha chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

BARAKA ZASHUKA PALESTINA HOSPITALI --FARIDA FOUNDATION YATOA MISAADA HOSPITALI YA PALESTINA SINZA NA KWA WALEMAVU ENEO LA UBUNGO DARAJANI

Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina Dk Hugoline Mselle akipoke Ndoo zitakazotumika kwa ajili ya kuhifadhia uchafu katika Hospitali hiyo,ambazo zilitolewa kama Msaada na Farida Foundation

 Mkurugenzi wa Farida Foundation akikabidhi moja ya msaada kwa kaimu Mganga mkuu wa Hospitali ya Palestina Dk Hugoline Mselle,Huku wafanyakazi wengine wa Hospitali hiyo wakishuhudia.
 Bi Farida Abdul Akikabidhi bandeji kwa ajili ya kufungia wagonjwa kwa Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina Dk Hugoline Mselle


 Bi Farida Abdul akimuonyesha kaimu Mganga mkuu wa Hospitali ya Palestina Dk Hugoline Mselle Vifaa ambavyo vimeletwa kama msaada kwenye Hospitali hiyo.Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Viti vya magurudumu vitatu ambavyo vitasaidia kubebea wagonjwa,Bandeji za kufungia vidonda,Ndoo za kuwekea taka,na vinginevyo.

TIGO NA HUAWEI WAFANYA MAAJABU MENGINE MUDA HUU,SASA "SMARTPHONES" BEI SAWA NA BURE,NUNUA URUDISHIWE HELA YAKO

Mkuu wa kitengo cha internent wa TIGO  bw DAVID ZACHARIA akizungumza na wanahabari muda mchache uliopita
 Kampuni ya mawasiliano ya TIGO Tanzania leo imetangaza kuingia katika ushirikiano na kampuni ya technologia ya HUAWEI ili kuwawezesha wateja wa kampuni hiyo ya simu nchini kuweza kupata simu za kisasa "SMARTPHONES " kwa bei nafuu.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam muda mchache uliopita mkuu wa kitengo cha internent wa tigo bw DAVID ZACHARIA amesema kuwa ushirikiano huo unawapa   wateja fursa ya kuweza kumiliki simu aina ya HUAWEI  Y330 kwa bei ya punguzo ya shilingi 130,000 na HUAWEI Y530 kwa shilingi 195,000 tu.
Ndio aina ya simu ambazo zitakuwa zinauzwa
 Kwa mujibu wa Bw ZACHARIA wanunuzi wa simu hizi mbili watapata kifurushi cha bure cha thamani ya shilingi 30,000 katika mwezi wa kwanza baada ya kununua ambapo kifurushi hicho kinajumuisha dakika 600 za muda wa maongezi,sms 8000,za bure na 1.5 GB za  data za internent.na katika miezi sita inayofuata mteja atakayenunua kifurushi cha mwezi cha shilingi 15,000 atarudishiwa kiwango sawa na alichonunulia,ambapo amesema   inamaanisha kuwa baada ya baada ya miezi sita mteja atakuwa amerudishiwa zaidi ya shilingi 120,000.
Akizungumza katika mkutano huo wa waandhishi wa habari meneja chapa wa kanda ya Africa  mashariki na kusini toka HUAWEI  AZALEA DU amesema kuwa HUAWEI  Y 330 ni simu za kisasa zinazolenga vijana ambapo kampuni yake inafarijika sana kuwapatia wateja wa tigo fursa ya kuitumia.
Mwakilishi kutoka HUAWEI akizungumza na wanahabari katika makao makuu ya TIGO TANZANIA
Ofa hii inakuja ikiwa ni miezi michache tangu kampuni ya tigo kutangaza kuwapa wateja wake uwezo wa kutumia FACEBOOK buree kabisa kwa lugha ya Kiswahili ambapo wateja wake wameonekana kuifurahia sana .

Wednesday, June 25, 2014

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS 26.06.2014


HII NDIO TAARIFA RASMI KUHUSU HABARI YA KIFO CHA MH SHUKURU KAWAMBWA


Kutokana na baadhi ya mitandao ya kuijamii muda mchache uliopita kuandika habatri juu ya kumuhusisha na kifo mbunge Shukuru kawambwa mtandao huu umezungumza na watu wa karibu wa waziri huyo na kudai kuwa shukuru kawambwa ni mzima wa afya na habari zinazoenea ni uzushi mkubwa na hazina ukweli wowote.

           Na hii ndio mesege kutoka Kwa mbunge RIDHIWAN KIKWETE juu ya uvumi huo.

    Ndg Watanzania,WanaBagamoyo na wapenda maendeleo, kwa niaba ya CCM-Bagamoyo na Ofisi ya Mbunge-Jimbo la Bagamoyo napenda kuleta kwenu Masikitiko yetu kwa niaba ya Chama na Familia ya Mheshimiwa Mbunge Shukuru Jumanne Kawambwa kutokana na Usumbufu ambao umesababishwa na habari zinazoenezwa Mitandaoni kwamba Mheshimiwa Kawambwa amekumbwa na Umauti akiwa njiani anaelekea Mwanza.

                UKWELI
        Mheshimiwa Shukuru Jumanne Kawambwa yupo Nchini Canada Akitimiza majukumu yake. Hivyo Watanzania na wana Bagamoyo mnaombwa radhi kwa usumbufu uliotokea na kwamba Mheshimiwa Mbunge yuko na Afya njema na utekelezaji wa Majukumu unaendelea kama kawaida.
Ndg.Ridhiwani Kikwete (Mnec)
Mbunge -Chalinze


BREAKING NEWZZ--UCHAGUZI CUF WAMALIZIKA LIPUMBA NA SEIF WAFUNIKA TENA WAPITISHWA KWA KURA ZAIDI YA ASLIMIA 90,CUF WASEMA BADO WANAWAAMINI SANA,FAIDI PICHA HAPA

Profesa LIPUMBA akipongezwa na aliyekuwa mpinzani wake katika uchaguzi huo baada ya matokeo kutangazwa muda huu hapa katika ukumbi wa ubungo plaza jijini Dar es salaam
 Uchaguzi mkuu wa cjhama cha wananchi CUF umemalizika hapa jijini dar es salaam ambapo aliyekuwa mwenyekiti profesa IBRAHIM HARUNA LIPUMBA amechaguliwa tena kukiongoza chama hicho kwa miaka mingine mitano baada ya kupata kura 659 kati yakura 689 zilizopigwa ambapo ni ushindi wa zaidi ya 95% ya kura zote ambapo aliyekuwa mpinzani wake pekee katika uchaguzi huo mh CHIEF YEMBA amepata kura 30 sawa na aslimia 4.3% ya kura zote zilizopigwa.

Katika nafasi ya makamu mwenyekiti mgombea alikuwa mmoja ambaye ni JUMA DUNI HAJI ambaye katika kura 667 zilizopigwa amepata 662 sawa na aslimia 99.25 ya kura zote na kutangazwa rasmi kuwa makamu mwenyekiti wa chama hicho.

Aidha katika nafasi ya katibu mkuu wa chama hicho kama kawaida mgombea alikuwa mmoja ambaye ni MH SEIF SHARIF HAMAD ambaye katika kura 678 zilizopigwa amejinyakulia kura 675 sawa na aslimia 99.5% ya kura zote zilizopigwa hivyo kutangazwa rasmi kuwa katibu mkuu wa chama hicho akiendelea kushika nafasi aliyokuwa anaiongoza.

Sura za furaha baada ya kurudi tena katika madaraka yao waliyokuwa nayo hapo awali kabla ya mchakato wa uchaguzi


Picha mbili ni mwenyekiti mpya wa CUF profesa LIPUMBA akiwashukuru wajumbe wa mkutano huo ambao ndio waliokuwa wapiga kura kwa kumpa kura za ndio na kumrejeshea tena kiti chake cha uenyekiti wa chama hicho


BREAKING NEWZZ--KINACHOENDELEA KATIKA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA CUF-PICHA NNE MUHIMU ZIPO HAPA

 Chama cha wananchi CUF muda huu kinanfanya uchaguzi wa viongozi wakuu wa chama chao ambapo wagombea mbalimbali wamejitokeza kugombea nafasi hizo.

Katika nafasi ya uenyekiti wa chama hicho taifa wagombea watatu wamejitokeza kugombea nafasi hiyo ambao kwa majina ni aliyekuwa mwenyekiti wake pr LIPUMBA,MH CHIEF LUTAYOSA YEMBA,pamoja na mh MBEZI ADAM BALARI,huku nafasi ya makamu mwenyekiti na katibu wakijitokeza wagombea mmoja mmoja ambao ni katika umakamu wa mwenyekiti amejitokeza mh JUM,A DUNI HAJI,na katika nafasi ya katibu mkuu wa chama hicho amejitokeza mh SEIF SHARIF HAMAD ambaye alikuwa ameshikilia nafasi hiyo.

Matokeo ya uchaguzi huu yatakujia baadae hapa hapa katika mtandao wenu
Wagombea wa uenyekiti wa chama hicho PROFESA IBRAHIMU LIPUMBA akiwa  anajadili jambo na mgombea mwezake kabla ya wajumbe kuamua nani wampe tena uenyekiti wa chama hicho cha CUF leo muda huu

Uchaguzi wa kuwapata wawakilishi katika mkutano mkuuu wa chama hicho tayari umemalizika na tayari wajume hawa ndio wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha wananchi CUF waliochaguliwa muda huu jijini Dar es salaam

Aliyekuwa katibu mkuu wa CUF  SEIF SHARIF HAMAD akiomba kura kupata nafasi hiyo kwa mara nyingine tena muda huu katika uchaguzi mkuu wa chama hicho unaoendelea muda huu ndani ya ukumbi wa ubungo plaza jijini dar es salaam

EXCLUSIVE--WALIOMKASHFU MBOWE NA VIONGOZI WA CHADEMA JUU YA UFISADI WAJIBIWA--SOMA TAMKO LOTE HAPA


 Ndugu wanahabari,wanachama na wapenzi wa chama cha Demokrasia na maendeleo kanda ya magharibi na nchini kwa ujumla.

       Tumewaalika leo hii ili kuja kuweka sawa kwa kile kinachoendelea kwa baadhi ya wanachama wa CHADEMA ambao hawana mapenzi mema na chama kwa kile walichokitoa mbele ya wanahabari huku wakiwa wamejivika vyeo ambavyo ama havipo au wamekaimishwa au wamekwishavuliwa hapo awali. Taarifa iliyopewa kichwa 

    ”TAARIFA YA WAJUMBE WA BARAZA KUU NA MKUTANO MKUU WA CHADEMA KWA UMMA” iliyotolewa tarehe 23/06/2014 katika Hoteli ya Lamada iliyopo jijini Dar es Salaam.

                              Ndugu wanahabari.
Mtindo huu umezuka sana hivi karibuni ambao kwa namna moja ama nyingine unaratibiwa na viongozi wa CCM kwa mgongo wa waliokuwa viongozi wa CHADEMA ambao kwa sasa ni viongozi wa chama kipya cha Alliance for Change and Transparence – Tanzania (ACT - Tanzania). Tunasema ni viongozi wa ACT - Tanzania kwa sababu ushahidi wa kimazingira, wa kimuonekano, wa kimwenendo na vidhibitisho visivyokuwa na shaka vipo!